Imetoka toleo la kwanza
c) d)
Mara nyingi mitihani ya kundi (a) mpaka (c) inaunda kundi la CA wakati ile ya kundi (d) inaunda kundi la mtihani wa mwisho (final examination ama FE). Ili upimaji ufanyike, ni lazima mtihani uwe na muundo stahiki wa alama (grading structure). Muundo huu hupangwa kulingana na maamuzi ya uwigo gani utumike. Kwa mfano, ngazi nyingi za elimu hutumia uwigo wa alama 0 hadi 100 na kuna sehemu nyingine uwigo wake ni 0 hadi 50. Kwa miaka mingi, uwigo wa alama kwa Kidato cha Kwanza hadi cha Sita hapa nchini umekuwa wa alama 0 hadi 100. Pia, kimsingi, kuna mifumo miwili ya upangaji wa viwango vya ufaulu duniani katika kutunuku ufaulu. Baadhi ya nchi au mifumo hutumia viwango vinavyobadilika (flexible grade ranges) ambavyo hupangwa kwa kutegemeana na ufaulu wa watahiniwa katika somo husika. Nchi au mifumo mingine hutumia viwango visivyobadilika (fixed grade ranges) ambavyo hupangwa na nchi au mifumo husika vitumike kama kipimo cha ufaulu kwa masomo mbalimbali. Katika mitihani ya elimu ya sekondari, Tanzania ilifuata mfumo wa kutumia viwango vinavyobadilika (Flexible Grades) kuanzia mwaka 1973 hadi 2011. Hata hivyo, kwa madhumuni ya kuwawezesha wadau kujua viwango vya ufaulu vinavyotumika katika kutunuku matokeo ya mitihani ya taifa ya sekondari, Serikali iliamua kuanza kutumika kwa utaratibu wa viwango vya ufaulu visivyobadilika (Fixed Grades) kuanzia mwaka 2012. Suala kubwa lililokuwa limebaki lilikuwa ushirikishwaji wa wadau ili kuliweka wazi suala hili na kila mdau aweze kujua mfumo na miundo yake ikiwemo mfiko wa alama na maana yake katika kila kundi la alama. 3. MAONI YA WADAU Kabla ya kuwashirikisha wadau, Wizara iliunda Kamati ndogo kupitia taarifa mbalimbali na kutoa mapendekezo ya jinsi muundo wa alama katika mitihani ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita unavyoweza kuwa. Kamati hii ilifanya kazi hiyo na kutoa mapendekezo yake ambayo nayo yalipelekwa kwa wadau kwa ajili ya majadiliano zaidi. Wadau mbalimbali walishirikishwa katika kutoa maoni juu ya utaratibu mpya wa upangaji wa viwango vya alama na ufaulu. Wadau hao ni pamoja na jukwaa la taasisi za elimu ya juu, chama cha wakuu wa shule za Sekondari nchini (TAHOSSA) wakuu wa vyuo vya ualimu vya umma, wamiliki na wakuu wa shule na vyuo visivyo vya Serikali (TAMONGSCO), wakaguzi wa shule kanda, muungano wa wanafunzi wa Taasisi za elimu ya juu nchini (TAHLISO), viongozi wa Wizara ya Elimu na
2
Mafunzo ya Amali Zanzibar, walimu, wanafunzi, wazazi, maafisa elimu Mkoa, Wilaya pamoja na maafisa taaluma wao, wadau kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wanataaluma na Wanasiasa. Maoni hayo yalikusanywa kupitia mikutano mbalimbali na kwa njia ya madodoso. Wadau wote walikubaliana kwamba mfumo nyumbufu wa alama siyo mzuri na hivyo taifa lihamie kwenye mfumo wa alama mgando katika mitihani mbalimbali. Kwa jumla wadau walipendelea utaratibu wa upangaji makundi ya alama kwa kuzingatia muachano wa alama kumi kumi kutoka kundi moja hadi jingine. Hali hii inasaidia kuondokana na muundo ambao unawalundika wanafunzi wengi na mara nyingi wasiofanana katika uwezo wao kielimu katika kundi moja. Aidha wadau walipendekeza kiwango cha chini cha ufaulu mzuri kuwa Cna hii iwe sawa na alama 40. Kwa upande wa alama endelevu, wadau pia walipendelea kuwa CA ichangie asilimia 40 katika matokeo ya mitihani ya kuhitimu ngazi husika ya masomo. Hata hivyo, wadau walitoa angalizo kwamba ni vyema kukawa na muundo na utaratibu mzuri wa kuzipata alama endelevu za mwanafunzi. Muundo na utaratibu huo unaweza kutumia mitihani ya Kidato cha Pili na ile ya mock ya Kidato cha Nne ambayo huwa inaandaliwa, kusimamiwa na kusahihishwa kwa umakini na weledi wa kutosha. Pia mwalimu naye asinyimwe fursa ya kuchangia kwenye alama za maendeleo ya mwanafunzi na hivyo matokeo ya mitihani ya muhula wa kwanza na wa pili ya Kidato cha Tatu nayo yanaweza kutumika kama sehemu ya alama endelevu. Hatua kali zichukuliwe kwa mtu na taasisi yoyote itakayobainika kukiuka maadili katika usimamiaji na uwasilishaji wa matokeo ya mitihani. Ili kuwaimarisha wanafunzi katika tasnia ya kufikiri na kuandika, kila mwanafunzi afanye project na matokeo yake yatumike kwenye alama endelevu. Projects hizi zianze kuandaliwa wakati mwanafunzi akiwa Kidato cha Tatu na kukamilishwa katika muhula wa kwanza Kidato cha Nne. Kuhusu muundo wa madaraja, wadau wengi walishauri muundo uliopo sasa wa madaraja uimarishwe ili kuanza kutumia muundo wa wastani wa alama katika ufaulu (Grade Point Average ama GPA). Muundo huu huwa ni rahisi kueleweka na kuuandaa kuliko muundo wa madaraja. Lakini pia, kwa kutumia muundo wa GPA inakuwa rahisi katika kukadiria uwezo wa mwanafunzi kielimu na kufanya maamuzi mbalimbali ikiwemo kuendelea na masomo katika ngazi mbalimbali za elimu. Mwisho, wadau walikubalianana pendekezo la muundo wa alama lijaribiwe katika mfumo halisi (actual testing) ili kujua faida na athari zake katika mfumo wa elimu kama pendekezo hilo likitekelezwa.
Inaendelea
No comments:
Post a Comment