Sunday, October 27, 2013

MEMORY IMPROVEMENT.

Memory Game

Memory improvementis part of this memory game, the process can be done with few steps that can be easyand performed effortlessly. Many people have trouble remembering faces ornames. How to remember things is only a technique that you need to utilize, forexample toremember a faceyou just need toexamine a person’s facediscretely when you are introduced. Try to find anunusual feature,ears, hairline, forehead, eyebrows, eyes, nose, mouth, chin, complexion, etc.
Createan association between that characteristic, the face, and the name in your mind. The association maybe to link the person with someone else you know with the same name.Alternatively it may be toassociate a rhyme or image of the name with theperson’s face or defining feature, try to apply that to one of the memory games below..
Alsowhen you are introduced, ask for the person to repeat their name. Use the nameyourself as often as possible (without overdoing it!). If it is unusual, askhow it is spelled or where it comes from, and if appropriate, exchange cards.Keep in mind that the more often you hear and see the name, the more likely itis to sink in.
Also,after you leave the person, review the name in your mind several times. If youare particularly keen you might decide to write it down and make notes, that would help and improve your memory search processThemethods suggested for remembering faces and names are fairly simple andobvious, but are useful.Association either with images of a name or withother people can really help. Repetition and review help to confirm your memory.
Thismemory game is going to activate some areas of your brain responsible for memory acquisition which therefore can help yourmemory improve.

SELF POWER AND MAGIC OF SELF APPOINTMENT.

Personal Power and the Magic of Self-Appointment


From a young age, you are appointed. Appointedto what and by whom? By your parents as “old enough to stay home alone.” By your institutions as “educated enough to enter the full time work force.” By your employers as “responsible enough for a promotion.”
Ask yourself these 2 important questions:
1)Have you become mentally conditioned by all the external appointments?
2)Have you given your personal power to something outside of yourself?
Could this be the invisibleforcethat is blocking you from rocketing toward your goals and reaching your full potential? For most of us, to one degree or another, the answer is “yes.”
From a young age, powerful forces within society condition you to undervalue who and what you are. Why? Because they want you to look to them for your sense of self-worth. They want you to look to them for validation, approval, and permission, through the appointments that they bestow on you.
You are much more than they want you to believe
Yes, we’ve all been hypnotized into believingwe are smaller and less than we really are. Just as a fishbowl keeps goldfish tiny, to one extent or another we’ve all been conned into believing our value is determined by the size of our external appointments.
The question is not: Have you given your personal power to someone or something outside of yourself? The real question is: How can you take it back? You see, personal power is an inside job. You do not need to import it from an external source. All you need to do is challenge the lies you’ve been told and persuaded to believe.
Break free of the conditioning
Realize that our school system, government, and industries reward dependency, NOT self-reliance. They reward conformity, NOT innovation. And they reward slavery to the status quo, NOT fearless adventure into the unknown.
Aside from the basics, much of what you learned through formalized education is irrelevant, outdated knowledge. Its main role is to control your focus and beliefs. Worse yet, it is designed to condition you to take your assigned place in the socially accepted order of things.
This results in the inevitable stunting of your initiative, creativity, and capacity for thinking outside the box. Under these circumstances, how could you possibly develop the skills to appoint yourself master of your own life and financial destiny. Instead, you end up waiting for permission to move slowly up the lower and middle rungs of the ladder of mediocre success.
Don’t accept mediocrity
Please don’t limit your life or your income while you wait for someone else to give you permission to be more. Expand your beliefs to encompass the life you were born for. Emerson said, “Do the thing, and you will have the power.” You don’t need anyone’s permission, appoint yourself.
Would you like to reclaim your personal power and learn to appoint yourself
as master of your own life?

DALILI KUMI 10 ZA MTU ASIYEJIAMINI.

Dalili kumi (10) za mtu asiyejiamini.


Kutojiamini ni tatizo la watu wengi, kwa kulijua hilo nimeona ni vyema tukajuzana mambo machache kuhusu "KUJIAMINI" dalili hizi kumi (10) nilizooredhesha hapo chini nimezipata katika mtandao mmoja wa kijamii wa hapa nchini kwetu, kwakuwa niliona ni jambo linalogusa watu wengi nikaona niweke hapa ili wote tufaidike. Soma kwa makini naamini kwa namna moja au nyingine utajifunza kitu. Dalili zenyewe ni kama zifuatazo...

DALILI KUMI ZA MTU ASIYEJIAMINI.

1.Kugusika kirahisi.
-Mtu asiyejiamini huwa anagusika kirahisi sana, jambo dogo linaweza kumnyima furaha kwa kiwango kikubwa. Jambo dogo linaweza kumuudhi kupindukia. Kuna watu ambao kwa utani mdogo sana wa kawaida wanakasirika sana, wanajihisi vibaya na kuumia sana.
2.Kuwategemea wengine kuthibitisha.
-Mtu asiyejiamini huwa haamini uwezo wake, maamuzi yake au hisia zake, hadi athibitishiwe na wengine kwanza. Hata kama anajua jambo, ana kipaji, hawezi kuamini katika uwezo na nguvu hizo hadi watu wengine wamthibitishie kuhusu usahihi na ubora huo.
3.Kujilinganisha katika kufanya mambo au thamani.
-Wengi tunakabiliwa na kutojiamini kwenye eneo hili. Tunajilinganisha sana na wengine. Tunafanya mambo yetu mengi kwa kushindana na kujilinganisha kuliko kufanya kwa ajili yetu na kwa viwango vyetu. Unanunua gari, siyo kwa sababu unahitaji gari, bali kwa sababu fulani amenunua gari, unataka kumuoneshea. Kila unachofanya ni kwa sababu ya wengine, siyo kwa sababu yako.
4.Kujishusha au kujipandisha thamani kuliko wengine.
-Kuringa na na kutamba ni dalili ya kutojiamini na sio kujiamini, kama wengine wanavyodhani. Mtu anayeringa na kujikweza sana anajaribu kupunguza maumivu ya hisia zake zilizo chini kuhusu thamani yake. Hii ni sawa na kujishusha. Mtu anajishusha kwa sababu anaamini kwa kujishusha watu watamwona ni wa maana na anayestahili. Lakini bado kujishusha maana yake ni kutafuta huruma na kukubaliwa na wengine, kutokana na hisia za kuwa mtupu. Mtu anayejishusha na yule anayejikweza wote ni mtu mmoja, bali wenye pande mbili tofauti. Kujikweza na kujishusha ni jambo lile lile kwa sura mbili tofauti.
5.Kutaka kuwafurahisha wengine kwa gharama, hasara yake.
-Asiyejiamini yuko tayari kuumia, lakini awafurahishe wengine, yaani wengine wamuone kuwa wa maana au wasimshushe. Mtu anatakiwa kulipa mchango wa tukio fulani, yaweza kuwa mchango wa harusi au harambee ya kuchangia jambo fulani ambapo kiwango kilichopangwa labda ni shilingi 20,000 tu. Lakini mtu huyu anaweza kusimama na kutangaza kutoa mchango mkubwa kupita kiasi kilichopangwa wakati fedha hizo hana, ili tu kujionyesha kwamba na yeye anazo. Mwisho wa siku anaingia kukopa na kulipa fedha hizo kwa maumivu makubwa sana. Angeweza kulipa kiwango alicho nacho au hata kama hana kuwa mkweli. Hapana, anataka wengine wamuone wa maana, lakini kwa gharama inayompa maumivu makubwa sana. Mifano ni mingi, lakini huu mmoja nadhani unakupa picha nazungumzia watu wa namna gani.
6.Kuogopa kuwajibika na kutupia wengine mizigo.
-Wengi tuna udhaifu huu, mtu asiyejiamini, hayuko tayari kuwajibika, kwani kuwajibika kunamfanya ahisi kushuka. Kwa hiyo ili asishuke, hata akikosea, atajitahidi kusingizia au kuwatupia wengine lawama. Hata kwenye kosa la wazi kabisa, ataanza kutafuta kosa dogo hata la mwaka juzi na kulitumia kosa hilo, kujisafisha. Hebu kagua kwenye uhusiano, hasa kwenye ndoa utaona sana udhaifu huu ukijitokeza. Mpenzi au mke anabeba mimba, mwanaume anakuwa wa kwanza kulaumu. Mwanaume anaweza kusema kwa kejeli na kulaumu, hayuko tayari kuwajibika kwamba hata yeye ana mchango katika jambo hilo. Kwake yeye mwanamke ndiye mwenye makosa.
7.Kutumia nguvu nyingi kulinda hadhi ya uongo.
-Kuna watu ambao wanaazima magari, wanaazima nguo na vitu vingine ili waonekane kuwa watu wa maana. Hufanya hivyo kwa matumizi ya nguvu nyingi kiakili, kihisia na kimwili ili wajionyeshe. Kuna idadi kubwa ya watu ambao hulinda hadhi za uongo kwa lengo la kutaka kuonesha kwamba, wana thamani. Hii kwa kawaida, ni tabia ambayo inatokana na kutojiamini.
8.Kuogopa sana au kutokuwa tayari kukosolewa, lakini kupenda sana kukosoa.
-Mtu asiyejiamini anaogopa na kuchukia sana kukosolewa. Ukimkosoa, bila kujali kama ni kwa njia ya kujenga au kubomoa, hatakubali. Mtu asiye jiamini ana kawaida ya kujihami sana, ili asionekane au kujulikana kuwa hajui au hawezi. Kwa hiyo, kumkosoa ni sawa na kumtia msumari wa moto kwenye kidonda. Ili sasa asionekane kuwa hajui, ili udhaifu wake usionekane, anakuwa na kawaida ya kuwakosoa wengine. Anataka wengine waonekane kuwa hawawezi, hawana nguvu, hawastahili na mwengine yanayofanana na hayo. Lengo lake ni kuwashusha hao wengine, akiamini kuwa, hiyo itampandisha yeye.
9.Aibu za ziada na kushindwa kutazama watu usoni.
-Mara nyingi aibu ni dalili ya mtu kushindwa kujiamini. Kwa kutojiamini, mtu anahisi kama vile, kila anachofanya kinaonwa na kufanyiwa tathmini, hivyo anaogopa atakosea na kila mtu atajua. Hiyo hasa ndiyo maana ya aibu. Aibu nyingine ni matokeo ya mtu kuamini kwamba, hana thamani, ukilinganisha na wale watu alionao. Hivyo, kwa kuhisi hana thamani, hujiona kama yuko chini mbele ya wale anaoamini kuwa wanathamni zaidi.
10.Kutawaliwa na majuto ya jana na hofu za kesho.
-Watu wasiojiamini wamejaa majuto ya siku za nyuma na wamesheheni hofu za maisha yao ya baadaye. Ni mara chache kwa mtu asiyejiamini kuishi maisha ya leoleo. Kama hajuti kuhusu maisha yake yaliyopita, basi atakuwa amejaa hofu za maisha yake ya kesho.

NJIA ZA KUKUFANYA UONEKANE NI MTU UNAEJIAMINI.

Njia za kukufanya uonekane ni mtu unayejiamini.
1. Jijengee mazoea ya kuongea kwa sauti kubwa ya kusikika vizuri na epuka kutamka maneno vibaya.
2. Unapokuwa umesimama simama wima, usiweke mikono mfukoni na pia usijiegemeze kwenye kitu chochote.
3. Unapoongea na mtu jipe nafasi ya kutosha kwa kuwa karibu na mtu unayeongea naye bila kumsogelea sana, yatawale mazingira yako. Tumia mikono yako kuelewesha kile unachokisema. Kama umekaa kwenye kiti basi kaa kistaarabu, pia unaweza weka miguu yako mkao wa kukunja nne lakini chunga usijilegeze na kuonekana umejitandaza.
4. Wakati wote jitahidi kutulia bila kujionyesha una wasiwasi. Ondoa wasiwasi unaoweza kukufanya usikae mahali kwa amani. Jitulize bila kuhofia kitu chochote, pumua taratibu na utajisikia vizuri mapigo yako ya moyo yatakuwa sawa na mwili wako utapata nguvu.
5. Unapoongea na mtu muangalie machoni kwa kuonyesha uso wa bashasha. Kuwa makini kumsikiliza na tikisa kichwa pale unapoafiki anachokuambia kama ishara ya kuwa unampata na kuelewa anachokwambia lakini usimkodolee macho sana. Unaweza pepesa macho pembeni lakini isiwe mara nyingi sana kuonekana husikilizi au una aibu.
6. Jiheshimu na jithamini uwe mtu wa kuheshimiwa. Watu watakuchukulia kwa namna utakavyojiweka. Kwa kadri utakavyojiheshimu na kujiona wewe yu jasiri ndivyo watu pia watakavyokuona.
7. Unapotaka kuangalia pembeni, zungusha kichwa upande kuelekea mahali unapotaka kutazama bila kujigeuza mwili mzima. Tazama bila kupepesa macho sana kuonekana unahofia kitu fulani.
8. Jitahidi sana kuwa mwenyewe, usitake kuigiza mtu mwingine anachofanya. Unaweza kujifanya kama mtu fulani kwa muda ikiwa tu unataka kujifunza kujiamini na kuwa kama yeye. Lakini utakapokuwa umeshajenga ujasiri ni vizuri ujiongoze mwenyewe kwa kufanya mazoezi zaidi ya kuongeza ujasiri wako. (Mfano kwa kuongea mbele ya umati wa watu, kujieleza na kumshawishi mtu afanye unalotaka nk)
9. Kama unategemea kuwasilisha ujumbe kwenye mhadhara au mkutano (kwa maana ya kufanya presentation) jiandae vyema na mapema kabisa hasa pale presentation inapokuhitaji uwe na notes au muongozo wa nini unatakiwa uwasilishe ili kuepusha kutoweza kusoma na kutamka baadhi ya maneno vizuri.
10. Vuta pumzi kila unapokuwa na hofu ya kushindwa kufanya kitu fulani kisha jiambie"NAWEZA"kisha fanya kitu hicho bila kufikiria kuwa utashindwa.
11. Fanya mambo yako kwa umakini na jiamini kuwa kila kitu kitakwenda vizuri, kwa kufanya hivyo utaonekana kwa watu unajiamini kwa kile unachoweza kufanya. Ni vizuri kujenga hisia za ujasiri ndani yako kuwaUNAWEZAkufanya lolote bila uwoga.
13. Unapokuwa unaongea na kuhisi sauti yako haitoki vizuri, kunywa maji kama unadhani mate yatakuwa yamekukauka na rekebisha koo kisha hesabu 1, 2, 3 mpaka 20 kwa kupaza sauti kwa kadri unavyokaribia kufika ishirini.
14. Unapoongea na mtu/watu zaidi ya wawili, jitahidi kumiliki ujumbe wako kwa kueleza vizuri kile unachosema. Kama hutoweza kusema vizuri ni rahisi mtu mwingine kukusaidia kuelezea hivyo utaonekeana hujajipanga. Jipange vizuri kwa kujua nini unataka kuongea kabla ya kuanza kuzungumza.
15. Ongea kwa kutamka maneno vizuri bila kwenda mbio na jitahidi kutoongea sana. Ongea kwa kiasi kisha tulia kwa sekunde kisha endelea. Hakuna sababu ya kutaka kuongea mengi bila kusimama lengo ni ujumbe ufike kwa wale wanaokusikiliza. Ukiongea kwa haraka utaonekana hufahamu vizuri unachokisema hivyo unataka kumaliza haraka.
16. Onyesha kujipenda kwa kutabasamu au kucheka kila unapofurahishwa na jambo fulani. Amini usiamini tabasamu humfanya mtu aonekane hana wasiwasi wowote kwa kuwa anajiamini.
17. Unapoongea unaweza pia kutumia misemo iliyowahi kusemwa na watu wengine kuhusiana na mada mnayoongelea ili kuongeza msisitizo wa kile mnachokiongelea.
18. Unaposhindwa na jambo jitahidi kutokuonyesha umejisikia vibaya kushindwa. Kukunja sura kwa huzuni au kwa kukasirika baada ya kushindwa jambo fulani kutakufanya uonekane umefadhaishwa na aibu.
19. Ni muhimu kuonyesha uaminifu na uadilifu wako kwa watu. Kujiamini kunaendana na kuaminika. Ukiwa unajiamini halafu huna maana kwa watu ni sawa na kujigamba pasipo kuwa na lolote la kujivunia. Jisikie kuwa wewe ni jasiri na mwingi wa furaha, onyesha uungwana wako kwa watu nao watakuthamini.
Makala nyingine za kupitia:
*. Dalili kumi (10) za mtu asiyejiamini.
*. Namna ya kupunguza msongo wa mawazo.
*. Sababu kumi (10) za wewe kuwa jasiri.
Kama unachochote cha kuongeza kuhusiana na mada hapo juu, tafadhali usisite kutoa maoni yako!

