Tuesday, October 15, 2013

MAGONJWA NYEMELEZI NA DALILI ZAKE.

Magonjwa nyemelezi na dalili zake.


Magonjwa nyemelezi ni yale ambayo hushambulia mwili wa binadamu pale uwezo wa kinga ya mwili kupigana na vimelea vya magonjwa inaposhuka. Ni magonjwa ambayo katika hali ya kawaida hayategemewi kujitokeza kwa mtu mwenye kinga kamili ya mwili.
Kwa kawaida mwili wa binadamu yoyote umeumbwa na kinga ya mwili ya asili ambayo lengo lake kuu ni kuulinda mwili dhidi ya vimelea vya magonjwa. Inapotokea kimelea (vimelea) kuingia katika mwili wa binadamu kwa njia yoyote (kunywa au kula vimelea, kugusana na majimaji au ngozi ya mtu mwenye vimelea au kupitia damu yenye vimelea n.k), mwili hutengeneza kingamwili (antibodies) ambazo hupigana na vimelea hivyo ili kuuweka mwili katika afya njema kama hapo awali.
Kushuka kwa kinga ya mwili hupelekea mwili kushindwa kupigana na vimelea vya magonjwa hivyo kusababisha kushambuliwa na magonjwa.Ifahamike kwamba baadhi ya vijidudu (microorganisms) pia hupatikana katika mwili wa binadamu bila madhara yoyote (normal flora) kama vile kwenye ngozi, mfumo wa chakula, ukeni, uumeni n.k. Mathalan vijidudu hivi huweza kuwa chanzo cha magonjwa iwapo kinga ya mwili itashuka.
`
Vitu gani hupelekea kushuka kwa kinga ya mwili?
Sababu mojawapo kubwa ya kushuka kwa kinga ya mwili haswa katika nchi zilizopo chini ya jangwa la Sahara ni Ukimwi/VVU. Pia ieleweke kwamba si kila mtu mwenye upungufu wa kinga mwilini ana VVU.
Kuna sababu nyingine nyingi ambazo husababisha kwa njia moja au nyingine kushuka kwa kinga ya mwili.Zifuatazo ni baadhi tu ya sababu hizo;...
Utapiamlo, kuugua mara kwa mara, sababu za kijenetiki (kurithi), madhara kwenye ngozi, msongo wa mawazo, ujauzito, madawa ya kutibu saratani, matumizi ya muda mrefu ya antibayotiki (antibiotics),steroidi (steroids) na madawa ya kushusha kinga mwilini (immunosuppressant drugs) ambayo hutumika wakati wa kupandikiza viungo mwilini kama figo n.k
Magonjwa nyemelezi husababishwa na vijidudu mbalimbali kamabacteria, virusi, fangasi na bakteria.
Magonjwa yatokanayo na Bakteria.
Baadhi ya magonjwa yasababishwayo na bakteria ni kama yafuatayo;
Kifua Kikuu (TB)
Ugonjwa huu husababishwa na kimelea kiitwachomycobacterium tuberculosisambacho ni moja katika kundi la Mycobacterium Avium Complex (MAC). Kushuka kwa kinga ya mwili hupelekea kulipuka kwa vimelea vya kifua kikuu ambavyo hupatikana, pamoja na viungo vingine, zaidi kwenye mapafu.
Dalili za kifua kikuu ni pamoja na kikohozi, homa (haswa nyakati za usiku) kwa zaidi ya wiki mbili, kutokwa jasho usiku (mara nyingi jasho huwa jingi mpaka kulowesha shuka), kupungua uzito (zaidi ya kilo moja na nusu ndani ya mwezi), kichomi na kukohoa damu.
Ugonjwa huu pia huweza kupelekea kupata homa ya uti wa mgongo (meningitis) ambayo huambata na dalili kama kuumwa kichwa, kichefu chefu na kutapika ikifutiwa na kuongezeka kwa joto la mwili na maumivu na kukaza kwa shingo.
Nimonia (Pneumonia).
Huu ni ugonjwa ambao kwa kiasi kikubwa huathiri mfumo wa hewa na haswa mapafu. Baadhi ya vimelea viletavyo nimonia ni kamapneumococcus ,haemopilus influenza, mycoplasma(haswa kwa watoto)piaklebsiella, staphylococcus aureus, pseudomonas aeuroginosa(kwa wagonjwa waliolazwa mahospitalini) na wengineo.
Ugonjwa huu huanza ghafla na dalili zake ni kama homa kali, kikohozi, maumivu wakati wa kupumua, baridi na kutetemeka.
Ugonjwa wa Ngozi.
Huu husababishwa na vimelea vyaStaphylococcus aureus.Vimelea hivi huishi katika mwili wa binadamu (kwenye ngozi ya kichwa na kinena (groins) na kwapani) bila madhara. Pia hupatikana kooni na katika utumbo mpana na mkojo.
Vimelea vya Staphylococcus husambaa kwenda sehemu nyingine ya mwili kutoka kwenye usaha, mgusano na ngozi ya mwenye maradhi, kutumia taulo, matandiko,vifaa vya mtu aliyeathirika n.k
Dalili zake ni pamoja na chunusi, majipu, kubabuka kwa ngozi na magamba magamba katika ngozi.
Magonjwa ya virusi.
Magonjwa yasababishwayo na virusi ni kama;
Ugonjwa wa Malengelenge.
Husababishwa na virusi vyaHerpes Simplex. Hivi vimegawanyika katika Herpes Simplex Virus-1 (HSV-1) na Herpes Simplex-2 (HSV-2).Virusi vya HSV-1 vyaweza ambukizwa kupitia ngozi laini (mucous membranes) za mwili na kubusiana. Huweza kusababisha mwasho kwenye mdomo, ulimi, fizi za meno au kingo za juu za kinywa (buccal mucosa). Kwa upande wa virusi vya HSV-2 hivi huweza kusababisha michubuko na maumivu kwenye uume, uke na njia ya haja kubwa.
Katika kiwango cha juu cha ugonjwa viungo vingine vya mwili kama macho, njia ya chakula, mfumo wa fahamu na na njia za mfumo wa hewa huathirika.
Dalili balimbali za ugonjwa huu ni malengelenge (blisters), mwasho na muunguzo. Kushindwa kumeza au kupata maumivu wakati wa kumeza (haswa chakula), tezi kuvimba na maumivu wakati wa haja kubwa au ndogo.

No comments:

Post a Comment