Makosa ya kuyaepuka katika maongezi.
Kuongea na watu ni kitu ambacho tunafanya kila siku, tunaongea na ndugu, jamaa au rafiki iwe ni kubadilishana mawazo, kuelekezana na kuelewana au kuhabarishana mambo ya hapa na pale.
Mahusiano baina yako na watu wengine yanategemea sana maongezi yako ya kila siku nawatu unaohusiana naokwa maana ya namna unavyoongea nao, unavyowasikiliza kwa makini na kuchangia mawazo yako pale ushauri unapohitajika na mambo mengine yanayokusababisha uongee. Bila maongezi maisha yanakuwa badohayajakamilika kwakuwatunaishi kwa kutegemeanakimahusiano na mahusiano yetu na watu mbalimbalihuletwakwa kufanyamaongezi.Ni rahisi kwako kupata marafiki na kujuana na watu wengi ikiwa utakuwa mchangamfu na mcheshi katika kuongea.
Maongezi mazuri ni lazima yawe ni yenye maelewanona yenye mantiki ya kile mnachozungumza. Kujua makosa ya kutokufanya wakati unaongeani ujanja na busara pia kwasababukuongea vizuri na watu kunakuongezeasifa nzuri na kukuza mahusiano yako. Soma hapo chini mambo ya kuyaepuka unapokuwaunaongea na mtu.
1.Usiongee maneno mengi kwa haraka.
Unapoongea na mtu, ongea taratibu kwa sauti ya kusikika vizuri.Watu wengi hupenda mtu mtaratibu katika uongeaji.Kama utaongea kwa haraka itakuwa ni vigumu kwa anayekusikiliza kukuelewa vizuri nini unachomaanisha. Vilevile hatoweza kupata kikamilifumaneno yako yote unayomwambia. Hivyo ukitaka ueleweke vizuri kwa watu,jieleze kwa kuongea taratibu. Ukifanya hivyoutamfanya pia huyo unayeongea naye akuone ni mtu unayejiaminina unauhakika wa kile unachomweleza.
2. Usiulize maswali mengi ndani ya muda mfupi.
Ulishawahi kukutana na mtu muongeaji kupita kiasi?Anakuuliza maswali zaidi ya mawili kwa wakati mmoja. Hii sio namna nzuri ya kuwasilisha mambo yako katika maongezi.Kama una swali uliza kwa mpangilio maalum kwa kuuliza swali moja na ujibiwe kisha ulizajingine. Ikiwa utakuwa upo mahali ambapo mnaouliza maswali ni wengibasi nivyema ukapangilia maswali yako kinambari yani swali la namba1,2, 3....ili unapoyawasilisha maswali yakomsikilizaji aweze kukuelewa na kujipanga vizuri namna ya kukujibu maswali yakoipasavyo.
3. Usianzishe mada ambayo haieleweki au haivutii kwa msikilizaji.
Unapotaka kuongea kuhusu kitu fulani ni vyema kiwe chenye kupendeza masikioni mwa mtu au watu wanaokusikiliza.Ukianzisha mada ambayoinaaminika kuwa ni uongo au ni ngumu kufikirika kirahisina kueleweka vizuriitamchosha msikilizaji.Epuka kuongea matusi au umbea uliopitiliza kwani hakuna mtu anayependa kusikia mambo hayo sana vilevile utaonekana wewe ni mtu wa ajabuusiyejieshimu. Lakinipia unawezakuwa mcheshi kwa kuwafurahisha watu kwa vichekesho au kuwatania kwa kiasi fulani bila kuonekana wewe ni kitukoikiwa utafanya hivyo katika mazingira maalum na wakati muafaka wa kufanya hivyo.
4. Usifanye mambo mengine yatakayosababisha msisikilizane.
Inakera sana kwa mtu mwingine unayeongea naye kukuona ukifanya mambo mengine badala ya kumsikiliza. Mambo ya kuwa unaongea na mtu huku unamtumia mtu mwingine ujumbe kwenye simu au kuzungumza na mtu mwingine wa pembeni wakati unaongea na simu sio mazuri kabisana yanakera hata kama ukijaribukujitetea hutaeleweka. Pia wakati unaongea na mtu usiwaze mambo menginetofauti na maongezi yenu. Kosa ambalo watu wengi hufanya ni kupeleka akili zao mahali pengine badala ya kusikilizawanachoelezwa.(Always Let Your Mind Be Where You Are)
5. Usijaribu kujionyesha unajua kila kitu.
Ukijifanya wewe ni mjuaji, unayeongea naye atakuona wewe unajifanya kuwa ni‘’MUCH KNOW’’sana hivyo atasita kukueleza mambo mengine ambayo ni muhimu kwako kuyajua. Pia ukijiona unajua mengiutakuwa unajifunga wewe mwenyewe usijue mambo mengine ambayo huyajui kutoka kwa wengine. Kila unapopata nafasi ya kuongea na mtu msikilizekwamakinikwakuwa kila mtuana jambo au wazo ambalo wewe hulijui. Hata kama kile mtu anachokwambia unakifahamu msikilizepiakwasababuhuenda katika maelezo yake atakuongezea wazo ambalo ulikuwa hulifahamu hapo kabla.Kuwa mdadisi kwa kujifanya hujui kitu unapoongea na watu hakika utajifunza mengi sana kutoka kwao. Kumbuka maneno haya yatakusaidiakutoridhika kutakakujua mambo kwakuwa hakuna ajuaye yote''Stay hungry, stay stupid."
No comments:
Post a Comment