Tuesday, October 22, 2013

Simu

Ni hayo

HOW TO DEVELOP YOUR COMMUNICATION SKILLS.

How do you develop your communication skills?


Oral communicationis the ability to explain and present your ideas in clear English, to diverse audiences. This includes the ability to tailor your delivery to a given audience, using appropriate styles and approaches, and an understanding of the importance of non-verbal cues in oral communication. Oral communication requires the background skills of presenting, audience awareness, critical listeningand body language.
Back to top
Written communicationis the ability to write effectively in a range of contexts and for a variety of different audiences and purposes, with a command of the English language. This includes the ability to tailor your writing to a given audience, using appropriate styles and approaches. It also encompasses electronic communication such as SMS, email, discussion boards, chat rooms and instant messaging.Written communication requires background skills such as academic writing, revision and editing, critical readingand presentation of data.
Back to top
Non-verbal communicationis the ability to enhance the expression of ideas and concepts without the use of coherent labels, through the use of body language, gestures, facial expression and tone of voice, and also the use of pictures, icons and symbols.Non-verbal communication requires background skills such as
audience awareness, personal presentationand body language.
Back to top
Background Skills
Revision and editingis:
*.Applying techniques to improve writing or presentation. Proofreading for spelling, grammar and style.
Back to top
Presentation skillsis:
*.Using appropriate technologies and techniques to present information to an audience (for example, in a tutorial, seminar, lecture or meeting).
Back to top
Academic writing skillsis:
*.Writing in order to analyse a topic closely, develop a point of view in relation to that topic through research and thought, and persuade your reader that the point of view you have developed is well supported by the ideas and information you present (for example, an essay, poster, paper or thesis).
*.Writing a clearly structured document that presents an account of what has happened in a practical session or as part of an experiment (for example, an experimental report or journal).
Back to top
Audience awarenessis:
*.Understanding the needs, experience and level of understanding of an audience (for example, the public, students, employers, stakeholders).
*.Displaying sensitivity to your audience in organising and presenting ideas, and responding to feedback (for example, favouring plain language over jargon when communicating with the general public).
*.Understanding the particular perspective of professionals in your field and communicating appropriately with colleagues (for example, presenting data at a seminar in a standard style for that field).
Back to top
Critical listening/readingis:
*.An awareness of both the content of the message and the style and method of communication, and an understanding of how the content and method combine to create the meaning of the message (for example, results published in a scientific paper may be given more credibility than results presented at a departmental seminar).
*.Actively listening, reading or viewing information to gain a complete and accurate understanding of the communicated message (for example, noting the steps in a presented argument, or extracting specific detail from an academic paper).
Back to top
Personal presentation and body languageis:
*.An understanding of and ability to use gestures, expressions and non-verbal cues to help communicate a message (for example, using changing the tone and volume of your voice to convey emotion and feeling, or controlling posture and nervous gestures to present confidence).
Back to top
Presentation of technical or scientific datais:
*.An understanding of the use of images, graphs and other methods to present data simply and concisely (for example, using appropriate graphing techniques in a scientific report, or well-chosen graphics to convey a concept).

Friday, October 18, 2013

NAMNA YA KUTUNZA AFYA YA AKILI NA MWILI WAKO.

Namna ya kutunza afya ya akili na mwili wako.
Afya ni hazina ya pekee inayotufanya tuishi kwa raha. Akili pia ni kitu muhimu kinachoendesha utendaji kazi wa mambo mengi katika miili yetu. Hatuwezi fanya jambo lolote la maana ikiwa hauna afya njema ndio maana ni muhimu kutunza afya zetu ili tuweze kuendelea kuishi vizuri na kuendelea kufanya shughuli za kujenga taifa.
Afya bora hujengwa na mambo kadha vikiwemovyakula bora, ufanyaji wa mazoezi ya mwili na kuishi katika mazingira safi na tulivu kwa maisha ya mwanadamu.
Kwa kulijua hilo soma mambo yafuatayo yatakayokusaidia kutunza afya yako...
1. Kula vyakula bora.
-Chakula ni dawa, ni vyema ukawa daktari wa mwili wako kwa kula vyema na kuwa mwenye afya bora na imara. Kila siku jitahidi kula chakula chenye virutubisho vingi vya vyakula tofauti tofauti (Live smart by eating a well balanced diet). Kula wanga na protini kiasi, mboga za majani na matunda kwa wingi. Kujua aina ya matunda na faida yake BONYEZA HAPA.
2. Kunywa maji mengi( kiasi cha lita 2 kwa siku ).
-Maji ni kinywaji chenye faida kubwa mwilini, kunywa maji kila unapofanya kazi. Kujua mengi kuhusu manufaa ya maji mwilini BONYEZA HAPAkusoma makala yangu niliyokwishawahi kuandika kuhusu sababu za maji kuwa ni muhimu kwa afya yako.
3. Pumzisha mwili wako.
-Lala kila unapojisikia usingizi hata kama ni mchana, watu wengihufikiri kulala mchana ni uvivuHAPANA, kama una nafasi sinzia kwenye kochi angalau kwa dakika 10 kisha endelea na kazi zako. Jipumzishe ili kuupa mwili wako muda wa kukusanya nguvu tena. Wewe sio dubwana (robot) ufanye kazi bila kupumzika, pumzika na ufute pumzi kwa afya.
4. Fanya mazoezi ya viungo.
-Mazoezi ni muhimu sana kwa afya yako, hata kama upo busy kiasi gani tafuta angalau dakika 20-30 kwa siku ufanye mazoezi iwe asubuhi au jioni. Mazoezi huondoa sumu mwilini kama hewa chafu, sumu itokanayo na vyakula tunavyokula na pia kwa kufanya mazoezi utaweka viungo vyako vizuri na kuviimaarisha.Angalia hii video hapa chini inaonyesha namna ya kufanya mazoezi nyumbani kwako bila kutumia vifaa vyovyote.
5. Penda kuchemsha bongo.
-Watu wengi hutamani kuwa ‘’GENIUS’’, ukitaka kuwa genius jijengee tabia kila siku ya kusoma mambo mengi tofauti tofauti ili uongeze uwezo wako wa maarifa (general knowledge). Soma kitu kipya kila siku kama mambo ya sayansi na teknolojia, jiografia ya ulimwengu, historia, lugha au mazingira yanayokuzunguka. Pia kula vyakula vya kuchangamsha ubongo na kuongeza uwezo wako wa kuhifadhi kumbukumbu kama njugu mawe, samaki wa kuchemsha (omega-3 amino acids), parachichi, maboga, karanga nakadhalika.
6. Cheza, imba au sikiliza music kila utakapojihisi umechoka.(RELAX!...)
-Mimi ni mpenzi wa R n B na rap wewe je? Amini usiamini muziki unaondoa stress kama unavyoongalia au kusikiliza vichekesho yani comedy. Nakushauri usikilize muziki, uimbe au kucheza kila unapohisi umechoka au umetingwa na mawazo mengi. Unajua ni kwanini kuna muda unatakiwa kujisahaulisha mambo yaliyo kichwani kwako kwa ku RELAX!!!...? ni kwasababu kichwa chako kinauwezo wa kubeba mambo mengi sana kuliko unavyofikiri. Jinsi unavyozidi kuongeza mambo kwa kufikiri matatizo yako ndipo unapozidi kuongeza msongo wa mawazo.
7. Kunywa chai kuchangamsha mwili.
-Chai huchangamsha ubongo na kufanya akili yako kuwa hai na kuongeza wepesi wa kufikiri kwa muda huo. Napendelea kunywa chai ya kijani (green tea) kuliko chai nyeusi (black tea), kujua kwanini nasema hivyo BONYEZA HAPAusome makala yangu niliyowahi kuandika kuhusu faida za kunywa chai ya kijani dhidi ya chai nyeusi.
8. Kama wewe ni mnywaji pombe, jitahidi kunywa kiasi kwa kujitambua.
-Starehe na kwa afya ni kunywa chupa 1 hadi 2 basi, zaidi ya hapo ni kujitafutia matatizo. Watalaamu wameeleza kunywa pombe kiasi kuna faida zake ambazo ni chache lakini utakapo kunywa pombe kupita kiasi hasara ni nyingi zikiwemo kukumbwa na matatizo ya kupoteza kumbukumbu, saratani za ini, koo, matiti, maradhi ya moyo na mengine mengi.
9. Jitahidi kukaa kwenye mazingira safi na tulivu.(hewa safi ni muhimu sana)
-Moja ya tatizo kubwa la miji mikubwa hapa nchini ni uchafuzi wa mazingira. Sisi binadamu hutegemea mazingira safi kwa maisha yetu, kama nyumbani kwako au kwenu hakuna miti basi ni vyema ukapanda ili mpate hewa safi na kivuli. Uwapo ofisini, nyumbani au sehemu yeyote ambamo hakuna uwazi mkubwa wa kupitisha hewa fungua madirisha ili uruhusu hewa safi kuingia ndani. Kama kuna kiyoyozi (air conditioner) unaweza ukawasha pia ili mradi tu upumue vizuri.
10. Cheka na kufurahi angalau mara kadhaa kwa siku.
-Hakuna kitu kinachotumaliza vibaya sisi wenyewe ndani kwa ndani kama HASIRA, KINYONGO, UNYONGE na KIBURI kwa kununa. Kuwa na jazba hakutatui tatizo lolote, furahi pale unapofurahishwa na cheka pale unapochekeshwa. Kucheka na kufurahi ni tiba ya msongo wa mawazo kwasababu huchangamsha na kusawazisha akili.

NAMNA YA KUONDOA UCHOVU UNAPOJIHISI UMECHOKA.

Namna ya kuondoa uchovu unapojihisi umechoka.

Kuna sababu nyingi za mtu kuchoka, unaweza kuchoka baada ya kufikiri au kutafakari sana kwa muda mrefu bila kutuliza akili (msongo wa mawazo). Vilevile uchovu unaweza kuwa ni wa mwili uliosababishwa na kufanya kazi nyingi au kazi nzito bila kupumzika. Uchovu ni dalili ya kuonyesha na kudhihirisha kuwa mwili wako unahitaji mapumziko ili uweze kurudia katika hali yako ya kawaida ya kuwa na nguvu.
Kupumzisha mwili na akili yako ni afya hivyo ni muhimu ujue namna za kujipumzisha kila unapokuwa umechoka na kurejesha mwili wako katika hali ya kawaida. Hizi hapa ni njia mbalimbali za kukusaidia kuondoa uchovu unapokuwa umechoka.
1. Kunywa kinywaji laini au kula chakula chepesi chenye kukupa nguvu.
-Maji au juisi fresh ya matunda ni nzuri sana, unapokunywa kinywaji laini mwili wako unapata nafasi ya kurudisha na kufiidia maji yaliyopotea mwilini na kurejea katika hali nzuri. Unaweza pia kula keki, crips, biskuti au kitafunio chochote kizuri cha kukuongezea nguvu lakini kumbuka usile vyakula ovyo (chips mayai, mishikaki, mihongo ya kukaanga nk) hasa vyakula vya magengeni kwakuwa sio vya kuaminika(kiusalama na kiusafi) na pia sio vizuri kwa kujenga afya yako.
2. Jipumzishe kwa kulala mahali safi na tulivu.
-Wakati mzuri wa kulala ni usiku kwasababu hakuna kelele za hapa na pale na pia kuna utulivu wa hali ya juu ukilinganisha na wakati wa mchana. Kiafya unatakiwa kulala kwa muda wa saa 6-8 na si vinginevyo. Ukilala sanakupitiliza ulalaji wa kawaida utauongezea mwili wako uchovu kwa kuwa na‘’depression’’. Kwa wakati wa mchana, unaweza ukajipumzisha kwa kusinzia kwa dakika chache 10-15 kwenye kochi kisha utakapojisikia vizuri endelea na kazi zako nyingine. Kumbuka lengo la kulala ni kuupumzisha mwili na ubongo ili upate nguvu na kuongeza ufanisi wake wa kiutendaji kazi. Zingatie usingizi bora (Quality Sleep) kwa afya bora.
Kujua zaidi: Soma Tips on how to improve your sleep.
3. Sikiliza muziki utakaokufanya ujiliwaze au pata burudani nyingine ya aina yeyote ya kukuchangamsha.
-Ala nzuri za muziki zinaweza kukuondolea msongo wa mawazo na kujihisi vizuri mwenye furaha. Kusikiliza wimbo na kucheza peke yako ni njia moja wapo ya kujichangamsha hasa pale unapofuatilia maneno yanayoimbwa katika wimbo huo. Raha ya muziki ni pale unapoimba na kwenda sambamba na ujumbe wa kile kinachoimbwa. Fanya hivyo na baada yaburudaniutajikuta hali yako imebadilika nakuwa nzuri kabisa.
4. Jinyooshe kwa kufanya zoezi dogo.(Pushups, Kusimama na Kukaa kwa Haraka haraka nakadhalika)
-Uchovu unaweza kusababisha jointi na viungo vingine kama kiuno kukaza. Dawa ya tatizo hili ni kufanya zoezi la kujinyoosha. Unajua kwanini nimesema ufanye zoezi la kupiga pushups? Pushup ni zoezi la kawaida tu lakini ukilifanya ipasavyo litaweka mwili wako sawa. Unashauriwa kila siku uamkapo asubuhi ukiweza piga pushups 60-100. Hii ni kwasababu pushup ni zoezi ambalo hupasha mwili kwa haraka, huboresha misuli, upumuaji wa mapafu na kufanya mzunguko wa damu kuwa mzuri.
Unaweza soma pia: Je unajua manufaa ya kufanya mazoezi.
5. Tafuta mahali penye hewa safi upunge upepo.
-Njia ya haraka ya kukufanya ujisikie vizuri ni kukaa au kutulia mahali penye upepo mwanana kwa dakika kadhaa. Labda unapenda kukaa mahali penye kivuli kizuri cha miti au ghorofani penye uwazi mkubwa wa kusimama na kuangalia mandhari mazuri ya mahali ulipo. Vyovyote vile lengo ni kupunga upepo na kutuliza akili bila kuwaza mbali au kufikiri mawazo ambayo yataendelea kukufanya ujisikie vibaya.
6. Cheza michezo ya kukuburudisha.(Computer and Mobile games)
-Kwenye simu za mkononi au computer kuna michezo kwaajili ya kujiburudisha. Kwanini usitumie angalau dakika 8 kucheza game ‘’angry bird’’ kwenye iPhone, iPad au ‘’karata’’ kwenye computer ili kuburudisha akili kisha uendelee na mambo yako mengine. Tusijichoshe sana kwa kuchat kwenye chatting messengers kama whatsapp, google talk nakadhalika bali tujenge tabia ya kupenda kitu kwa kiasi na si sana mpaka kupitiliza.

