2. Kunywa maji kwa wingi.(glasi 8-10 kwa siku)
Maji ni kinywaji asilia na muhimu sana kwa afya yako, usipende kunywa sana soda au vinywaji vyenye sukari nyingi. Wengi wetu hupendelea kunywa zaidi chai au soda (vinywaji baridi kama Cocacola, Pepsi, Redull nk). Vinwaji vingi jamii ya soda vina gesi ambayo sio nzuri kwa afya yako kwasababu huongeza uwezekano wa mtu kupata vidonda vya tumbo. Kunywa maji lita 2 kwa siku na pia unashauriwa kunywa maji dakika 10-20 kabla ya kula chakula au nusu saa kuendelea baada ya kupata chakula.Ni kwasababu utakapokunywa maji kabla ya chakula itakusaidia kutokula chakula kingi kupita kiasi kwakuwa utakuwa umeshiba hivyo utaepukana na kula sana ambapo kunaweza kukuongezea uzito wa mwili na hasa kunenepa.
Wakati wa kula chakula usinywe maji kwa kubugia harakaharaka hata kama una kiu kali ya maji. Hii ni kwasababu unapokula chakula huku unabugia maji unapunguza nguvuya chakula,unajaza tumbo maji na kuchelewesha mmeng’enyo wa chakula (digestion). Chakula kisipomeng’enywa vizuri kitaketi tu tumboni. Matokeo yake hali hii ikiendelea kwa muda mrefu itakusababishia kitambi uonekane na tumbo kubwa ambalo si zuri. Kama hutofanya mazoezi ya kusawazisha mwili wako hasa tumbo, hali hii itasababishatumbo kwenda pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa watu wa makamo na kuleta maradhi kama kisukari, kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbonakadhalika.
3. Tafuna chakula vizuri.
Chakula huanza kumeng’enywa au kusagwa mdomoni. Mate ni chanzo cha uchambuaji chakula. Unapobugia chakula bila kutafuna sawa sawa unasababisha mambo mawili. Moja chakula kutochambuliwa vizurinapili chakula kwenda kukaa tumboni bila kutumika au kama kikipita hakitatumika ipasavyo mwilini.
Tafuna chakula taratibu na kwa uhakika ili kusaidia umeng’enyaji mzuri kwa matumizi ya mwili. Ukitafuna chakula vizuri pia utakuwa unajiepushia matatizo kama ya kuvimbiwa, kupata choo kigumu nakadhalika.
4. Punguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi.
Mafuta yanahitajika kwa kiasi mwilini, ni vyema ukala vyakula vyenye mafuta kwa mpangilio mzuri unaohitajika mwilini. Kula vyakula kwa kuuwianisha viwango sahihi vya vyakula hivyo(Eat a Well Balanced Diet which Contain Foods at Right Proportion).Chakula bora kilichokamilika hujumuisha wanga (mfano ugali, ndizi, wali, viazi, mikate, mahindi, nk), protini (mfano mboga na nyama), madini (mfano mbegu mbegu mbichi ambazo hazija kaangwa sana, chumvi nk) na “vitamini” (matunda, maziwa, mayai, nk).
Nyama ni muhimu sana kwasababu ina madini aina ya chuma (hasa kwa nyama nyekundu), protini, mafuta na pia inaongeza nguvu. Ila mafuta yaliyoko katika nyama si mazuri kwasababu huganda mwilini. Unashauriwa kula zaidi nyama ya samaki kwakuwa mafuta yake ni mazuri na yana Omega-3 fattyacids ambayo husaidia kuongeza kinga ya maradhi mwilini na pia ni chakula bora kwa afya ya ubongo wako.
PENDEKEZO:Kula korosho, karanga (ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi kidogo) kuliko nyama kwasababu mafuta yake ni yenye rotuba kuliko mafuta ya kwenye nyama vilevile hayawezi kukuongezea unene.
5. Fanya mazoezi ya mwili na viungo.
Mazoezi ninjia nzuri sana na ya pekee ya kupunguza unene, fanya mazoezi ya kukufanya moyo uendo mbio (cardio excercises) kama kukimbia, kuogelea, kuendesha baiskeli nk yatakusaidia kuchoma na kuyayusha mafuta mwilini.Ni vyema ukafanyamazoezi mpaka mwili utokwe na jasho kwani hiki ni kipimo kizuri cha kudhihirisha umefanya zoezi kwa kiwango stahiki na umeondoa sumu na taka nyingine mwilini. Kama wewe ni mwanachama na unahudhuria GYM kwenda kufanya mazoezi nakushauri uwe na mshirika wa kuwa unafanya naye mazoezi, mkiwa wawili au hata watatu sio mbaya kwa pamoja mtashindana kufanya mazoezi vizuri na ipasavyo. Vilevilemtapeana moyo kuendelea na mazoezi yenu kilaitokeapo mmoja wenu anajihisi kukata tamaa.
Mfanomzuri zaidi wa namna ya kufanyamazoeziukiwa nyumbanitumia dakika 10 kuangaliahiyo video clip hapo chini, inaonyesha namna ya kufanya mazoezi ipasavyo yatakayokusaidiakuchoma calories mwiliniilikupunguza unene na uzito wa mwili.
6. Jiwekee malengo thabiti ya kutaka kupunguza unene.
Kupunguza mwili na kuona mabadiliko sio jambo la muda mfupi, linahitaji uvumilivu na subira hasa pale unapokaribia kukata tamaa. Zingatia ulaji bora wa mlo wako wa kila siku na fanya mazoezi ipasavyo bila kuchoka au kuzembea. Ni vyema ukawa na notebook ya kuandika chini maendeleo yako. Mfano unaweza kujiwekea malengo ya kupunguza kilo 1 kila baada ya wiki,ni vyema ukashikiliamsimamo wako mpaka ufanikiweufikie mahali ujionena kujiridhisha kwa kujipima ukubwa wako wa sasa na kulinganisha na vipimo vyako vya zamani.
Kwa hayo machache naamini ukiyafanyia kazi yatakusaidia kupunguza unenewa mwili wako na kuwa mwenye umbo zuri la kuvutia. Kila la heri na nakutakia afya njema!...
No comments:
Post a Comment