Namna ya kuondoa uchovu unapojihisi umechoka.
Kuna sababu nyingi za mtu kuchoka, unaweza kuchoka baada ya kufikiri au kutafakari sana kwa muda mrefu bila kutuliza akili (msongo wa mawazo). Vilevile uchovu unaweza kuwa ni wa mwili uliosababishwa na kufanya kazi nyingi au kazi nzito bila kupumzika. Uchovu ni dalili ya kuonyesha na kudhihirisha kuwa mwili wako unahitaji mapumziko ili uweze kurudia katika hali yako ya kawaida ya kuwa na nguvu.
Kupumzisha mwili na akili yako ni afya hivyo ni muhimu ujue namna za kujipumzisha kila unapokuwa umechoka na kurejesha mwili wako katika hali ya kawaida. Hizi hapa ni njia mbalimbali za kukusaidia kuondoa uchovu unapokuwa umechoka.
1. Kunywa kinywaji laini au kula chakula chepesi chenye kukupa nguvu.
-Maji au juisi fresh ya matunda ni nzuri sana, unapokunywa kinywaji laini mwili wako unapata nafasi ya kurudisha na kufiidia maji yaliyopotea mwilini na kurejea katika hali nzuri. Unaweza pia kula keki, crips, biskuti au kitafunio chochote kizuri cha kukuongezea nguvu lakini kumbuka usile vyakula ovyo (chips mayai, mishikaki, mihongo ya kukaanga nk) hasa vyakula vya magengeni kwakuwa sio vya kuaminika(kiusalama na kiusafi) na pia sio vizuri kwa kujenga afya yako.
2. Jipumzishe kwa kulala mahali safi na tulivu.
-Wakati mzuri wa kulala ni usiku kwasababu hakuna kelele za hapa na pale na pia kuna utulivu wa hali ya juu ukilinganisha na wakati wa mchana. Kiafya unatakiwa kulala kwa muda wa saa 6-8 na si vinginevyo. Ukilala sanakupitiliza ulalaji wa kawaida utauongezea mwili wako uchovu kwa kuwa na‘’depression’’. Kwa wakati wa mchana, unaweza ukajipumzisha kwa kusinzia kwa dakika chache 10-15 kwenye kochi kisha utakapojisikia vizuri endelea na kazi zako nyingine. Kumbuka lengo la kulala ni kuupumzisha mwili na ubongo ili upate nguvu na kuongeza ufanisi wake wa kiutendaji kazi. Zingatie usingizi bora (Quality Sleep) kwa afya bora.
Kujua zaidi: Soma Tips on how to improve your sleep.
3. Sikiliza muziki utakaokufanya ujiliwaze au pata burudani nyingine ya aina yeyote ya kukuchangamsha.
-Ala nzuri za muziki zinaweza kukuondolea msongo wa mawazo na kujihisi vizuri mwenye furaha. Kusikiliza wimbo na kucheza peke yako ni njia moja wapo ya kujichangamsha hasa pale unapofuatilia maneno yanayoimbwa katika wimbo huo. Raha ya muziki ni pale unapoimba na kwenda sambamba na ujumbe wa kile kinachoimbwa. Fanya hivyo na baada yaburudaniutajikuta hali yako imebadilika nakuwa nzuri kabisa.
4. Jinyooshe kwa kufanya zoezi dogo.(Pushups, Kusimama na Kukaa kwa Haraka haraka nakadhalika)
-Uchovu unaweza kusababisha jointi na viungo vingine kama kiuno kukaza. Dawa ya tatizo hili ni kufanya zoezi la kujinyoosha. Unajua kwanini nimesema ufanye zoezi la kupiga pushups? Pushup ni zoezi la kawaida tu lakini ukilifanya ipasavyo litaweka mwili wako sawa. Unashauriwa kila siku uamkapo asubuhi ukiweza piga pushups 60-100. Hii ni kwasababu pushup ni zoezi ambalo hupasha mwili kwa haraka, huboresha misuli, upumuaji wa mapafu na kufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri.
Unaweza soma pia: Je unajua manufaa ya kufanya mazoezi.
5. Tafuta mahali penye hewa safi upunge upepo.
-Njia ya haraka ya kukufanya ujisikie vizuri ni kukaa au kutulia mahali penye upepo mwanana kwa dakika kadhaa. Labda unapenda kukaa mahali penye kivuli kizuri cha miti au ghorofani penye uwazi mkubwa wa kusimama na kuangalia mandhari mazuri ya mahali ulipo. Vyovyote vile lengo ni kupunga upepo na kutuliza akili bila kuwaza mbali au kufikiri mawazo ambayo yataendelea kukufanya ujisikie vibaya.
6. Cheza michezo ya kukuburudisha.(Computer and Mobile games)
-Kwenye simu za mkononi au computer kuna michezo kwaajili ya kujiburudisha. Kwanini usitumie angalau dakika 8 kucheza game ‘’angry bird’’ kwenye iPhone, iPad au ‘’karata’’ kwenye computer ili kuburudisha akili kisha uendelee na mambo yako mengine. Tusijichoshe sana kwa kuchat kwenye chatting messengers kama whatsapp, google talk nakadhalika bali tujenge tabia ya kupenda kitu kwa kiasi na si sana mpaka kupitiliza.
Thank uu
ReplyDeleteUjumbe mzuri Sana
ReplyDeleteAsante sana
ReplyDeleteAsante Sana
ReplyDeletepoa
ReplyDelete