NJIA ZA KUPUNGUZA UNENE WA MWILI.(second release)

2. Kunywa maji kwa wingi.(glasi 8-10 kwa siku)
Maji ni kinywaji asilia na muhimu sana kwa afya yako, usipende kunywa sana soda au vinywaji vyenye sukari nyingi. Wengi wetu hupendelea kunywa zaidi chai au soda (vinywaji baridi kama Cocacola, Pepsi, Redull nk). Vinwaji vingi jamii ya soda vina gesi ambayo sio nzuri kwa afya yako kwasababu huongeza uwezekano wa mtu kupata vidonda vya tumbo. Kunywa maji lita 2 kwa siku na pia unashauriwa kunywa maji dakika 10-20 kabla ya kula chakula au nusu saa kuendelea baada ya kupata chakula.Ni kwasababu utakapokunywa maji kabla ya chakula itakusaidia kutokula chakula kingi kupita kiasi kwakuwa utakuwa umeshiba hivyo utaepukana na kula sana ambapo kunaweza kukuongezea uzito wa mwili na hasa kunenepa.
Wakati wa kula chakula usinywe maji kwa kubugia harakaharaka hata kama una kiu kali ya maji. Hii ni kwasababu unapokula chakula huku unabugia maji unapunguza nguvuya chakula,unajaza tumbo maji na kuchelewesha mmeng’enyo wa chakula (digestion). Chakula kisipomeng’enywa vizuri kitaketi tu tumboni. Matokeo yake hali hii ikiendelea kwa muda mrefu itakusababishia kitambi uonekane na tumbo kubwa ambalo si zuri. Kama hutofanya mazoezi ya kusawazisha mwili wako hasa tumbo, hali hii itasababishatumbo kwenda pembeni (chini ya mbavu) hasa kwa watu wa makamo na kuleta maradhi kama kisukari, kiungulia, kuvimbiwa, uyabisi wa tumbonakadhalika.
3. Tafuna chakula vizuri.
Chakula huanza kumeng’enywa au kusagwa mdomoni. Mate ni chanzo cha uchambuaji chakula. Unapobugia chakula bila kutafuna sawa sawa unasababisha mambo mawili. Moja chakula kutochambuliwa vizurinapili chakula kwenda kukaa tumboni bila kutumika au kama kikipita hakitatumika ipasavyo mwilini.
Tafuna chakula taratibu na kwa uhakika ili kusaidia umeng’enyaji mzuri kwa matumizi ya mwili. Ukitafuna chakula vizuri pia utakuwa unajiepushia matatizo kama ya kuvimbiwa, kupata choo kigumu nakadhalika.
4. Punguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi.
Mafuta yanahitajika kwa kiasi mwilini, ni vyema ukala vyakula vyenye mafuta kwa mpangilio mzuri unaohitajika mwilini. Kula vyakula kwa kuuwianisha viwango sahihi vya vyakula hivyo(Eat a Well Balanced Diet which Contain Foods at Right Proportion).Chakula bora kilichokamilika hujumuisha wanga (mfano ugali, ndizi, wali, viazi, mikate, mahindi, nk), protini (mfano mboga na nyama), madini (mfano mbegu mbegu mbichi ambazo hazija kaangwa sana, chumvi nk) na “vitamini” (matunda, maziwa, mayai, nk).
Nyama ni muhimu sana kwasababu ina madini aina ya chuma (hasa kwa nyama nyekundu), protini, mafuta na pia inaongeza nguvu. Ila mafuta yaliyoko katika nyama si mazuri kwasababu huganda mwilini. Unashauriwa kula zaidi nyama ya samaki kwakuwa mafuta yake ni mazuri na yana Omega-3 fattyacids ambayo husaidia kuongeza kinga ya maradhi mwilini na pia ni chakula bora kwa afya ya ubongo wako.
PENDEKEZO:Kula korosho, karanga (ziwe mbichi badala ya kukaanga na chumvi kidogo) kuliko nyama kwasababu mafuta yake ni yenye rotuba kuliko mafuta ya kwenye nyama vilevile hayawezi kukuongezea unene.
5. Fanya mazoezi ya mwili na viungo.
Mazoezi ninjia nzuri sana na ya pekee ya kupunguza unene, fanya mazoezi ya kukufanya moyo uendo mbio (cardio excercises) kama kukimbia, kuogelea, kuendesha baiskeli nk yatakusaidia kuchoma na kuyayusha mafuta mwilini.Ni vyema ukafanyamazoezi mpaka mwili utokwe na jasho kwani hiki ni kipimo kizuri cha kudhihirisha umefanya zoezi kwa kiwango stahiki na umeondoa sumu na taka nyingine mwilini. Kama wewe ni mwanachama na unahudhuria GYM kwenda kufanya mazoezi nakushauri uwe na mshirika wa kuwa unafanya naye mazoezi, mkiwa wawili au hata watatu sio mbaya kwa pamoja mtashindana kufanya mazoezi vizuri na ipasavyo. Vilevilemtapeana moyo kuendelea na mazoezi yenu kilaitokeapo mmoja wenu anajihisi kukata tamaa.
Mfanomzuri zaidi wa namna ya kufanyamazoeziukiwa nyumbanitumia dakika 10 kuangaliahiyo video clip hapo chini, inaonyesha namna ya kufanya mazoezi ipasavyo yatakayokusaidiakuchoma calories mwiliniilikupunguza unene na uzito wa mwili.
6. Jiwekee malengo thabiti ya kutaka kupunguza unene.
Kupunguza mwili na kuona mabadiliko sio jambo la muda mfupi, linahitaji uvumilivu na subira hasa pale unapokaribia kukata tamaa. Zingatia ulaji bora wa mlo wako wa kila siku na fanya mazoezi ipasavyo bila kuchoka au kuzembea. Ni vyema ukawa na notebook ya kuandika chini maendeleo yako. Mfano unaweza kujiwekea malengo ya kupunguza kilo 1 kila baada ya wiki,ni vyema ukashikiliamsimamo wako mpaka ufanikiweufikie mahali ujionena kujiridhisha kwa kujipima ukubwa wako wa sasa na kulinganisha na vipimo vyako vya zamani.
Kwa hayo machache naamini ukiyafanyia kazi yatakusaidia kupunguza unenewa mwili wako na kuwa mwenye umbo zuri la kuvutia. Kila la heri na nakutakia afya njema!...

NJIA ZA KUPUNGUZA UNENE WA MWILI WAKO.

Njia za kupunguza unene wa mwili wako.


Wastani wa maisha ya mtanzania (na waafrika wengi) ni miaka 40-50. Kati ya sababu kuu zinazopunguza uhai ni kuwa na afya mbovu,makala ya leo inahusu tatizo la unene wa mwili.Tatizo hili la unene na uzito uliozidi sababu yake kuu nikutokujua namna ya kutunza mwili wako kwa kula vizuri na kufanya mazoezi. Unene usio wa kawaida ni tatizo kubwa kwa watu wengi hivyo kama wewe ni mmoja wapo na unataka kupunguza mwili wako, hizi hapa ni njia za kukusaidia kupunguza unene na kuwa mtu mwenye muonekana mzuri na afya njema.
1. Kula vizuri.
Ipo mifumo miwili ya kula vizuri. Kwanza ni chakula unachokula na pili ni namna unavyokilachakula hicho.
*.Ulaji bora wa chakula.
Kuna ulaji wa kula vyakula vidogo vidogo vyenye madini, vitamini, mafuta nk mara nyingi kwa siku au kula milo michache (mmoja au miwili) mikubwa ili kujaza tumbo. Ulaji mdogo mdogo husaidia afya na kuingia mwilini vyema kuliko ulaji mkubwa wa mara chache. Tumbo lina misuli inayofanya kazi kama mashine au mnyama. Gari likijaa sana hupata taabu kwenda. Punda hivyo hivyo. Ulaji mdogo mdogo ni bora maana mwili unachambua kila kitu kwa wepesi na haraka. Unapokula milo michache mikubwa unaparilia zaidi mafuta mwili na kusababisha kukaa kwa mafutatumboni bila kutumika ambapo baadae itapelekea mtu kupata kitambi.PENDEKEZO:Asubuhi kunywa maji kwanza, matunda, kisha ndiyo unywe chai na vitu vingine kama mkate au maandazi.
Namna ya kula matunda na mboga za majani kwa mpangilio mzuri.
Watu wengi hukosea kula matunda na mboga za majani kwa usahihi. Nasema hivyo kwa maana ya kwambawengi hula matunda baada ya chakula, hii si namna nzuri ya kula kwasababu vimeng’enya chakula (enzymes) zilizopo tumboni hufanya kazi kwa namna tofauti. Enzymeshizi namna zinavyonyambua na kumeng'enya matunda ni tofauti na namna zinavyomeng’enya vitu vigumu kama nyama au vyakula vingine jamii ya wanga hivyo matunda hunyambuliwa haraka zaidi kuliko vyakula vingine. Ni bora kula matunda dakika 10-20 kabla ya kula chakula kwasababu unapokula matunda baada ya kupata chakula hugeuzwa na kuwa aina fulani ya pombe (fermented food) inayoelea juu ya chakula na kubakia kitu kingine badala ya kuingizwa haraka ndani ya mfumo wa damu kupitia utumbo mdogo, wengu, moyo, ininakadhalika.
Mseto wa vyakula ni muhimu. Kwa mfano vyakula vyenye uchachu (“acid”) na vile vinavyomung'unyuka haraka (“alkaline”) havitakiwi viliwe kwa pamoja. Mfano mzuri ni matunda. Matunda yenye uchachu kama machungwa, mananasi na maembe yanatakiwa yaliwe pamoja na yale laini zaidi kama ndizi mbivu, matikiti maji, mapapai, matufaha, nk nayo yaliwe kivyake kwasababu mfumo wake wa kumeng'enywa ni tofauti.
Vilevile nyama nyeupe (nyama za ndege na samaki) unashauriwa ziliwe tofauti na nyama nyekundu (nyama za ng’ombe, mbuzi, kondoo nk) ziliwe tofauti.
*.Chakula bora kwa afya njema.Kula vyakula bora vyenye thamani kwa mwili wako, epuka vyakula vyenye sukari nyingi, mafuta mengi au chumvi nyingi badala yake zidisha kula mboga mboga zilipikwa kiasi bila kuiva sana mpaka kupoteza nguvu. Ni vizuri pia kula mboga mbichi kama salad (unaweza kuiita kachumbari vyovyote ujuavyo) si lazima iwe kachumbari ya nyanya, vitunguu na chumvi tu.
Waweza kuchanganya matango, nyanya na maparachichi au vitunguu saumu, giligilani na karoti. Huu mseto wa mboga mbichi ni mzuri ukila na chakula chenye nyama za minofu na wanga (ugali, wali, ndizi za kupika nk). Ulaji wa wanga asubuhi, mchana na jioni kila siku sio mzuri kwasababu huchangia kunenepa.
PENDEKEZO:Unaweza kula ugali kwa samaki, mboga za majani, matango na nyanya bila kuweka chumvi nyingi.
Inaendelea..

MAKOSA YA KUYAEPUKA KATIKA MAONGEZI.

Makosa ya kuyaepuka katika maongezi.

