Imetoka toleo la pili
Matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2012 na Kidato cha Sita mwaka 2013 yatumike katika kufanya majaribio na hivyo wataalamu wa mifumo wa NECTA wafanye kazi hiyo na kuleta mapendekezo yao kabla ya uamuzi wa mwisho kufikiwa. Hili lilifanyika (angalia Kiambatansho A Jedwali la 3 na la 4). Baada ya majumuisho ya uchambuzi wa maoni ya wadau, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI walikutana na kushauriana nini kifanyike katika kupanga viwango vya alama za mitihani na ufaulu. Katika kikao hicho, Mawaziri, Makatibu Wakuu wa Wizara hizo na Kamishna wa Elimu, walipata nafasi ya kupitia maoni ya wadau, kujadili na kupendekeza viwango vipya vya alama za ufaulu vitakavyotumika katika mitihani ya Kidato cha Nne ya mwaka 2013 na Kidato cha Sita ya mwaka 2014. Viwango vilivyopendekezwa vilizingatia pia maoni yaliyotolewa na wadau hapo juu na hivyo kuridhia kwamba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi sasa itangaze utaratibu wa alama za mitihani ya taifa kwa Kidato cha Nne mwaka 2013 na Kidato cha Sita kuanzia mwaka 2014. 4. VIWANGO NA UTARATIBU KUANZIA MWAKA 2013 KWA KIDATO CHA NNE NA MWAKA 2014 KIDATO CHA SITA
Baada ya kufanya tathmini ya maoni mbalimbali ya wadau, misingi ifuatayo ilizingatiwa katika maamuzi kuhusu makundi ya alama na muachano wake:
3
a) Alama zitakazotumika zitakuwa A, B, C, D, E na F. Muachano wa alama kati ya kundi moja hadi jingine utafanana, isipokuwa tu pale ambapo itaonekana kuna sababu na hakuna athari za kuwa na muachano tofauti na ule ambao umetumika katika makundi mengine. b) Makundi ya alama hayatakuwa na clusters isipokuwa pale ambapo itaonekana kufanya hivyo kunaleta tija katika kupata picha ya wahitimu kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Kwa mantiki hii makundi ya alama A, C, D, E na F yabaki na cluster moja moja bali kundi la alama B litakuwa na clusters mbili. Kundi la kwanza litakuwa la wale ambao wamepata alama kati ya 50 mpaka 59 na litaitwa B na lingine litakuwa la wale ambao wamevuka uwigo wa 50 hadi 59 na kuelekea uwigo wa 60 hadi 74 na hili litaitwa B+ (angalia jedwali hapo chini). (ii) Pamoja na kuwa na muachano wa alama 26 kama jedwali linavyoonesha hapo chini, alama A kwa miaka mingi imekuwa ikianzia alama 75 hadi 100 na kwamba pamoja na uwigo huo bado wanaofaulu kwa kiwango hicho ni wachache sana. Kwa mantiki hii, hakuna haja ya kubadilisha uwigo ila juhudi ziendelee katika ufundishaji na ujifunzaji ili kiwango cha ufaulu kiongezeke na kupata wanafunzi wengi zaidi wanaofaulu katika kundi hili. (iii) Pia, pamoja na kuwa na muachano wa alama 20 kama jedwali linavyoonesha hapo chini kwa miaka mingi, huko shuleni mwanafunzi aliyepata alama 21 na hadi 30 alihesabiwa kuwa na ufaulu wa chini kabisa au hafifu kwa kiwango cha alama D na ingawa ilikubalika ufaulu wa aina hiyo kwa mazingira ya nchi yetu unaridhisha. Alama F ilikuwa ni kwa wale waliopata chini ya hapo. Hivyo, alama F itaendelea kuwepo na itaanzia alama 0 hadi 19 na E itaanzia alama 20 hadi 29 na D 每 30 -39. Lengo la muundo huu ni kuwa alama mbalimbali, isipokuwa kwa makundi machache, zianzie kwenye 0 yaani 0, 10, 20, 30, 40 na kuendelea badala ya kuanzia kwenye moja yaani 1, 11, 21, 31, 41 na kuendelea. Hii ni kwa ajili ya kuleta mtizamo unaofanana katika ngazi mbalimbali za elimu ambapo kwa sasa ngazi ambazo siyo za elimu msingi na sekondari zinatumia muundo wa kuanzia kwenye 0 badala ya 1. c) Uwigo wa jumla wa alama kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita utaendelea kuwa wa alama 0 hadi 100 na kila kundi katika uwigo huu limepewa tafsiri kwa ajili ya kuamua mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya mwanafunzi kulingana na malengo ya mtihani husika. Kimsingi, tafsiri zifuatazo zitakatumika (i) Alama A itakuwa na maana ya ufaulu uliojipambanua (distincion or outstanding performance), (ii) Alama B+ itakuwa na maana ya ufaulu bora sana (excellent performance), (iii) Alama B itakuwa na maana ya ufaulu mzuri sana ( very good perfomance), (iv) Alama C itakuwa na maana ya ufaulu mzuri (good performance); (v) Alama D itakuwa na maana ya ufaulu wa wastani (low performance), (vi) Alama E itakuwa na maana ya ufaulu hafifu (very low performance), na (vii) Alama F itakuwa na maana ya ufaulu usioridhisha (unsatisfactory performance). Wataalamu katika maeneo mbalimbali ya elimu na ulimwengu wa kazi, kwa kushirikiana na Wizara, watatoa maana ya tafsiri hizi kiutendaji katika maeneo yao kulingana pia na mahitaji yao.
Inaendelea toleo la mwisho
No comments:
Post a Comment