Njia za kupunguza unene wa mwili wako.
Wastani wa maisha ya mtanzania (na waafrika wengi) ni miaka 40-50. Kati ya sababu kuu zinazopunguza uhai ni kuwa na afya mbovu,makala ya leo inahusu tatizo la unene wa mwili.Tatizo hili la unene na uzito uliozidi sababu yake kuu nikutokujua namna ya kutunza mwili wako kwa kula vizuri na kufanya mazoezi. Unene usio wa kawaida ni tatizo kubwa kwa watu wengi hivyo kama wewe ni mmoja wapo na unataka kupunguza mwili wako, hizi hapa ni njia za kukusaidia kupunguza unene na kuwa mtu mwenye muonekana mzuri na afya njema.
1. Kula vizuri.
Ipo mifumo miwili ya kula vizuri. Kwanza ni chakula unachokula na pili ni namna unavyokilachakula hicho.
*.Ulaji bora wa chakula.
Kuna ulaji wa kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache. Tumbo lina misuli inayofanya kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata taabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unaparilia zaidi mafuta mwili na kusababisha kukaa kwa mafutatumboni bila kutumika ambapo baadae itapelekea mtu kupata kitambi.PENDEKEZO:Asubuhi kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo unywe chai na vitu vingine kama mkate au maandazi.
Namna ya kula matunda na mboga za majani kwa mpangilio mzuri.
Watu wengi hukosea kula matunda na mboga za majani kwa usahihi. Nasema hivyo kwa maana ya kwambawengi hula matunda baada ya chakula, hii si namna nzuri ya kula kwasababu vimeng’enya chakula (enzymes) zilizopo tumboni hufanya kazi kwa namna tofauti. Enzymeshizi namna zinavyonyambua na kumeng'enya matunda ni tofauti na namna zinavyomeng’enya vitu vigumu kama nyama au vyakula vingine jamii ya wanga hivyo matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine. Ni bora kula matunda dakika 10-20 kabla ya kula chakula kwasababu unapokula matunda baada ya kupata chakula hugeuzwa na kuwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya mfumo wa damu kupitia utumbo mdogo, wengu, moyo, ininakadhalika.
Mseto wa vyakula ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu (“acid”) na vile vinavyomung'unyuka haraka (“alkaline”) havitakiwi viliwe kwa pamoja. Mfano mzuri ni matunda. Matunda yenye uchachu kama machungwa, mananasi na maembe yanatakiwa yaliwe pamoja na yale laini zaidi kama ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk nayo yaliwe kivyake kwasababu mfumo wake wa kumeng'enywa ni tofauti.
Vilevile nyama nyeupe (nyama za ndege na samaki) unashauriwa ziliwe tofauti na nyama nyekundu (nyama za ng’ombe, mbuzi, kondoo nk) ziliwe tofauti.
*.Chakula bora kwa afya njema.Kula vyakula bora vyenye thamani kwa mwili wako, epuka vyakula vyenye sukari nyingi, mafuta mengi au chumvi nyingi badala yake zidisha kula mboga mboga zilipikwa kiasi bila kuiva sana mpaka kupoteza nguvu. Ni vizuri pia kula mboga mbichi kama salad (unaweza kuiita kachumbari vyovyote ujuavyo) si lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu.
Waweza kuchanganya matango, nyanya na maparachichi au vitunguu saumu, giligilani na karoti. Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukila na chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika nk). Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku sio mzuri kwasababu huchangia kunenepa.
PENDEKEZO:Unaweza kula ugali kwa samaki, mboga za majani, matango na nyanya bila kuweka chumvi nyingi.
Inaendelea..
No comments:
Post a Comment