Kuongea na watu ni kitu ambacho tunafanya kila siku, tunaongea na ndugu, jamaa au rafiki iwe ni kubadilishana mawazo, kuelekezana na kuelewana au kuhabarishana mambo ya hapa na pale.
Mahusiano baina yako na watu wengine yanategemea sana maongezi yako ya kila siku nawatu unaohusiana naokwa maana ya namna unavyoongea nao, unavyowasikiliza kwa makini na kuchangia mawazo yako pale ushauri unapohitajika na mambo mengine yanayokusababisha uongee. Bila maongezi maisha yanakuwa badohayajakamilika kwakuwatunaishi kwa kutegemeanakimahusiano na mahusiano yetu na watu mbalimbalihuletwakwa kufanyamaongezi.Ni rahisi kwako kupata marafiki na kujuana na watu wengi ikiwa utakuwa mchangamfu na mcheshi katika kuongea.
Maongezi mazuri ni lazima yawe ni yenye maelewanona yenye mantiki ya kile mnachozungumza. Kujua makosa ya kutokufanya wakati unaongeani ujanja na busara pia kwasababukuongea vizuri na watu kunakuongezeasifa nzuri na kukuza mahusiano yako. Soma hapo chini mambo ya kuyaepuka unapokuwaunaongea na mtu.
1.Usiongee maneno mengi kwa haraka.
Unapoongea na mtu, ongea taratibu kwa sauti ya kusikika vizuri.Watu wengi hupenda mtu mtaratibu katika uongeaji.Kama utaongea kwa haraka itakuwa ni vigumu kwa anayekusikiliza kukuelewa vizuri nini unachomaanisha. Vilevile hatoweza kupata kikamilifumaneno yako yote unayomwambia. Hivyo ukitaka ueleweke vizuri kwa watu,jieleze kwa kuongea taratibu. Ukifanya hivyoutamfanya pia huyo unayeongea naye akuone ni mtu unayejiaminina unauhakika wa kile unachomweleza.
2. Usiulize maswali mengi ndani ya muda mfupi.
Ulishawahi kukutana na mtu muongeaji kupita kiasi?Anakuuliza maswali zaidi ya mawili kwa wakati mmoja. Hii sio namna nzuri ya kuwasilisha mambo yako katika maongezi.Kama una swali uliza kwa mpangilio maalum kwa kuuliza swali moja na ujibiwe kisha ulizajingine. Ikiwa utakuwa upo mahali ambapo mnaouliza maswali ni wengibasi nivyema ukapangilia maswali yako kinambari yani swali la namba1,2, 3....ili unapoyawasilisha maswali yakomsikilizaji aweze kukuelewa na kujipanga vizuri namna ya kukujibu maswali yakoipasavyo.
3. Usianzishe mada ambayo haieleweki au haivutii kwa msikilizaji.
Unapotaka kuongea kuhusu kitu fulani ni vyema kiwe chenye kupendeza masikioni mwa mtu au watu wanaokusikiliza.Ukianzisha mada ambayoinaaminika kuwa ni uongo au ni ngumu kufikirika kirahisina kueleweka vizuriitamchosha msikilizaji.Epuka kuongea matusi au umbea uliopitiliza kwani hakuna mtu anayependa kusikia mambo hayo sana vilevile utaonekana wewe ni mtu wa ajabuusiyejieshimu. Lakinipia unawezakuwa mcheshi kwa kuwafurahisha watu kwa vichekesho au kuwatania kwa kiasi fulani bila kuonekana wewe ni kitukoikiwa utafanya hivyo katika mazingira maalum na wakati muafaka wa kufanya hivyo.
4. Usifanye mambo mengine yatakayosababisha msisikilizane.
Inakera sana kwa mtu mwingine unayeongea naye kukuona ukifanya mambo mengine badala ya kumsikiliza. Mambo ya kuwa unaongea na mtu huku unamtumia mtu mwingine ujumbe kwenye simu au kuzungumza na mtu mwingine wa pembeni wakati unaongea na simu sio mazuri kabisana yanakera hata kama ukijaribukujitetea hutaeleweka. Pia wakati unaongea na mtu usiwaze mambo menginetofauti na maongezi yenu. Kosa ambalo watu wengi hufanya ni kupeleka akili zao mahali pengine badala ya kusikilizawanachoelezwa.(Always Let Your Mind Be Where You Are)
5. Usijaribu kujionyesha unajua kila kitu.
Ukijifanya wewe ni mjuaji, unayeongea naye atakuona wewe unajifanya kuwa ni‘’MUCH KNOW’’sana hivyo atasita kukueleza mambo mengine ambayo ni muhimu kwako kuyajua. Pia ukijiona unajua mengiutakuwa unajifunga wewe mwenyewe usijue mambo mengine ambayo huyajui kutoka kwa wengine. Kila unapopata nafasi ya kuongea na mtu msikilizekwamakinikwakuwa kila mtuana jambo au wazo ambalo wewe hulijui. Hata kama kile mtu anachokwambia unakifahamu msikilizepiakwasababuhuenda katika maelezo yake atakuongezea wazo ambalo ulikuwa hulifahamu hapo kabla.Kuwa mdadisi kwa kujifanya hujui kitu unapoongea na watu hakika utajifunza mengi sana kutoka kwao. Kumbuka maneno haya yatakusaidiakutoridhika kutakakujua mambo kwakuwa hakuna ajuaye yote''Stay hungry, stay stupid."

Mambo ambayo watu wengi hawapendi kusikia wakizungumziwa kuhusu wao.

Mambo ambayo watu wengi hawapendi kusikia wakizungumziwa kuhusu wao.
(Things that most people don’t like to hear about themselves.)
Katika maongezi huwa tunaongea mambo mengi sana yahusiyo Maisha, Michezo, Mahusiano, Siasa, Kazi nakadhalika. Ili uwe muongeaji mzuri usiyechukiza watu unao ongea nao ni hekima kuchunga kauli yako na kujua unaongea nini kwa mtu/watu wanaokusikiliza.
Watu unao ongea nao watavutiwa na kuendelea kukusikliza iwapo watapenda unachokiongea. Kwa upande mwingine kuongea na watu kunaweza kukujengea uhusiano mzuri au kubomoa uhusiano wenu. Kujua ni mambo gani watu hawapendi kusikia kutakusaidia kujua nini cha kusema na kipi cha kuacha kusema wakati wa maongezi yenu.
Yafuatayo ni mambo ambayo wanaume na wanawake hawapendi kusikia kuhusu wao.
Wanaume hawapendi kusikia mambo haya kuhusu wao.
1. Kumwambia kuwa hawezi kutunza pesa zake vizuri au ni mfujaji mali.
2.Kumwambia yeye hana akili au ni mjinga.
3. Kuimwambia yeye ni mfupi (andunje)
4. Kumwambia yeye si mcheshi au amezuuba sana.
5. Kumwamba anaonekana kama amezeeka.
6. Kumwambia kuwa yeye ni mwoga au dhaifu au ni mshamba wa mambo.
7. Kumwambia kuwa yeye hajui kujali au kubembeleza mwanawake.
8. Kumwambia kuwa yeye hana hela au ni maskini tu.
9. Kumwambia kuwa yeye ni bahili sana.
10. Kumwambia kuwa yeye hajui kuongea na watu vizuri. (domo zege)
11. Kumlinganisha yeye na wanaume wenzake waliomzidi kimaendeleo au kwa chochote kile.
-Kama wewe ni mwanamke na unataka kuimarisha au kukuza ujuzi wako wa kuongea na wanaume kuwa makini sana unapotumia maneno hayo kuzungumza na wanaume kwani wengi wao hawapendi kabisa kusikia wakiambiwa hivyo.
Wanawake hawapendi kusikia mambo haya kuhusu wao.
1.Kumwambia kuwa yeye hana umbo la kuvutia au ana kasoro na umbule lake.
2. Kumwambia yeye ni mnene sana au ameongezeka uzito.
3. Kumwambia kuwa yeye amezeeka.
4. Kumtajia umri wake kuwa yeye ni mkubwa sana.
5. Kumuuliza kama alishawi kuolewa hapo nyuma.
6. Kumfananisha yeye na mwanawake mwingine ambaye hapendezwi naye.
7. Kumwambia kuwa hajapendeza na nguo alizovaa.
8. Kumwambia kuwa yeye ana sauti mbaya siyo nyoror o ya kuvutia.
9. Kumuuliza yeye ana watoto wangapi ikiwa maongezi yenu hayahusu mambo ya kifamilia.
10. Kumlinganisha yeye na mwanamke mwingine amemzidi kwa kitu chochote. Mfano: Uzuri, Pesa, Mali.
Natumaini kuwa utakuwa umejua mambo ambayo watu hawapendi kusikia , huchukia kila wanapoaambiwa mambo hayo kuhusu wao. Kila mtu hupenda kusifiwa kwa namna yake ya kipekee, hivyo chunga usimfadhaishe mtu kwa kumzungumzia vibaya .
Mpe mtu sifa nzuri na stahiki kuhusu yeye na kwa pamoja mfurahie maisha kwakuwa kila mtu ana uzuri wake na kasoro zake!

Mambo ambayo watu wengi hawapendi kusikia wakizungumziwa kuhusu wao.

Mambo ambayo watu wengi hawapendi kusikia wakizungumziwa kuhusu wao.
(Things that most people don’t like to hear about themselves.)
Katika maongezi huwa tunaongea mambo mengi sana yahusiyo Maisha, Michezo, Mahusiano, Siasa, Kazi nakadhalika. Ili uwe muongeaji mzuri usiyechukiza watu unao ongea nao ni hekima kuchunga kauli yako na kujua unaongea nini kwa mtu/watu wanaokusikiliza.
Watu unao ongea nao watavutiwa na kuendelea kukusikliza iwapo watapenda unachokiongea. Kwa upande mwingine kuongea na watu kunaweza kukujengea uhusiano mzuri au kubomoa uhusiano wenu. Kujua ni mambo gani watu hawapendi kusikia kutakusaidia kujua nini cha kusema na kipi cha kuacha kusema wakati wa maongezi yenu.
Yafuatayo ni mambo ambayo wanaume na wanawake hawapendi kusikia kuhusu wao.
Wanaume hawapendi kusikia mambo haya kuhusu wao.
1. Kumwambia kuwa hawezi kutunza pesa zake vizuri au ni mfujaji mali.
2.Kumwambia yeye hana akili au ni mjinga.
3. Kuimwambia yeye ni mfupi (andunje)
4. Kumwambia yeye si mcheshi au amezuuba sana.
5. Kumwamba anaonekana kama amezeeka.
6. Kumwambia kuwa yeye ni mwoga au dhaifu au ni mshamba wa mambo.
7. Kumwambia kuwa yeye hajui kujali au kubembeleza mwanawake.
8. Kumwambia kuwa yeye hana hela au ni maskini tu.
9. Kumwambia kuwa yeye ni bahili sana.
10. Kumwambia kuwa yeye hajui kuongea na watu vizuri. (domo zege)
11. Kumlinganisha yeye na wanaume wenzake waliomzidi kimaendeleo au kwa chochote kile.
-Kama wewe ni mwanamke na unataka kuimarisha au kukuza ujuzi wako wa kuongea na wanaume kuwa makini sana unapotumia maneno hayo kuzungumza na wanaume kwani wengi wao hawapendi kabisa kusikia wakiambiwa hivyo.
Wanawake hawapendi kusikia mambo haya kuhusu wao.
1.Kumwambia kuwa yeye hana umbo la kuvutia au ana kasoro na umbule lake.
2. Kumwambia yeye ni mnene sana au ameongezeka uzito.
3. Kumwambia kuwa yeye amezeeka.
4. Kumtajia umri wake kuwa yeye ni mkubwa sana.
5. Kumuuliza kama alishawi kuolewa hapo nyuma.
6. Kumfananisha yeye na mwanawake mwingine ambaye hapendezwi naye.
7. Kumwambia kuwa hajapendeza na nguo alizovaa.
8. Kumwambia kuwa yeye ana sauti mbaya siyo nyoror o ya kuvutia.
9. Kumuuliza yeye ana watoto wangapi ikiwa maongezi yenu hayahusu mambo ya kifamilia.
10. Kumlinganisha yeye na mwanamke mwingine amemzidi kwa kitu chochote. Mfano: Uzuri, Pesa, Mali.
Natumaini kuwa utakuwa umejua mambo ambayo watu hawapendi kusikia , huchukia kila wanapoaambiwa mambo hayo kuhusu wao. Kila mtu hupenda kusifiwa kwa namna yake ya kipekee, hivyo chunga usimfadhaishe mtu kwa kumzungumzia vibaya .
Mpe mtu sifa nzuri na stahiki kuhusu yeye na kwa pamoja mfurahie maisha kwakuwa kila mtu ana uzuri wake na kasoro zake!

JINSI YA KUPIMA MAENDELEO YAKO KWA KUJIULIZA MASWALI HAYA.

Pima maendeleo yako kwa kujiuliza maswali haya.


Kwa mtu makini na hodari anayependa kujiendeleza iwe kiimani, kimahusiano, kiafya, kikazi au kitaaluma hujiwekea malengo na kumbukumbu ya mafanikio yakekila wakati anapopiga hatua.
Yafuatayo ni maswali kadhaa yatakayokusaidia kutafakari na kupima mafanikio au udhaifu wako ikiwa unadhumuni la kuwa mtu bora zaidi.
Jiulize maswali yafuatayo...
1. Umefanikisha nini katika miezi mitatu (3) iliyopita, na kwanini kitu hicho kilikuwa na maana kubwa kwako?
2. Je ulipata changamoto gani katika kufanikisha malengo yako ya nyuma? Mambo gani yalikukwaza? Utafanya nini kusonga mbele?
3. Ni maeneo gani katika maisha yako yanayohitaji mkazo au umakini zaidi?
Mfano: Je unahitaji kukazia katikauchumi wako, afya yako, kazi yako, familia yako au uhusiano wako na ndugu, jamaa au rafiki zako.. Utafanyaje ili kuweka mambo sawa?
4. Je ni zipi ndoto zako au matumaini yako? Je umeweka mikakati mizuri ya kupata utakacho?
5.Je ni maeneo gani ya kazi au shughuli zako unataka kubadilisha au kuboresha zaidi ili kuongeza tija na mafanikio yako ya baadae?
6. Je ni mafanikio ya kiasi gani unayofurahi kuyapata na kutoa msaada kwa wengine?
Itakuwa ni vyema kila baada ya miezi mitatu (3) upime maendeleo ya maisha yako. Weka jitihada na mafanikio yako katika darubini kulingana na mategemeo yako. Kisha endelea kuongeza bidii na kuwa na imani utafanikiwa, Unaweza pia ukawa na kitabu rasmi kwaajili ya kuweka kumbukumbu za maendeleo yako. Kila hatua ndogo unayopiga rekodi kwenye kitabu, hii itakusaidia kuona ni jinsi gani upo karibu au mbali na malengo yako. Kumbuka usisahau kujipongeza kwa kila mafanikio madogo au makubwa unayoyapata.

JINSI YA KUPIMA MAENDELEO YAKO KWA KUJIULIZA MASWALI HAYA.

Pima maendeleo yako kwa kujiuliza maswali haya.


Kwa mtu makini na hodari anayependa kujiendeleza iwe kiimani, kimahusiano, kiafya, kikazi au kitaaluma hujiwekea malengo na kumbukumbu ya mafanikio yakekila wakati anapopiga hatua.
Yafuatayo ni maswali kadhaa yatakayokusaidia kutafakari na kupima mafanikio au udhaifu wako ikiwa unadhumuni la kuwa mtu bora zaidi.
Jiulize maswali yafuatayo...
1. Umefanikisha nini katika miezi mitatu (3) iliyopita, na kwanini kitu hicho kilikuwa na maana kubwa kwako?
2. Je ulipata changamoto gani katika kufanikisha malengo yako ya nyuma? Mambo gani yalikukwaza? Utafanya nini kusonga mbele?
3. Ni maeneo gani katika maisha yako yanayohitaji mkazo au umakini zaidi?
Mfano: Je unahitaji kukazia katikauchumi wako, afya yako, kazi yako, familia yako au uhusiano wako na ndugu, jamaa au rafiki zako.. Utafanyaje ili kuweka mambo sawa?
4. Je ni zipi ndoto zako au matumaini yako? Je umeweka mikakati mizuri ya kupata utakacho?
5.Je ni maeneo gani ya kazi au shughuli zako unataka kubadilisha au kuboresha zaidi ili kuongeza tija na mafanikio yako ya baadae?
6. Je ni mafanikio ya kiasi gani unayofurahi kuyapata na kutoa msaada kwa wengine?
Itakuwa ni vyema kila baada ya miezi mitatu (3) upime maendeleo ya maisha yako. Weka jitihada na mafanikio yako katika darubini kulingana na mategemeo yako. Kisha endelea kuongeza bidii na kuwa na imani utafanikiwa, Unaweza pia ukawa na kitabu rasmi kwaajili ya kuweka kumbukumbu za maendeleo yako. Kila hatua ndogo unayopiga rekodi kwenye kitabu, hii itakusaidia kuona ni jinsi gani upo karibu au mbali na malengo yako. Kumbuka usisahau kujipongeza kwa kila mafanikio madogo au makubwa unayoyapata.

