Tumia uwezo wako wa kufikiri.
Nguvu ya pekee uliyonayo ni ya‘’KUFIKIRI’’.Tambua kuwa una uwezo mkubwa wa akili ambapo kama ukitumia akili yako vizuriunaweza ukabadilisha maisha yako kufikia mahali bora kimaendeleo unapopotaka.
Kila mtu anaweza kujifunza namna ya kushirikisha akili na kile anachotaka kufanyakwa ufahamu wa kutaka kushinda analokusudia. Labda unatakauhuru, amani, upendo , mali au afya njema na kwa kuwa una nia thabiti ni wazi kuwa utafanikiwa.
Watu wengi hushindwa kufanikiwa katika mambo yao kwaajili ya kukosa dhamira ya kweli kwa kile wanachotaka. Kama utaweka ufahamu wa kufanikiwa kwenye akili yako ni rahisi kwako kuona fursa nyingi za kupata unachotafuta.
Tumeumbwa tuishi maisha tunayoyataka kwa uhuru, afya njema, kutafuta na kupata mali ili maisha yetu kuwa rahisi lakini kama tu tutaweka nia na jitihada endelevu zitakazotupelekea kufaulu na kushinda changamoto kabla ya kufanikiwa. Nasema hivi nikiwa na maana mafanikio huja kwa kuwa na fikrachanya za kuamini utafanikiwakama utaweka juhudi zako binafsi na kuwa na moyo wa kuendelea kutafuta.
Fikra zetu ni zana za kimaendeleo katika maisha yetu zinazoweza kukufanya uwe na faraja ,amani, uwezo wa kupata mali au umasikini. Kama maisha yako sio kama unavyotegemea yawe basi ujue kuna tatizo la kimazingira linalokukwamisha kufanikiwa mfano- Mazingira duni kiuchumi,migogoro ya kifamilia ,ukosefu wa elimu na maarifa au fikra ambazo sio sahihi za kutotambua rasilimali zinazokuzunguka na hujitendei haki kutojitambua na kubadilisha maisha yako.
Kama unataka badilisha maisha yako badilika kwanza kimawazo na mambo mengine yatafuata muelekeo unaotaka. Una uwezo wa kuchagua utafikri kufikiri, hakuna mtu mwenye mamlaka ya kukufanya kutofikiri utakacho bali ni wewe tu. Ni jukumu lako kufikiri utakavyo kwakuwa wewe ndio rubani wa fikra zako na maisha yako.
Chukua muda wa kutosha kutafakari mambo yatakayo kuletea majibu mazuri. Kamwe usifikiri mambo ambayo hutaki yatokee maishani mwako. Usifikiri mambo ambayo hayanatija mfano mambo ambayo unajua hayawezekani kwako. Kama hutaki kuwa mjinga basi kamwe usifikiri kuwa wewe ni mjinga bali jiamini wewe ni mwenye akili na uliye bora. Kama wewe hutaki kumpoteza mpenzi wako basi kamwe usifikiri kumwacha au kuachwa na yule umpendaye.
Kwa kufikiri vizuri mambo haya yanaweza kukubadilisha kitabia .
-Usiwe mtu wa kuongea hovyo bila kutafakari unachokiongea, kabla ya kuongea jua unataka kuongea nini.
-Kabla ya kutenda chochote,fikiri kwanza. Kwa kufanya hivi utaepuka kufanya makosa yanayoweza kuepukika.
-Kabla ya kuanza safari jua mwanzo na mwisho wa safari. Hapa nina maana usianze kufanya shughuli yoyote kabla ya kujua mwisho wake.
Yote ya yote usiyape nafasi mawazo ya kukubomoa, chagua kufikiri kwa busara na umakini kuhusu maisha yako. Fikra ni nguvu . Kila unapofikiri unaongeza uwezo wako wa ufahamu.Je ni nini au ni kipi cha kufkiri ? Jawabu unalo wewe mwenyewe.
Kila kitendo na hisia ni kichocheo kitokanacho na fikrazako. Mwisho tumia muda wako mwingi kufikiria mamba ambayo yanawezekana na kukujenga kimaendeleo. Ni swala tu la kufanya mazoezi na kutafakari ili kuongeza ufahamu wako.
REMEMBER:‘’Once you ‘ve learned and known to master your thoughts, you become the master of your life.’’
No comments:
Post a Comment