Umefanya nini kipya wiki iliyopita?
Leo ni jumapili siku ya mwisho kwa wiki hii kulingana na kalenda tunayotumia. Siku ya mwisho wa wiki ni siku ya kutathmini yale yote uliyofanya, mategemeo yako na mipango yako ijayo. Hakuna kitu kizuri kama kuwa mtu mwenye kusonga mbele vizuri na maisha yako, raha zaidi ni pale mambo yote yanapokwenda sawa kama ulivyopanga.
Haitapendeza kupitisha wakati wako muhimu kwa siku au wiki pasipo kujiuliza mambo kadhaa kuhusu wewe mwenyewe kama:
*.Umefanya kitu gani kizuri wiki iliyopita?
*.Je wiki jana na wiki hii inayoisha umejiimarisha mapungufu yako?
-Labda ulikuwa unaumwa na sasa umepona.
-Labda ulikuwa na hasira sana lakini sasa una amani na mwingi wa furaha.
-Labda ulikuwa mzito wa kutekeleza kazi zako muhimu lakini sasa wewe yu mchapa kazi.
-Labda uligombana na mtu lakini sasa mmepatana kwa kusameheana na kuboresha uhusiano wenu.
*.Je umepanga kufanya kitu gani cha kukunufaisha wiki ijayo?
*.Je umejipongeza kwa lolote zuri ulilofanikisha kwa kuona umepiga hatua na unastahili kujivunia?
*.Je umebuni nini cha kukukuza au kuongeza maarifa yako?
-Labda umebuni mtindo wako mpya wa mavazi unaouona unakupendeza na kuonekana mtanashati kwa watu.
-Labda umejifunza kupika chakula kitamu cha aina yake.
-Labda umebuni mpango mpya wa kufanya kazi zako kwa urahisi hapo awali.
-Labda umesoma kitabu cha kukuongezea ujuzi kazini.
Ukifanya wakati wako unaotumia kwa wiki kuhesabika, utakuwa mtu bora kila wiki unapotathmini maendeleo ya maisha yako. Jiboreshe, kuwa mbunifu na tegemea mambo mazuri hakika utakuwa mtu mwenye furaha na neema tele zitakuzunguka.
WORDS OF THE DAY:‘’To be strong one should have faith in one's self and trust in one's strength. It takes strong heart to overcome every hardship that will come. Have faith in yourself and believe.”
No comments:
Post a Comment