Tuesday, October 15, 2013

FAHAMU FAIDA ZA KULA NDIZI MBIVU.

Je ulikuwa ukijua faida za kula ndizi mbivu?
Ndizi ni matunda yanayopatikana kila mahali. Siku hizi kila penye kioski au grocery ya matunda ni rahisi kupata ndizi. Ndizi hizo huuzwa kwa bei ya kawaida tu kwako kuweza kununua. Ndizi ni tunda lenye rangi ya kijani liwapo bichi na rangi ya njano likiwa limeiva vizuri. Tumezoea kuona ndizi kwenye migomba shambani au vichane vya ndizi sokoni tunapokwenda kununua vitu mbalimbali kwaajili ya mlo. Swali ni, je tumeshawahi kujuiliza ni faida gani tunapata tunapokula ndizi hizo?
Labda huu ni wakati sahihi sasa tujue manufaa ya kula ndizi mbivu. Na hapa ni baadhi ya faida za kula tunda hili zuri na lenye lanya tamu.
1. Ndizi ni tunda lenye vitamin nyingi na madini kadhaa.
-Vitamin B6naChupatikana kwenye ndizi. Vitamin B6 ipo katika kiwango kikubwa kwenye ndizi ukilinganisha na Vitamin C ambayo ni kidogo. Madini yanayopatikana kwenye ndizi nimagnesium,manganesenapotassium. Madini ya magnesium na manganese yana compound inayojulikana kama‘’cytokinin’’ambayo huongeza idadi ya chembe chembe nyeupe za damu hivyo huboresha na kuongeza kinga ya mwili. Madini ya potassium nayo husaidia kudhibiti shinikizo kubwa la damu (high blood pressure) na kuimarisha utendaji kazi wa moyo. Vile vile madini ya potassium huzuia upotevu wa madini muhimu ya calcium mwilini ambayo hutumika katika utengenezaji wa mifupa. Kwa kifupi vitamins na madini yanayopatikana kwenye ndizi husaidia kupambana na seli za saratani.
2. Ndizi husaidia kupambana na vidonda vya tumbo.
-Sio tu kwamba ndizi hupambana na seli za saratani lakini pia hukinga tumbo kupata vidonda vya tumbo kwa uwezo wa compounds mbalimbaliilizonazo. Compounds hizi zinazopatikana kwenye ndizi hujenga tabaka nene kwenye kuta za tumbo ambazo hukinga tumbo kuathirika na tindikali ijulikanayo kama‘’hydrochloric acid’’. Pia ndizi zina enzyme inayojulikana kama‘’protease inhibitor’’ambayo huzuia bakteria wasababishao vidonda vya tumbo. Huh,…ni faida ilioje. Yani ukila ndizi tu unaweza usimwone daktari kwaajili ya tatizo la vidonda vya tumbo.
3. Ndizi huboresha ngozi.
-Kama ilivyo ngozi yako maganda ya ndizi nayo ni muhimu pia kwani yanaweza kupendezesha kabisa ngozi yako kama yakisagwa vizuri na matunda mengine kama parachichi. Virutubisho hivyo kwa pamoja hulainisha ngozi na kuifanya yenye muonekano mzuri wa kung’aa.
4. Ndizi huongeza nguvu mwilini.
-Ili uweze kufanya kazi zako kwa umahiri ni lazima mwili uwe na nguvu. Ndizi mbivu huwa na sukari ujulikanayo kama‘’glucose’’ambayo huongeza nguvu mwilini. Sukari hii inahitajika katika kiasi maalum mwilini.
5. Kambakamba za kwenye ndizihusaidia kuimarisha mfumo wa chakula.
-Ni kweli kabisa kambakamba za kwenye ndizi husaidia chakula kuteleza vizuri kwenye njia ya chakula. Kwa maana hiyo chakula kinaweza kupita kirahisi bila kipingamizi.
6.Hii labda ndio ulikuwa hujui kabisa‘’ndizi husaidia kupunguza stress na kukufanya uwe katika mood nzuri.’’
-Unaweza kujiuliza kivipi? Kama ulikuwa hujui ndizi zina kemikali mahsusi iitwayo‘’tryptophan’’ambayo iwapo mwilini hubadilishwa na kuwa‘’serotonin’’. Kemikali hii ya serotonin iwapo mwilini husaidia mtu ajisikie vizuri na kuwa katika mood nzuri na hatimaye kupunguza stress. (msongo wa mawazo)
Makala nyinginezo za kupitia:
*. Fahamu faida za matunda haya kwa ubora wa afya yako.
*. Magonjwa nyemelezi na dalili zake.
*. Fahamu ugonjwa wa kisukari. (diabetes)
Kama una chochote cha kuongeza kuhusiana na mada hapo juu, tafadhali usisite kutoa maoni yako!

FAHAMU FAIDA ZA KULA NDIZI MBIVU.

FAHAMU UGONJWA WA KISUKARI (DIABETES). Toleo la pili

Chakula


Chakula cha jioni (Chajio):Nusu kikombe cha pasta na kipande kimoja cha mkate.
Kitafunio:Biskuti sita.
Mboga.
Mboga ni bora kwa afya hasa kwa watu walio na ugonjwa wa kisukari (diabetis). Kula mboga kila siku, mboga zitakupatia vitamin na madini. Chagua mboga zenye rangi.Mfanokaroti, pilipili, biringanya, nyanya na mchicha.
Matunda.
Tunda ni asili ya afya kwa kila mtu, wakiwamo watu walio na shida ya kisukari (diabetis). Tunda hukupatia nguvu, vitamin na madini. Penda kula matunda kwa namna hii,
-Kula tofaa (apple) ama pera moja.
-Nusu kikombe cha juisi ya tofaa (apple) ama chungwa.
-Nusu kikombe cha juisi ya zabibu.
-Ndizi moja ndogo au nusu ya ndizi kubwa.
Kama utatengeneza juisi ya matunda usiongeze sukari.
Maziwa na vyakula vya mtindi.
Maziwa yenye idadi ndogo ya fats ni mazuri kwa afya kwa watu wote, wakiwamo watu wenye kisukari. Maziwa (fresh) na mtindi yatakupatia nguvu, protini, calcium, vitamin A, na vitamin nyingine na madini mbalimbali.
Kunywa maziwa yasiyo na fats au kiasi kidogo cha fats (1%) kila siku. Kunywa mtindi usio na
fats au wenye kiasi kidogo cha fats ili kuepuka kuongeza kiwango cha cholesterol kwenye damu.Usitumie mtindi wa kwenye makopo unaosema, “fruit on the bottom” kwasababu kwa jinsi ulivyotengenezwa una sukari nyingi.
Nyama, kuku, samaki na mayai.
Kundi hili la chakula ni la nyama ya (ng’ombe, nguruwe, kondoo), kuku, bata mzinga, mayai, samaki nakadhalika. Vyakula vyote hivi ni vyenye protini kwa wingi na husaidia kujenga misuli na mifupa pia vinaupa mwili vitamin na madini.
Katika mlo wako unaweza kuweka hivi,
-Samaki wawili au watatu.
-Nyama ya kuku.
-Yai moja.
-Vijiko viwili vya siagi ya njugu au karanga.
Mapendekezo ya Kusaidia:
-Kama utanunua nyama ya ng’ombe au mbuzi yenye mafuta basi ondoa sehemu ya mafuta.
-Kula kuku au bata mzinga bila ngozi.
-Pika vyakula vyenye protini kwa mafuta kidogo wa wakati wa kukaanga, kuoka,
kutokosa, kuchoma, kupika kwa mvuke ama kuchemsha.
Tamutamu (sweet foods).
Tamutamu ni vyakula vya sukari vyenye kalori bila vitamin au madini. Vyakula vingine vinasukari nyingi kama keki, pai, na biskuti.Kwa kula vyakula vingi vyenye sukari na mafuta mengi kutakuletea shida katika harakati za kutibu ugonjwa wa kisukari.
Kama utapendelea kula vyakula vya namna hii basi zingatia kutoweka sukari nyingi ili kuepusha matatizo. Mfano unaweza weka,...
-Kijiko kimoja cha mafuta.
-Kijiko kimoja cha mafuta ya saladi.
-Vijiko viwili vya mayonnaise.
Au kama unataka kupata breakfast ule biskuti moja, andazi moja.
Nakutakia afya njema katika maisha yako.
Kama una chochote cha kuongeza kuhusiana na mada hapo juu, tafadhali usisite kutoa maoni yako!

FAHAMU UGONJWA WA KISUKARI (DIABETES). Toleo la pili

Chakula


Chakula cha jioni (Chajio):Nusu kikombe cha pasta na kipande kimoja cha mkate.
Kitafunio:Biskuti sita.
Mboga.
Mboga ni bora kwa afya hasa kwa watu walio na ugonjwa wa kisukari (diabetis). Kula mboga kila siku, mboga zitakupatia vitamin na madini. Chagua mboga zenye rangi.Mfanokaroti, pilipili, biringanya, nyanya na mchicha.
Matunda.
Tunda ni asili ya afya kwa kila mtu, wakiwamo watu walio na shida ya kisukari (diabetis). Tunda hukupatia nguvu, vitamin na madini. Penda kula matunda kwa namna hii,
-Kula tofaa (apple) ama pera moja.
-Nusu kikombe cha juisi ya tofaa (apple) ama chungwa.
-Nusu kikombe cha juisi ya zabibu.
-Ndizi moja ndogo au nusu ya ndizi kubwa.
Kama utatengeneza juisi ya matunda usiongeze sukari.
Maziwa na vyakula vya mtindi.
Maziwa yenye idadi ndogo ya fats ni mazuri kwa afya kwa watu wote, wakiwamo watu wenye kisukari. Maziwa (fresh) na mtindi yatakupatia nguvu, protini, calcium, vitamin A, na vitamin nyingine na madini mbalimbali.
Kunywa maziwa yasiyo na fats au kiasi kidogo cha fats (1%) kila siku. Kunywa mtindi usio na
fats au wenye kiasi kidogo cha fats ili kuepuka kuongeza kiwango cha cholesterol kwenye damu.Usitumie mtindi wa kwenye makopo unaosema, “fruit on the bottom” kwasababu kwa jinsi ulivyotengenezwa una sukari nyingi.
Nyama, kuku, samaki na mayai.
Kundi hili la chakula ni la nyama ya (ng’ombe, nguruwe, kondoo), kuku, bata mzinga, mayai, samaki nakadhalika. Vyakula vyote hivi ni vyenye protini kwa wingi na husaidia kujenga misuli na mifupa pia vinaupa mwili vitamin na madini.
Katika mlo wako unaweza kuweka hivi,
-Samaki wawili au watatu.
-Nyama ya kuku.
-Yai moja.
-Vijiko viwili vya siagi ya njugu au karanga.
Mapendekezo ya Kusaidia:
-Kama utanunua nyama ya ng’ombe au mbuzi yenye mafuta basi ondoa sehemu ya mafuta.
-Kula kuku au bata mzinga bila ngozi.
-Pika vyakula vyenye protini kwa mafuta kidogo wa wakati wa kukaanga, kuoka,
kutokosa, kuchoma, kupika kwa mvuke ama kuchemsha.
Tamutamu (sweet foods).
Tamutamu ni vyakula vya sukari vyenye kalori bila vitamin au madini. Vyakula vingine vinasukari nyingi kama keki, pai, na biskuti.Kwa kula vyakula vingi vyenye sukari na mafuta mengi kutakuletea shida katika harakati za kutibu ugonjwa wa kisukari.
Kama utapendelea kula vyakula vya namna hii basi zingatia kutoweka sukari nyingi ili kuepusha matatizo. Mfano unaweza weka,...
-Kijiko kimoja cha mafuta.
-Kijiko kimoja cha mafuta ya saladi.
-Vijiko viwili vya mayonnaise.
Au kama unataka kupata breakfast ule biskuti moja, andazi moja.
Nakutakia afya njema katika maisha yako.
Kama una chochote cha kuongeza kuhusiana na mada hapo juu, tafadhali usisite kutoa maoni yako!

FAHAMU UGONJWA WA KISUKARI (DIABETES). Toleo la pili

FAHAMU UGONJWA WA KISUKARI (DIABETES)

Fahamu ugonjwa wa kisukari (diabetes).

Diabetis(Ugonjwa wa kisukari).

