Friday, October 18, 2013

Mambo ambayo watu wengi hawapendi kusikia wakizungumziwa kuhusu wao.

Mambo ambayo watu wengi hawapendi kusikia wakizungumziwa kuhusu wao.
(Things that most people don’t like to hear about themselves.)
Katika maongezi huwa tunaongea mambo mengi sana yahusiyo Maisha, Michezo, Mahusiano, Siasa, Kazi nakadhalika. Ili uwe muongeaji mzuri usiyechukiza watu unao ongea nao ni hekima kuchunga kauli yako na kujua unaongea nini kwa mtu/watu wanaokusikiliza.
Watu unao ongea nao watavutiwa na kuendelea kukusikliza iwapo watapenda unachokiongea. Kwa upande mwingine kuongea na watu kunaweza kukujengea uhusiano mzuri au kubomoa uhusiano wenu. Kujua ni mambo gani watu hawapendi kusikia kutakusaidia kujua nini cha kusema na kipi cha kuacha kusema wakati wa maongezi yenu.
Yafuatayo ni mambo ambayo wanaume na wanawake hawapendi kusikia kuhusu wao.
Wanaume hawapendi kusikia mambo haya kuhusu wao.
1. Kumwambia kuwa hawezi kutunza pesa zake vizuri au ni mfujaji mali.
2.Kumwambia yeye hana akili au ni mjinga.
3. Kuimwambia yeye ni mfupi (andunje)
4. Kumwambia yeye si mcheshi au amezuuba sana.
5. Kumwamba anaonekana kama amezeeka.
6. Kumwambia kuwa yeye ni mwoga au dhaifu au ni mshamba wa mambo.
7. Kumwambia kuwa yeye hajui kujali au kubembeleza mwanawake.
8. Kumwambia kuwa yeye hana hela au ni maskini tu.
9. Kumwambia kuwa yeye ni bahili sana.
10. Kumwambia kuwa yeye hajui kuongea na watu vizuri. (domo zege)
11. Kumlinganisha yeye na wanaume wenzake waliomzidi kimaendeleo au kwa chochote kile.
-Kama wewe ni mwanamke na unataka kuimarisha au kukuza ujuzi wako wa kuongea na wanaume kuwa makini sana unapotumia maneno hayo kuzungumza na wanaume kwani wengi wao hawapendi kabisa kusikia wakiambiwa hivyo.
Wanawake hawapendi kusikia mambo haya kuhusu wao.
1.Kumwambia kuwa yeye hana umbo la kuvutia au ana kasoro na umbule lake.
2. Kumwambia yeye ni mnene sana au ameongezeka uzito.
3. Kumwambia kuwa yeye amezeeka.
4. Kumtajia umri wake kuwa yeye ni mkubwa sana.
5. Kumuuliza kama alishawi kuolewa hapo nyuma.
6. Kumfananisha yeye na mwanawake mwingine ambaye hapendezwi naye.
7. Kumwambia kuwa hajapendeza na nguo alizovaa.
8. Kumwambia kuwa yeye ana sauti mbaya siyo nyoror o ya kuvutia.
9. Kumuuliza yeye ana watoto wangapi ikiwa maongezi yenu hayahusu mambo ya kifamilia.
10. Kumlinganisha yeye na mwanamke mwingine amemzidi kwa kitu chochote. Mfano: Uzuri, Pesa, Mali.
Natumaini kuwa utakuwa umejua mambo ambayo watu hawapendi kusikia , huchukia kila wanapoaambiwa mambo hayo kuhusu wao. Kila mtu hupenda kusifiwa kwa namna yake ya kipekee, hivyo chunga usimfadhaishe mtu kwa kumzungumzia vibaya .
Mpe mtu sifa nzuri na stahiki kuhusu yeye na kwa pamoja mfurahie maisha kwakuwa kila mtu ana uzuri wake na kasoro zake!

No comments:

Post a Comment