Chakula
Chakula cha jioni (Chajio):Nusu kikombe cha pasta na kipande kimoja cha mkate.
Kitafunio:Biskuti sita.
Mboga.
Mboga ni bora kwa afya hasa kwa watu walio na ugonjwa wa kisukari (diabetis). Kula mboga kila siku, mboga zitakupatia vitamin na madini. Chagua mboga zenye rangi.Mfanokaroti, pilipili, biringanya, nyanya na mchicha.
Matunda.
Tunda ni asili ya afya kwa kila mtu, wakiwamo watu walio na shida ya kisukari (diabetis). Tunda hukupatia nguvu, vitamin na madini. Penda kula matunda kwa namna hii,
-Kula tofaa (apple) ama pera moja.
-Nusu kikombe cha juisi ya tofaa (apple) ama chungwa.
-Nusu kikombe cha juisi ya zabibu.
-Ndizi moja ndogo au nusu ya ndizi kubwa.
Kama utatengeneza juisi ya matunda usiongeze sukari.
Maziwa na vyakula vya mtindi.
Maziwa yenye idadi ndogo ya fats ni mazuri kwa afya kwa watu wote, wakiwamo watu wenye kisukari. Maziwa (fresh) na mtindi yatakupatia nguvu, protini, calcium, vitamin A, na vitamin nyingine na madini mbalimbali.
Kunywa maziwa yasiyo na fats au kiasi kidogo cha fats (1%) kila siku. Kunywa mtindi usio na
fats au wenye kiasi kidogo cha fats ili kuepuka kuongeza kiwango cha cholesterol kwenye damu.Usitumie mtindi wa kwenye makopo unaosema, “fruit on the bottom” kwasababu kwa jinsi ulivyotengenezwa una sukari nyingi.
Nyama, kuku, samaki na mayai.
Kundi hili la chakula ni la nyama ya (ng’ombe, nguruwe, kondoo), kuku, bata mzinga, mayai, samaki nakadhalika. Vyakula vyote hivi ni vyenye protini kwa wingi na husaidia kujenga misuli na mifupa pia vinaupa mwili vitamin na madini.
Katika mlo wako unaweza kuweka hivi,
-Samaki wawili au watatu.
-Nyama ya kuku.
-Yai moja.
-Vijiko viwili vya siagi ya njugu au karanga.
Mapendekezo ya Kusaidia:
-Kama utanunua nyama ya ng’ombe au mbuzi yenye mafuta basi ondoa sehemu ya mafuta.
-Kula kuku au bata mzinga bila ngozi.
-Pika vyakula vyenye protini kwa mafuta kidogo wa wakati wa kukaanga, kuoka,
kutokosa, kuchoma, kupika kwa mvuke ama kuchemsha.
Tamutamu (sweet foods).
Tamutamu ni vyakula vya sukari vyenye kalori bila vitamin au madini. Vyakula vingine vinasukari nyingi kama keki, pai, na biskuti.Kwa kula vyakula vingi vyenye sukari na mafuta mengi kutakuletea shida katika harakati za kutibu ugonjwa wa kisukari.
Kama utapendelea kula vyakula vya namna hii basi zingatia kutoweka sukari nyingi ili kuepusha matatizo. Mfano unaweza weka,...
-Kijiko kimoja cha mafuta.
-Kijiko kimoja cha mafuta ya saladi.
-Vijiko viwili vya mayonnaise.
Au kama unataka kupata breakfast ule biskuti moja, andazi moja.
Nakutakia afya njema katika maisha yako.
Kama una chochote cha kuongeza kuhusiana na mada hapo juu, tafadhali usisite kutoa maoni yako!
No comments:
Post a Comment