Tuesday, October 15, 2013

FAHAMU UGONJWA WA KISUKARI (DIABETES)

Fahamu ugonjwa wa kisukari (diabetes).

Diabetis(Ugonjwa wa kisukari).

Diabetis ni nini?Diabetis ni ugonjwa unaosababisha mwili kutokuwa na matumizi ya kutosha ya insulin. Insulin ni homoni yenye uwezo wa kubadilisha umbo la sukari, wanga, na vyakula vingine kuwa nguvu au kani ya uhai wa kila siku.
Matibabu ya ugonjwa wa kisukari (diabetis) yakoje?
Matibabu ya diabetis yapo katika sehemu tatu:
1. Kula vizuri kwa afya (good diet).
2. Kufanya mazoezi ya mwili.
3. Kwa kutumia dawa (kama utalazimika).
Utawezaje kumudu ugonjwa wa kisukari (diabetis)?Utaweza kumudu ugonjwa wa kisukari au kiwango cha sukari kwenye damu (blood glucose) kwa kula chakula chenye afya (good diet), kufanya mazoezi ya mwili, na kwa kuwa na uzito wa mwili wenye afya (healthy weight).
Uzito wenye afya (healthy weight) utakusaidia pia kumudu kiwango cha mafuta (fats) kwenye damu (cholesterol) na kupunguza msongo wa damu (blood pressure).
Watu wengi wenye diabetis wanahitaji pia kutumia dawa kusaidia kutawala sukari (blood glucose).
Kula vizuri kwa afya.
Kwa kutumia mwongozo wa ulaji (food guide pyramid) kutakusaidia kula vyakula mbalimbali
kwa afya. Kula vyakula mbalimbali au chakula chenye mseto wa aina tofauti tofauti ya virutubisho (balanced diet). Unapokula balanced diet kila siku, utapata vitamin na madini mengi yanayohitajika kwa ubora wa afya yako.
Huu ni mfano wa kula chakula chenye virutubisho mbalimbali (balanced diet).
Siku ya kwanza Siku ya Pili
Mbegu (grains): chapati mchele wa rangi (brown rice)
Tunda: tofaa (apple) embe
Mboga: brokoli nyanya
Maziwa: maziwa (fresh) mtindi
Protini: kuku maharagwe
Kula vyakula vyenye virutubisho vyote.
-Nunua mikate ya chembe (grain breads) na mikate ya nafaka (cereal breads) na ngano,
-Punguza kula vyakula vya kukaanga na vyenye mafuta kama maandazi na biskuti.
-Matunda ni bora zaidi, ukinunua matunda ya kwenye kopo, tazama maneno “canned in their own juice”. (“yametayarishwa na juisi yake”)
-Nunua matunda madogo madogo, na unywe juisi kiasi kidogo kidogo.
-Kula mboga ambazo hazijapikwa kwa maafuta mengi.
-Tumia haradali (mustard) badala ya siagi nyingi kwenye mkate.
-Tumia mafuta ya mboga badala ya mafuta ya kawaida, siagi au samli.
-Namna bora ya kupika ni kuvumbika, kuchemsha, kutokosa, kuchoma, kwa
mvuke na kuoka. Usitumie mafuta mengi wakati wa kupika.
-Tumia nyama isiyo na mafuta kama kuku, bata mzinga. Unaponunua nyama ya nguruwe,
nyama ya ng’ombe na kiweo, kata unono ( extra fat ) wake.
-Tumia maziwa yasiyo na mafuta (fats), na vyakula vinavyotokana na maziwa bilafats.
Punje (grains), maharagwe na mboga yenye kanji (starch).
Kanji (starch) au kabohaidreti/wanga ni nini?
Kanji (starches) ni vyakula kama mikate, punje (grains), nafaka, pasta, maharagwe au mboga yenye kanji (starch). Kula kanji ama kabohaidreti chache kila unapokula. Watu wanaweza kukuambia usile kanji (starch) ama kabohaireti nyingi lakini huo si ukweli. Kula kanji (starch) ama kabohaidreti kuna faida za kiafya ikiwa ni pamoja na kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari (diabetis).
Unahitaji kanji (starches) ama kabohaireti/wanga ngapi kila siku?Resheni (servings) 6 hadi 11 kila siku.
Idadi ya resheni unayotakiwa kula kwa siku inategemea na kalori (calories), unazohitaji mpango wa tiba na hali yako ya kisukari (diabetis).
Kanji (starches) na kabohaidreti/wanga hufanya nini katika mwili wako?Kanji (starch) huupa mwili wako nguvu, vitamin B, madini na vitembwe (fibre). Punje (grains) ni zenye afya zaidi kwa vile zina vitamin, madini, na vitembwe (fibre). Vitembwe (fibre) hukusaidia kupata choo. Pia hukusuaidia katika uwezo wa kumudu au kuongeza idadi ya sukari kwenye damu (blood glucose).
Mlo mmoja wa starch ama wanga upo hivi,
-Kipande kimoja cha mkate
-Kiazi kidogo, mhogo au ndizi moja
-Nusu (1/2) kikombe cha nafaka ya kupika kama uji au ngano.
-Sehemu ya ¾ ya kikombe cha nafaka ngumu kama corn flakes.
-Sehemuya kikombe cha wali.
Unaweza kula mlo wa namna hii.Mfano,
Chakula cha asubuhi:Sehemu ¾ ya kikombe cha nafaka ngumu na kipande kimoja cha mkate.
Chakula cha mchana:Sehemu 1/3 ya kikombe cha mchele na ndizi za
kupika.

No comments:

Post a Comment