Diabetis ni nini?Diabetis ni ugonjwa unaosababisha mwili kutokuwa na matumizi ya kutosha ya insulin. Insulin ni homoni yenye uwezo wa kubadilisha umbo la sukari, wanga, na vyakula vingine kuwa nguvu au kani ya uhai wa kila siku.
Matibabu ya ugonjwa wa kisukari (diabetis) yakoje?
Matibabu ya diabetis yapo katika sehemu tatu:
1. Kula vizuri kwa afya (good diet).
2. Kufanya mazoezi ya mwili.
3. Kwa kutumia dawa (kama utalazimika).
Utawezaje kumudu ugonjwa wa kisukari (diabetis)?Utaweza kumudu ugonjwa wa kisukari au kiwango cha sukari kwenye damu (blood glucose) kwa kula chakula chenye afya (good diet), kufanya mazoezi ya mwili, na kwa kuwa na uzito wa mwili wenye afya (healthy weight).
Uzito wenye afya (healthy weight) utakusaidia pia kumudu kiwango cha mafuta (fats) kwenye damu (cholesterol) na kupunguza msongo wa damu (blood pressure).
Watu wengi wenye diabetis wanahitaji pia kutumia dawa kusaidia kutawala sukari (blood glucose).
Kula vizuri kwa afya.
Kwa kutumia mwongozo wa ulaji (food guide pyramid) kutakusaidia kula vyakula mbalimbali
kwa afya. Kula vyakula mbalimbali au chakula chenye mseto wa aina tofauti tofauti ya virutubisho (balanced diet). Unapokula balanced diet kila siku, utapata vitamin na madini mengi yanayohitajika kwa ubora wa afya yako.
Huu ni mfano wa kula chakula chenye virutubisho mbalimbali (balanced diet).
Siku ya kwanza Siku ya Pili
Mbegu (grains): chapati mchele wa rangi (brown rice)
Tunda: tofaa (apple) embe
Mboga: brokoli nyanya
Maziwa: maziwa (fresh) mtindi
Protini: kuku maharagwe
Kula vyakula vyenye virutubisho vyote.
-Nunua mikate ya chembe (grain breads) na mikate ya nafaka (cereal breads) na ngano,
-Punguza kula vyakula vya kukaanga na vyenye mafuta kama maandazi na biskuti.
-Matunda ni bora zaidi, ukinunua matunda ya kwenye kopo, tazama maneno “canned in their own juice”. (“yametayarishwa na juisi yake”)
-Nunua matunda madogo madogo, na unywe juisi kiasi kidogo kidogo.
-Kula mboga ambazo hazijapikwa kwa maafuta mengi.
-Tumia haradali (mustard) badala ya siagi nyingi kwenye mkate.
-Tumia mafuta ya mboga badala ya mafuta ya kawaida, siagi au samli.
-Namna bora ya kupika ni kuvumbika, kuchemsha, kutokosa, kuchoma, kwa
mvuke na kuoka. Usitumie mafuta mengi wakati wa kupika.
-Tumia nyama isiyo na mafuta kama kuku, bata mzinga. Unaponunua nyama ya nguruwe,
nyama ya ng’ombe na kiweo, kata unono ( extra fat ) wake.
-Tumia maziwa yasiyo na mafuta (fats), na vyakula vinavyotokana na maziwa bilafats.
Punje (grains), maharagwe na mboga yenye kanji (starch).
Kanji (starch) au kabohaidreti/wanga ni nini?
Kanji (starches) ni vyakula kama mikate, punje (grains), nafaka, pasta, maharagwe au mboga yenye kanji (starch). Kula kanji ama kabohaidreti chache kila unapokula. Watu wanaweza kukuambia usile kanji (starch) ama kabohaireti nyingi lakini huo si ukweli. Kula kanji (starch) ama kabohaidreti kuna faida za kiafya ikiwa ni pamoja na kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari (diabetis).
Unahitaji kanji (starches) ama kabohaireti/wanga ngapi kila siku?Resheni (servings) 6 hadi 11 kila siku.
Idadi ya resheni unayotakiwa kula kwa siku inategemea na kalori (calories), unazohitaji mpango wa tiba na hali yako ya kisukari (diabetis).
Kanji (starches) na kabohaidreti/wanga hufanya nini katika mwili wako?Kanji (starch) huupa mwili wako nguvu, vitamin B, madini na vitembwe (fibre). Punje (grains) ni zenye afya zaidi kwa vile zina vitamin, madini, na vitembwe (fibre). Vitembwe (fibre) hukusaidia kupata choo. Pia hukusuaidia katika uwezo wa kumudu au kuongeza idadi ya sukari kwenye damu (blood glucose).
Mlo mmoja wa starch ama wanga upo hivi,
-Kipande kimoja cha mkate
-Kiazi kidogo, mhogo au ndizi moja
-Nusu (1/2) kikombe cha nafaka ya kupika kama uji au ngano.
-Sehemu ya ¾ ya kikombe cha nafaka ngumu kama corn flakes.
-Sehemuya kikombe cha wali.
Unaweza kula mlo wa namna hii.Mfano,
Chakula cha asubuhi:Sehemu ¾ ya kikombe cha nafaka ngumu na kipande kimoja cha mkate.
Chakula cha mchana:Sehemu 1/3 ya kikombe cha mchele na ndizi za
kupika.

FAHAMU UGONJWA WA KISUKARI (DIABETES)

Fahamu ugonjwa wa kisukari (diabetes).

Diabetis(Ugonjwa wa kisukari).

Diabetis ni nini?Diabetis ni ugonjwa unaosababisha mwili kutokuwa na matumizi ya kutosha ya insulin. Insulin ni homoni yenye uwezo wa kubadilisha umbo la sukari, wanga, na vyakula vingine kuwa nguvu au kani ya uhai wa kila siku.
Matibabu ya ugonjwa wa kisukari (diabetis) yakoje?
Matibabu ya diabetis yapo katika sehemu tatu:
1. Kula vizuri kwa afya (good diet).
2. Kufanya mazoezi ya mwili.
3. Kwa kutumia dawa (kama utalazimika).
Utawezaje kumudu ugonjwa wa kisukari (diabetis)?Utaweza kumudu ugonjwa wa kisukari au kiwango cha sukari kwenye damu (blood glucose) kwa kula chakula chenye afya (good diet), kufanya mazoezi ya mwili, na kwa kuwa na uzito wa mwili wenye afya (healthy weight).
Uzito wenye afya (healthy weight) utakusaidia pia kumudu kiwango cha mafuta (fats) kwenye damu (cholesterol) na kupunguza msongo wa damu (blood pressure).
Watu wengi wenye diabetis wanahitaji pia kutumia dawa kusaidia kutawala sukari (blood glucose).
Kula vizuri kwa afya.
Kwa kutumia mwongozo wa ulaji (food guide pyramid) kutakusaidia kula vyakula mbalimbali
kwa afya. Kula vyakula mbalimbali au chakula chenye mseto wa aina tofauti tofauti ya virutubisho (balanced diet). Unapokula balanced diet kila siku, utapata vitamin na madini mengi yanayohitajika kwa ubora wa afya yako.
Huu ni mfano wa kula chakula chenye virutubisho mbalimbali (balanced diet).
Siku ya kwanza Siku ya Pili
Mbegu (grains): chapati mchele wa rangi (brown rice)
Tunda: tofaa (apple) embe
Mboga: brokoli nyanya
Maziwa: maziwa (fresh) mtindi
Protini: kuku maharagwe
Kula vyakula vyenye virutubisho vyote.
-Nunua mikate ya chembe (grain breads) na mikate ya nafaka (cereal breads) na ngano,
-Punguza kula vyakula vya kukaanga na vyenye mafuta kama maandazi na biskuti.
-Matunda ni bora zaidi, ukinunua matunda ya kwenye kopo, tazama maneno “canned in their own juice”. (“yametayarishwa na juisi yake”)
-Nunua matunda madogo madogo, na unywe juisi kiasi kidogo kidogo.
-Kula mboga ambazo hazijapikwa kwa maafuta mengi.
-Tumia haradali (mustard) badala ya siagi nyingi kwenye mkate.
-Tumia mafuta ya mboga badala ya mafuta ya kawaida, siagi au samli.
-Namna bora ya kupika ni kuvumbika, kuchemsha, kutokosa, kuchoma, kwa
mvuke na kuoka. Usitumie mafuta mengi wakati wa kupika.
-Tumia nyama isiyo na mafuta kama kuku, bata mzinga. Unaponunua nyama ya nguruwe,
nyama ya ng’ombe na kiweo, kata unono ( extra fat ) wake.
-Tumia maziwa yasiyo na mafuta (fats), na vyakula vinavyotokana na maziwa bilafats.
Punje (grains), maharagwe na mboga yenye kanji (starch).
Kanji (starch) au kabohaidreti/wanga ni nini?
Kanji (starches) ni vyakula kama mikate, punje (grains), nafaka, pasta, maharagwe au mboga yenye kanji (starch). Kula kanji ama kabohaidreti chache kila unapokula. Watu wanaweza kukuambia usile kanji (starch) ama kabohaireti nyingi lakini huo si ukweli. Kula kanji (starch) ama kabohaidreti kuna faida za kiafya ikiwa ni pamoja na kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari (diabetis).
Unahitaji kanji (starches) ama kabohaireti/wanga ngapi kila siku?Resheni (servings) 6 hadi 11 kila siku.
Idadi ya resheni unayotakiwa kula kwa siku inategemea na kalori (calories), unazohitaji mpango wa tiba na hali yako ya kisukari (diabetis).
Kanji (starches) na kabohaidreti/wanga hufanya nini katika mwili wako?Kanji (starch) huupa mwili wako nguvu, vitamin B, madini na vitembwe (fibre). Punje (grains) ni zenye afya zaidi kwa vile zina vitamin, madini, na vitembwe (fibre). Vitembwe (fibre) hukusaidia kupata choo. Pia hukusuaidia katika uwezo wa kumudu au kuongeza idadi ya sukari kwenye damu (blood glucose).
Mlo mmoja wa starch ama wanga upo hivi,
-Kipande kimoja cha mkate
-Kiazi kidogo, mhogo au ndizi moja
-Nusu (1/2) kikombe cha nafaka ya kupika kama uji au ngano.
-Sehemu ya ¾ ya kikombe cha nafaka ngumu kama corn flakes.
-Sehemuya kikombe cha wali.
Unaweza kula mlo wa namna hii.Mfano,
Chakula cha asubuhi:Sehemu ¾ ya kikombe cha nafaka ngumu na kipande kimoja cha mkate.
Chakula cha mchana:Sehemu 1/3 ya kikombe cha mchele na ndizi za
kupika.

MAGONJWA NYEMELEZI NA DALILI ZAKE.(toleo la pili)

Mkanda wa jeshi.
Husababishwa na kirusi kiitwachoVaricella Zoster (VSV).Mara nyingi hutokana na kuamshwa kwa ugonjwa ambao ulikuwepo mwilini hapo awali (reactivation of an earlier infection).Mbali ya kuathiri ‘uwanda’ (dermatome) moja au zaidi wa mishipa ya fahamu (neva), pia huweza kudhuru jicho (herpes zoster opthalmicus) na sikio (herpes zoster oticus).
Dalili zake ni maumivu makali katika ‘uwanda’ ulioathirika, homa, vipele, maumivu ya kichwa, uchovu na maumivu ya macho kutokana na mwanga (photophobia).
Maumivu ya Retina
Kwa lugha ya kitaalamu huitwa CMV Retinitis na husababishwa na kirusi kiitwacho Cytomegalovirus (CMV). Kirusi hiki, mbali ya kuathiri jicho na haswa retina, pia huathiri viungo vingine kama mapafu na kusababisha nimonia, utumbo mpana na mfumo wa fahamu ambako husababisha maumivu.
Dalili zake ni pamoja na kutoona vizuri, macho kuuma, kutokwa na machozi kwa wingi.Kutopata matibabu mapema huweza kusababisha upofu.Pia Huweza kuathiri viungo vingine na kusababisha homa, nimonia, kichefuchefu, kuharisha na kupungua uzito.
Magonjwa yatokanayo na Fangasi.
Fangasi pia huweza kujitokeza iwapo kinga ya mwili itashuka.
Kandidiasisi.
Ugonjwa huu uliozoeleka pia hujulikana kwa kitaalamu kama Candidiasis. Kandidiasisi husababishwa na fangasi aitwayeCandida albicansambaye huathiri kinywa, mfumo wa chakula,uke na mfumo wa hewa.Kandidiasisi katika uke huweza tokea kwa mwanamke mwenye afya asiye na VVU.
Dalili za Kandidiasisi katika kinywa ni pamoja na kubadilika kwa ladha, maumivu kwenye ulimi, utando mweupe kwenye ulimi na kingo za juu za kinywa (buccal mucosa), kushindwa kumeza ,maumivu wakati wa kumeza chakula ikiwa fangasi imesambaa sana. Pia mwasho na maumivu ukeni pamoja na kutokwa na majimaji meupe ukeni.
Homa ya Uti wa mgongo.
Homa ya uti wa mgongo au Meningitis kwa kitaalamu husababishwa na fangasi aitwayeCryptococcal neoformans. Uti wa mgongo utokanao na aina hii ya fangasi huweza kusababisha kifo usipotibiwa. Aina hii ya fangasi ambayo huathiri zaidi ubongo na uti wa mgongo, hutokana na kuvuta hewa yenye vumbi litokanalo na ndege lenye vimelea vya ugonjwa.
Baadhi ya dalili zake ni homa, kutoona vizuri, macho kuuma kutokana na mwanga, kuchanganyikiwa akili, maumivu ya kichwa ka kukakamaa na kuuma kwa shingo.
Histoplasmosisi.
Aina hi ya fangasi hutokana na vimelea vyaHistoplasma capsulatum. Fangasi huyu huathiri mapafu pamoja na viungo vingine. Dalili zake ni homa,uchovu,kupungua uzito na kupumua kwa shida. Pia kukohoa na kuvimba kwa tezi kwaweza kutokea.
Nimonia.
Kama bakteria na fangasi pia huweza kusababisha nimonia ijulikanayo kwa kitaalamu kama Pneoumocystis Pneumonia (PCP). Vimelea vya Pneumocystis jiroveci (awali vilijulikana kama Pneuomocystis carinii) huathiri mfumo wa hewa. Fangasi huyu pia huweza kuathiri viungo vingine kama ini, wengu (spleen) na figo katika baadhi ya wagonjwa.
Dalili zake ni kikohozi kikavu,kifua kubana,kupumua kwa shida,homa,kuishiwa pumzi na kutokwa jasho nyakati za usiku.
Magonjwa yatokanayo na Protozoa.
Toksoplasmosisi ya Ubongo.
Cerebral toxoplasmosis, kama ujulikanavyo kitaalamu, hutokana na kuamshwa kwa ugonjwa wa awali kutokana na vimelea vyaToxoplasma gondii(kimelea kiwezacho kuishi ndani ya seli kinachoathiri ndege, wanyama na binadamu). Kimelea hiki kiathiricho zaidi mfumo wa fahamu hupatikana kwenye nyama isiyopikwa vizuri na kinyesi cha paka. Huathiri zaidi ubongo na kusababisha maumivu ya kichwa, kuchanganyikiwa, udhaifu wa viungo, homa, kupoteza fahamu, kupooza na kifafa.
Kriptosporidiosisi.
Huu ni ugonjwa utokanao na vimelea vyaCryptosporidium. Huathiri zaidi mfumo wa chakula na hutokana na kutumia kwa maji au chakula vilivyoathirika na vimelea vya ugonjwa huu. Dalili zake ni kuharisha sana kiasi cha kusababisha kupungukiwa na maji mwilini (dehydration), maumivu wakati wa haja kubwa, kichefuchefu na kutapika. Wagonjwa wa aina hii huwa na joto la mwili la kawaida.
MATIBABU NA USHAURI.
Aina ya matibabu hutegemea na aina ya ugonjwa na mtu, pia kutokana na kuwepo kwa Ukimwi/VVU hutegemea kiwango cha seli za CD4 mwilini. Iwapo una dalili kati ya zilizotajwa hapo juu ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.
Kuwepo kwa dalili zilizotajwa hapo juu hakumanishi kuwa mgonjwa ana VVU na si kila mwenye VVU huwa na dalili hizo. Pia kujitokeza kwa dalili kunaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu. Hata hivyo ni vyema kupima afya yako kila mara haswa VVU ili kujua chanzo cha kupungua kwa kinga ya mwili ambayo huweza kupelekea kupata magonjwa nyemelezi.
NAKUTAKIA AFYA NJEMA NA MAFANIKIO TELE KATIKA MAISHA YAKO.
Kama una chochote cha kuongeza kuhusiana na mada hapo juu, tafadhali usisite kutoa maoni yako!

MAGONJWA NYEMELEZI NA DALILI ZAKE.

Magonjwa nyemelezi na dalili zake.


Magonjwa nyemelezi ni yale ambayo hushambulia mwili wa binadamu pale uwezo wa kinga ya mwili kupigana na vimelea vya magonjwa inaposhuka. Ni magonjwa ambayo katika hali ya kawaida hayategemewi kujitokeza kwa mtu mwenye kinga kamili ya mwili.
Kwa kawaida mwili wa binadamu yoyote umeumbwa na kinga ya mwili ya asili ambayo lengo lake kuu ni kuulinda mwili dhidi ya vimelea vya magonjwa. Inapotokea kimelea (vimelea) kuingia katika mwili wa binadamu kwa njia yoyote (kunywa au kula vimelea, kugusana na majimaji au ngozi ya mtu mwenye vimelea au kupitia damu yenye vimelea n.k), mwili hutengeneza kingamwili (antibodies) ambazo hupigana na vimelea hivyo ili kuuweka mwili katika afya njema kama hapo awali.
Kushuka kwa kinga ya mwili hupelekea mwili kushindwa kupigana na vimelea vya magonjwa hivyo kusababisha kushambuliwa na magonjwa.Ifahamike kwamba baadhi ya vijidudu (microorganisms) pia hupatikana katika mwili wa binadamu bila madhara yoyote (normal flora) kama vile kwenye ngozi, mfumo wa chakula, ukeni, uumeni n.k. Mathalan vijidudu hivi huweza kuwa chanzo cha magonjwa iwapo kinga ya mwili itashuka.
`
Vitu gani hupelekea kushuka kwa kinga ya mwili?
Sababu mojawapo kubwa ya kushuka kwa kinga ya mwili haswa katika nchi zilizopo chini ya jangwa la Sahara ni Ukimwi/VVU. Pia ieleweke kwamba si kila mtu mwenye upungufu wa kinga mwilini ana VVU.
Kuna sababu nyingine nyingi ambazo husababisha kwa njia moja au nyingine kushuka kwa kinga ya mwili.Zifuatazo ni baadhi tu ya sababu hizo;...
Utapiamlo, kuugua mara kwa mara, sababu za kijenetiki (kurithi), madhara kwenye ngozi, msongo wa mawazo, ujauzito, madawa ya kutibu saratani, matumizi ya muda mrefu ya antibayotiki (antibiotics),steroidi (steroids) na madawa ya kushusha kinga mwilini (immunosuppressant drugs) ambayo hutumika wakati wa kupandikiza viungo mwilini kama figo n.k
Magonjwa nyemelezi husababishwa na vijidudu mbalimbali kamabacteria, virusi, fangasi na bakteria.
Magonjwa yatokanayo na Bakteria.
Baadhi ya magonjwa yasababishwayo na bakteria ni kama yafuatayo;
Kifua Kikuu (TB)
Ugonjwa huu husababishwa na kimelea kiitwachomycobacterium tuberculosisambacho ni moja katika kundi la Mycobacterium Avium Complex (MAC). Kushuka kwa kinga ya mwili hupelekea kulipuka kwa vimelea vya kifua kikuu ambavyo hupatikana, pamoja na viungo vingine, zaidi kwenye mapafu.
Dalili za kifua kikuu ni pamoja na kikohozi, homa (haswa nyakati za usiku) kwa zaidi ya wiki mbili, kutokwa jasho usiku (mara nyingi jasho huwa jingi mpaka kulowesha shuka), kupungua uzito (zaidi ya kilo moja na nusu ndani ya mwezi), kichomi na kukohoa damu.
Ugonjwa huu pia huweza kupelekea kupata homa ya uti wa mgongo (meningitis) ambayo huambata na dalili kama kuumwa kichwa, kichefu chefu na kutapika ikifutiwa na kuongezeka kwa joto la mwili na maumivu na kukaza kwa shingo.
Nimonia (Pneumonia).
Huu ni ugonjwa ambao kwa kiasi kikubwa huathiri mfumo wa hewa na haswa mapafu. Baadhi ya vimelea viletavyo nimonia ni kamapneumococcus ,haemopilus influenza, mycoplasma(haswa kwa watoto)piaklebsiella, staphylococcus aureus, pseudomonas aeuroginosa(kwa wagonjwa waliolazwa mahospitalini) na wengineo.
Ugonjwa huu huanza ghafla na dalili zake ni kama homa kali, kikohozi, maumivu wakati wa kupumua, baridi na kutetemeka.
Ugonjwa wa Ngozi.
Huu husababishwa na vimelea vyaStaphylococcus aureus.Vimelea hivi huishi katika mwili wa binadamu (kwenye ngozi ya kichwa na kinena (groins) na kwapani) bila madhara. Pia hupatikana kooni na katika utumbo mpana na mkojo.
Vimelea vya Staphylococcus husambaa kwenda sehemu nyingine ya mwili kutoka kwenye usaha, mgusano na ngozi ya mwenye maradhi, kutumia taulo, matandiko,vifaa vya mtu aliyeathirika n.k
Dalili zake ni pamoja na chunusi, majipu, kubabuka kwa ngozi na magamba magamba katika ngozi.
Magonjwa ya virusi.
Magonjwa yasababishwayo na virusi ni kama;
Ugonjwa wa Malengelenge.
Husababishwa na virusi vyaHerpes Simplex. Hivi vimegawanyika katika Herpes Simplex Virus-1 (HSV-1) na Herpes Simplex-2 (HSV-2).Virusi vya HSV-1 vyaweza ambukizwa kupitia ngozi laini (mucous membranes) za mwili na kubusiana. Huweza kusababisha mwasho kwenye mdomo, ulimi, fizi za meno au kingo za juu za kinywa (buccal mucosa). Kwa upande wa virusi vya HSV-2 hivi huweza kusababisha michubuko na maumivu kwenye uume, uke na njia ya haja kubwa.
Katika kiwango cha juu cha ugonjwa viungo vingine vya mwili kama macho, njia ya chakula, mfumo wa fahamu na na njia za mfumo wa hewa huathirika.
Dalili balimbali za ugonjwa huu ni malengelenge (blisters), mwasho na muunguzo. Kushindwa kumeza au kupata maumivu wakati wa kumeza (haswa chakula), tezi kuvimba na maumivu wakati wa haja kubwa au ndogo.

NAMNA YA KUPUNGUZA MSONGO WA MAWAZO.

Namna ya kupunguza msongo wa mawazo.


-Je una msongo wa mawazo ambao unashindwa kuuepuka? Katika hali ya kawaida ukiushika kwa kuubana mkono wako kwa sekunde kadhaa na kuuachilia, utagundua ni jinsi gani kuubana mkono wako kunavyochosha.
Kushikilia kitu unatumia nguvu nyingi, haijalishi ni nini hasa unachoshikilia kichwani kwako kama ni misukosuko ya mali, kazi, mahusiano yako na watu wako wa karibu katika maisha na mengineyo. Kushikilia au kubeba mzigo huu wa msongo wa mawazo humaliza nguvu nyingi kufikiria ufumbuzi wa matatizo uliyonayo.
‘’Kwanini tusitue mzigo huu wa msongo wa mawazo?’’
Kuna sababu nyingi za mtu kutoepukana na msongo wa mawazo, zikiwemo za kihisia (challenging emotions) na mazingira yanayomzunguka (watu, mali nk).
Mfano;-Unaweza kuogopa kuvunja uhusiano wenu wa kimapenzi na mwenza wako kwasababu unaogopa kuwa mpweke utakapokuacha.
--Unaweza kuogopa kuacha au kufukuzwa kazi kwasababu una wasiwasi wa kukosa kazi mahali pengine hapo baadae au kupata matatizo ya kifedha.
-Swala la msingi hapa ni kujua namna ya kumudu hisia (emotional intelligence) na mawazo yako katika hali ngumu uliyonayo. Huwezi pata jawabu sahihi la matatizo yako mpaka uache kufikiria sana kwanini au imekuaje umepata matatizo yanakusibu na uhamishe mawazo yako katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo uliyonayo. Ninachosisitiza hapa, tumia muda na nguvu nyingi kufikiria suluhu au ufumbuzi wa matatizo yako kuliko matatizo uliyonayo.
Utakapohamisha mawazo yako kwenye kupata ufumbuzi, ni rahisi kufunguka kihisia na kiakili na kupata afadhali katika kupunguza msongo wa mawazo.
-Katika mifano ya matatizo niliyotoa hapo awali ukiwemo wa kuogopa kuachwa na mpenzi wako utaweza kutatua na kupunguza msongo wa mawazo kwa kusema,..’’Naondoa wasiwasi wangu wa kuwa mpweke kwa sasa.’’NenoKWA SASAhusaidia kupunguza msongo wa mawazo kwa wakati huo kwa kukukumbusha kuwa mambo yote hubadilika. Hali ya ukame ya sasa haimanishi itadumu mpaka masika.
Kubadilika ni swala la kibinadamu, mtu huweza kubadilika kila mara kulingana na msukumo wa ndani yake (hisia na akili zake) au shinikizo la kimazingira yanayomzunguka. Kwa kawaida mtu mwenye kushikilia sana matatizo yake sana kiakili hufanya mambo kuwa magumu zaidi kuliko yule aliyeamua kutua mzigo wa msongo wa mawazo.
Ushauri wa namna ya kupunguza msongo wa mawazo.
-Kama tatizo lako ni kubwa, jaribu kutatua shida ndogondogo kwanza hatimaye kumalizia na shidailiyokubwa.
-Kubali kutua mzigo wa msongo wa mawazo kwa kuacha kubeba na kushikilia kichwani mambo ambayo yapo nje ya uwezo wako. Utakapofanya hivyo ni kama kitendo cha kuhema, unatoa hewa chafu nje na kuvuta hewa safi ya uzima ndani. Kwa kufanya hivyo unapumzisha akili.
-Kama tatizo lako ni dogo tu labda mtu amekuudhi au umeshindwa kabisa kumudu hisia zako na mawazo yako ni heri kwenda mahali penye watu wengi penye starehe ya aina fulani kama labda ni beach, cinema au mahali pa kukufanya ujiliwaze na kupunguza mawazo yako. Kwenda mahali penye watu wengi ni muhimu pia kwasababu unapokuwa katika sehemu yenye watu wengi ni rahisi kusaidiwa na watu wanaokuzunguka iwapo utataka kufanya jambo la ajabu kwasababu ya mawazo au hasira ulizonazo.
-Ikiwa hupati majibu kwa yale mambo yanayokufanya uwaze sana, tafuta ndugu, jamaa au rafiki yako wa karibu sana unayemuamini na umueleze matatizo yanayokusibu huenda ukapata ushauri au njia mbadala ya kutatua matatizo yako.
-Pima uzito wa mambo yanayokupa mawazo tele, kama jambo hilo sio la msingi sana katika maisha yako unaweza kuupuza na usilipe nafasi katika akili yako. Mawazo mengi yasiyo ya kukujenga kimaisha au mawazo yasiyo na tija ni vyema ukayapuuza ili kuondekana na msongo wa mawazo usio wa lazima. Akili yako ina mambo mengi ya kufikiri, ijaze na mambo mazuri yatakayokusaidia sasa na hapo baadae. Usiijaze na sumu kama hasira, mawazo potofu na mambo mengine yatakayoweza kukubomoa.
Kama una chochote cha kuongeza kuhusiana na mada hapo juu, tafadhali usisite kutoa maoni yako!

20 PLACES TO EDUCATE YOURSELF ONLINE FOR FREE.

20 Places to Educate Yourself Online for Free.

10. iTunes UMany of these same online courses can be accessed away from your computer with the help of iTunes U, a free app that can be downloaded to you iPad, iPhone or iPod Touch. It says that it includes 500,000 different courses, with material ranging from elementary school to college-level.
There’s also educational material here from respected institutions like the New York Public Library and MoMA. You can also add notes to the videos, share with friends and keep your course materials in iBooks so you have everything you need to learn wherever you are.
11. TEDThe TED talksare a legendary source of information on all sorts of topics, and any discussion of how to educate yourself for free online needs to include them. There are now thousands of videos on all sorts of topics available on the site.
If you’re a fan of whimsy you can also get the site to suggest a fascinating, beautiful or informative video for you, among other tags. This may not be formal education but it certainly can be life-changing.
12. 99ULove videos by experts on all sorts of topics? After you visit TED, check out 99U, which is another great source of educational videos on all sorts of topics. It has a strong focus on the subject of creativity, business development and innovation, so it’s sure to be of interest if you’re an entrepreneur or in a creative line of work.
13. IgniteIf you want to learn something new and you’re really pressed for time, check out Ignite videos. The purpose of this series of speaking events is to have each person share something innovative or inspiring in just five minutes. Sounds silly, but you can get a big dose of greatness in a short amount of time.
14. WikiversityIf you prefer your learning to be text-based, check out Wikiversity. As you might imagine, this site is part of the Wikimedia Foundation and includes detailed pages on a variety of subjects. It includes information of value to learners from preschool to college and beyond, and like other wiki projects is open-source and collaborative.
This is a good site or browsing, and the “random” button is a lot of fun.
15. Project GutenbergAccess more than 4,200 free ebooks at Project Gutenberg, an excellent source for public domain books from throughout history as well as contemporary free ebooks. You’ll find literature, historic documents, nonfiction books on all sorts of subjects and much more, all free and downloadable to your computer or ereader.
16. BartlebyA similar resource is Bartleby, which boasts a large collection of reference works, poetry, fiction and nonfiction. There are some really great resources here such as The Harvard Classics Shelf of Fiction, Oxford Shakespeare, Bullfinch’s Mythology, Bartlett’s Quotations and much more.
This is a great site to look at if you’re looking for quotes about a specific subject or just want to delve into the classics you probably should have read in school.
17. The Free LibraryBoasting a collection of more than 21 million free articles and books, The Free Libraryis the place to go for access to newspapers, magazines, journal articles (from 1984 to the present) and classic books. It’s a great place to start if you’re doing research for an academic paper or just want to find out more about a particular topic.
You can search by keyword or browse by source, topic or author, or just look at random articles and see what develops.
18. UdacityVideo courses in math, computer science, business, physics and psychology are available for free at Udacity. This clean site is easy to navigate and has the added bonus of a little icon next to the videos that shows you how advanced a course is so you know to start with an easier course if you’re new to a subject.
19. YouTubeIt seems that just about anything you could ever want to learn is available these days on YouTubefor instant, bite-sized, free consumption. Browse channels to find general topics that interest you, or search for the specific thing you want to learn and you’ll be on your way in no time.
There are more than 6,000 channels in the science and education section, more than 600 in cooking and nearly 2,000 in DIY, so whatever you want to educate yourself about you’re sure to find something good here.
20. Google, etc.The search engines are a great place to start if you have something specific you are looking for. Googlein particular provides a great overview of subjects right in your browser. Search for a person and you’ll get a mini bio without clicking on any other pages, and you’ll have lots of places to go for more information. This is your best bet if you’re looking for specialized information, because all of these sites are general and Google can let you know the best places to go to find exactly what you’re looking for.

20 PLACES TO EDUCATE YOUR SELF ONLINE FOR FREE.

20 Places to Educate Yourself Online for Free


It seems like these days you can learn just about anything online for free, but of course some of that information is better than others. The good news is there are plenty of reputable places to educate yourself online for free, and here’s a good 20 of them to get you started.
1. CourseraThe coolest thing about Internet learning is that you can take college courses which in the past were only available to people who forked over immense sums of money to attend elite colleges. Courserabrings a bunch of those classes together into one site, offering nearly 400 courses ranging from Introduction to Guitar from Berklee College of Music to Constitutional Law from Yale.
Courses typically include videos and certain coursework (such as online quizzes) that must be completed in a certain amount of time, as these courses are monitored by a professor. Stop by regularly to see what’s new, or search for topics that interest you can put them on a watch list so you’ll be notified when a new class begins.
2. Khan AcademyHome to more than 3,000 videos on subjects ranging from SAT prep to cosmology, art history to calculus, Khan Academyis a great place to learn. Detailed courses are broken into smaller sections of text or videos for ease of learning that fits into your schedule, and all are self-paced so you can spend as much or as little time with the subject as you like.
You can also leave comments or ask questions if you want more information or if something isn’t clear in the lessons.
3. OpenCourseWareThe OpenCourseWare Consortiumis a worldwide effort to make college and university level course materials accessible for free on the Internet. Search for a specific topic that interests you, or search by language (20 are available) or the source of the coursework.
There are more than 5,000 classes in English alone, covering everything from statistical thermodynamics (Middle East Technical University) to Epidemics in South African History (University of Cape Town) and Creole Language and Culture (University of Notre Dame).
4. ALISON
A global-learning resource with courses in English, French and German, ALISONcovers everything from SAT prep to health and safety courses required in Ireland. There are lessons on everything from study skills to American copyright law, currency exchange to nonprofit fundraising, and general accounting to negotiating when buying a house.
Completion of a course grants you “certification,” which is a British designation, but it’s still kind of fun.
5. MIT Open CoursewareIf you always wanted to attend a big-name school like the Massachusetts Institute of Technology, now you can do the next best thing by taking many of its courses for free from your home on your own time. The MIT Open Coursewaresite posts course materials from a wide variety of classes you can search by department.
Choosing a course will show you when it was originally taught and by whom, and will give you access to the syllabus, course calendar, readings, assignments and study materials. You can download the course materials and work through the course at your own pace.
6. Academic EarthIf you’d like a broader collection of courses than MIT provides, Academic Earthis a great place to look. This free course aggregator has a stunning collection of courses from around 50 universities across the globe. You can search by source or general subject.
Don’t miss the curated playlists on topics such as natural laws, the nature of evil and the economic crisis. The video electives—with subjects like how to take a punch and why World War II made us fat—are lots of fun, too.
7. Open Learning InstituteThe Open Learning Institutefrom Carnegie Mellon University allows access to a handful of course materials so you can learn at your own pace from the same kind of materials and self-guided assessments that would be used in a classroom. Their offerings are limited, but there’s a lot of detail in the coursework. Instructor-led courses are also sometimes available.
8. Open CultureThis site isn’t very pretty, but Open Culturedoes boast a collection of more than 700 downloadable courses, including college-level, certificate-bearing classes, language lessons, educational materials for K-12 and more.
There are also just some interesting links that aren’t to courses but you’ll still learn something from, such as this post on a reading listsuggested by Ernest Hemingway.
9. Open Education DatabaseThe well-designed Open Education Databaseclaims more than 10,000 courses from universities from around the world. Search by topic and you’ll see the number of full courses, as well as which courses have audio lessons, video lessons or mixed media, so you can learn in whatever way you like.
You can also use this site to learn about online and offline schools, should you choose to continue your education in a more formal way.

Friday, October 11, 2013

MBINU ZA KUSOMA NA KUFAULU MTIHANI.

Mbinu za kusoma na kufaulu mitihani darasani. Kusoma kwa bidii ni moja ya sababu kubwa inayomfanya mwanafunzi kufanya vizuri shuleni, licha ya kuongeza bidii kwenye masomo yako kuna mambo mengine ambayo tumezoea kuyaweka pembeni lakini nayo pia wewe kama mwanafunzi ukiyazingatia mambo hayo yatakusaidia kusoma vizuri zaidi na kuongeza ufaulu wako darasani au kwa sisi tulio vyuoni itakusaidia kuongeza GPA yako kuwa ya 3.8 na zaidi. Mimi binafsi nazitumia hizi mbinu na nimefanikiwa kwa kiasi fulani. Ni vyema nawe ukajaribu uone mabadiliko: 1. Tafuta mahali pazuri pa kusomea.(Zingatia ukimya na utulivu) -Sehemu ya kusomea nayo ni chanzo kikubwa cha uelewaji wako wakati wa kusoma. Ni vizuri ukikaa mahali ambapo hakuna kelele au muingiliano wa sauti. Ni muhimu kuwe kimya kwani kutakuongezea umakini katika kusoma. Kama unasomea ndani ya chumba maalum hakikisha madirisha yapo wazi kuruhusu hewa kuingia, muhimu hapa ni kusoma mahali ambapo utakuwa huru hakuna kelele, upepo mkali au usumbufu wa aina yeyote. 2. Muhimu kujua unataka kusoma nini na kwa kina gani. -Kabla ya hujaanza kusoma ni vyema ukajua unataka kusoma nini kwa muda huo, ni kwa kiasi gani unataka uchimbe na kuelewa unachotaka kusoma (do you want to read deep or just shallow). Kusoma kwa kuzingatia mipaka ya unachosoma kutakusaidia usitoke au kwenda mbali na malengo yako ya kile unachotaka kusoma. Kama unasomea mtihani ni vyema ukamuuliza mwalimu wako atatoa mtihani katika mipaka gani ili ujue wapi unatakiwa usome na kutilia mkazo. Angalia pia curriculum ya masomo yako ujue unatakiwa ufahamu mambo gani, hii itakusaidia usome kwa malengo na kujua unatakiwa kuelewa nini kabla ya kuletewa mtihani. 3. Zima simu au iweke kimya(silence)mbali kabisa na mahali unaposomea. -Moja ya vitu vinavyosababisha upoteze shabaha ya malengo yako ya kusoma ni matumizi ya simu wakati ukisoma. Ukiwa na simu karibu ni rahisi kuchat au kuongea na wako rafiki kwenye simu bila kujua huo si muda sahihi wa wewe kufanya hivyo. Epuka kufanya mambo mengine kinyume na malengo yako ya kusoma kwa muda huo.Nidhamu ni muhimu sana katika kusoma. 4. Waambie watu unahitaji muda wako binafsi wa kufanya mambo yako. -Kama unakaa nyumbani au hostel na watu wengi, ni rahisi watu kukusumbua wakati unasoma. Ni heri ukawaambia waheshimu muda wako wa kusoma ili kuepusha usumbufu wa hapa na pale utakaokuharibia muda wako maalum wa kusoma. Kama unatumia saa 2 kusoma hakikisha unatumia muda huo kweli kusoma na sio mambo mengine. Jifunze kusema''HAPANA''unapoona mtu mwingine anataka kukupotezea muda wako wa thamani. Ikiwezekana waambie hutopatikana hadi saa fulani ili wakutafute baadae kama wanashida na wewe. 5. Tumia saa yako vizuri. -Panga muda maalum wa kusoma, licha ya kuwa na ratiba ya kawaida ya darasani kuwa na ya kwako binafsi(private study timetable)ujisomee kila unapopata nafasi. Kama utaanda ratiba rasmi ya kujisomea basi inapendekezwa utumie dakika 30-45 kusoma kisha pumzika kwa dakika 5-10. Usisome sana mpaka ukachoka kufikia macho kuchoka au kichwa kuuma,(read smart and not so hard to make you feel pain). Ndio maana ni muhimu kusoma na kupumzika. Wewe sio mashine bali ni binadamu unahitaji kupumzika kidogo na kuendelea na kazi. 6. Wakati wa kusoma, jitahidi kuondoa mawazo nje ya kile unachosoma. Ukihisi umechoka pumzika kwa kuvuta pumzi ili ukusanye nguvu ya kusoma tena. -Jitahidi kutowaza mambo mengine wakati unasoma isipokuwa yale yanayohusiana na kile unachosoma.Jitahidi sana kuweka mawazo yako darasani uwapo darasani, mimi napenda kuutumia huu msemo''wherever you are be there''. 7. Pata muda wa kutosha kupumzika kwa kulala muda wa kutosha. -Wataalamu wa afya wanashauri ulale kiasi cha saa 6 hadi 8 kwa siku kwa ubora wa afya yako. Kwa kulala kiasi cha muda huo utaupa nafasi mwili hasa ubongo wako, kujikarabati na kupata nguvu upya ya kuendelea na kazi uamkapo asubuhi. Pia ni vizuri ukijiwekea muda maalum wa kila siku wa kulala na wa kuamka ili mwili wako uzoe hali hiyo. Kuna tabia ambayo hata mimi nilipokuwa A-Level nilikuwa naifanya kimakosa ya kutotumia muda vizuri wakati wa mchana na kukesha usiku. Mchepuo niliokuwa nasoma ni PCB kweli masomo ni magumu naweza sema kwa wadogo zangu walioko O-level na A-level jitahidini kusoma sana na kutumia muda wenu vizuri hasa mchana ili usiku angalau upate muda wa kulala angalau masaa matano(5) yani unaweza ukalala saa 7 usiku na kuamka saa 12 asubuhi na mapema. Kama ukilala masaa hayo matano vizuri kabisa basi utakuwa umeupumzisha mwili wako(sleep of good quality ensures good health). 8. Soma mambo mbalimbali yanayohusu masomo yako kwenye vitabu au mahali popote.(maktaba au intanet) 9. Hudhuria vipindi vya masomo(lectures)zote za siku na fanya kazi zote mwalimu atakazowapa. - NAKUTAKIA MASOMO MEMA!...

Wednesday, October 9, 2013

FAIDA YA MATUNDA YAFUATAYO.

Fahamu faida za matunda haya kwa ubora wa afya yako. Kuna faida nyingi za kula matunda licha ya kupenda ladha tamu zamatunda tunayokula. Matunda yana virutubisho vingi ikiwa vitamin A na C hupatikana kwenye matunda mengi ukilinganisha na virutubisho vingine vilivyopo kwenye matunda mengine. Matunda husaidia kupunguza matatizo ya moyo( heart diseases ), stroke ( kiharusi ), shinikizo la damu ( blood pressure ), cholesterol, aina mbalimbali za saratani (cancer ), matatizo ya uwezo wa macho kuona na mengine mengi. Matunda yote yana manufaa kwa miili yetu lakini napenda ujue haya machache kuhusu faida zaapple,parachichi,ndizi,zabibu,embe,chungwa,papainananasi. Matunda haya niliyoyataja huwa tumezoea kuyala lakini naamini wengi wetu hatujui sana kuhusu ni vitu gani tunanufaika kutokana na kula matunda haya. Zijue faida za matunda..... APPLE. -Hupunguza uwezekano wa kupata kisukari ( diabetes ) na pumu (asthma ) -Husaidia kinywa kutokuwa na harufu mbaya ( natural mouth fresher )vilevile apple husafisha meno kila unapotafuna. Je Unajua?Harufu nzuri ya apple hupatikana kwenye maganda/ngozi yake, hivyo ni vyema ukalitafuna pasipo kulimenya kwani vitamin nyingi pia hupatikana kwenye maganda/ngozi ya juu. PARACHICHI. -Ni chanzo cha vitamin E. -Hupunguza kiwango cha cholesterol mwilini. -Kwa afya njema ya moyo wako, kwenye sandwich au mkate tumia parachichi badala ya siagi. Je Unajua?Watoto hupenda sana kula parachichi kwasababu ni laini na pia mafuta ya parachichi husaidia katika kukuwa kwa mtoto na kuwa mwenye afya bora. NDIZI. -Ni chanzo cha vitamin B6 na madini ya potassium. -Licha ya kuwa na ladha nzuri, ndizi zina madini mengi ya potassium ukilinganisha na matunda mengine ambayo husaidia kupunguza ongezeko la shinikizo la damu ( blood pressure ). Je Unajua?Watu wenye aleji na material ya mpira( rubber latex ) wanaweza pia kuathirika kwa aleji ya ndizi kwakuwa mpira na ndizi vyote zina aina moja ya protini. ZABIBU. -Ni chanzo cha madini ya manganese. -Hupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya moyo kwa kusaidia kushusha kiwango cha shinikizo la damu ( blood pressure ) -Huepusha magonjwa ya aina mbalimbali za saratani kwa kuzuia usambaaji wa seli za saratani ya titi ( breast cancer ), tumbo ( stomach cancer ) na utumbo ( colon cancer ). Je Unajua?Unaweza gandisha zabibu za kijani na nyekundu na ukazitumia kama barafu ( ice cubes ) kwenye kinywaji chako upendacho. EMBE. -Ni chanzo cha vitamin A na E. -Vitamin Ailiyopo kwenye embe husaidia kuboresha macho yako kwa kukuwezesha uweze kuona vizuri. Pia husaidia kupunguza uwezekano wa upofu kwa wazee kwa kuimarisha macho yao. Je Unajua?Embe ni tamu sana likiwa limeiva lakini pia likiwa bichi unaweza kutumia embe kutengenezea kachumbari, achali, chutney na salad. CHUNGWA. -Ni chanzo cha vitamin C na madini ya potassium. -Chungwa lina vitamin inayojulikana kama‘’folate’’( B-Group Vitamin ) ambayo husaidia katika kujengeka kwa ubongo wa mtoto kwa mama mjamzito. -Chungwa lina kemikali zinazojulikana kama‘’hesperidin’’ambazo hupunguza kiwango cha cholesterol kwenye damu. Je Unajua?Sehemu nyeupe ya chungwa ( gome lililo ndani ya chungwa ) lina thamani ya vitamin karibia sawa na nyama ya chungwa hivyo ni vyema kula chungwa lote baada ya kumenya maganda yake. PAPAI. -Ni chanzo cha vitamin A na C. -Papai lina enzyme ijulikanayo kama‘’papain’’ambayo husaidia katika kusaga au mmeng’enyeko wa chakula. -Pia vitamin A iliyopo kwanye papai husaidia husaidia kuboresha afya ya ngozi yako. Je Unajua?Mbegu nyeusi za papai zinaweza kuliwa japo kuwa ni chungu lakini unaweza kuzisaga na salad kwa kutumia blender badala ya pili. NANASI. -Nanasi lina enzyme asilia ijulikanayo kama‘’bromelain’’ambayo husaidia kuvunjavunjaprotini hivyo husaidia katika mmeng’enyeko wa chakula. -Vilevile enzyme yabromelainhusaidia kupunguza ukuaji wa seli za saratani na kuchochea uponaji wa vidonda kwa haraka. Kwa hayo machache hapo juu unaona ni jinsi gani matunda yalivyo muhimu kwa kujenga afya zetu na kutumika kama dama kwa miili yetu. Napendekeza upende kula angalau tunda moja kwa siku kwa uboreshaji wa afya yako. Kama una chochote cha kuongeza kuhusiana na mada hapo juu, tafadhali usisite kutoa maoni yako!