Thursday, January 16, 2014

Sababu Ya Wewe Kuamka Asubuhi na Mapema.

Wengi wetu huwa tunakuwa macho kwa muda mrefu wakati wa usiku badala ya kupumzika kwa kulala. Kuna sababu nyingi za mtu kuchelewa kulala zikiwemo kuendelea kufanya kazi aliyopanga kumaliza kwa siku hiyo, matatizo ya kutopata usingizi na mambo mengine kadha wa kadha.
Kutolala usiku au kuchelewa kulala bila sababu ya msingi sio vizuri kiafya. Utafiti unaonyesha watu wanaopata kupumzika vizuri na kuamka asubuhi na mapema huwa na furaha na afya njema. Vilevile utafiti wa hivi karibuni unaeleza kwamba watu ambao huchelewa kulala au ambao hawapumziki kwa muda wa kutosha hupata matatizo ya ''utendaji kazi mbaya wa moyo (bad cadiac functioning) yakiwemo mapigo mabaya ya moyo (heart rate) na shinikizo la damu (blood pressure).
Utafiti pia unaonyesha kwamba muda wa asubuhi (alfajiri) ni muda pekee mzuri wa kuweza kufanya mambo yako kwa umakini na ufanisi mkubwa kwa kuwa wakati huo ubungo unakuwa hauna msongo wa mawazo.
''This is Robin Sharma a leadership mentor but also acts as a motivator, here he gives you some tips on how you should discipline yourself to get up early in the morning and become a great perfomer of your daily tasks.''
Kwa kujua hivyo, nakushauri ujitahidi kufanya kazi zako muhimu wakati wa asubuhi kukiwa kumetulia kuliko mchana ambapo kuna pilikapilika au mihangaiko mingi. Pia jitahidi sana kumaliza kazi zako wakati wa mchana ili usiku upate muda wa kutosha kupumzika (kulala).
Haya ni mambo machache ya kujaribu….
1.Wakati wa mchana tumia muda wako vizuri.
-Tekeleza au fanya kazi zako mchana ili kuepusha kufanya kazi wakati wa usiku na kuchelewa kulala.
2. Epukana na kelele au sauti za kukusumbua wakati wa usiku.
-Sio kila siku wewe ni mtu wa kuhudhuria sherehe au party za usiku, unahitaji kupumzika ili uondoe uchovu uliotokana na mishughuliko ya siku. Mwili wako hujitibu kwa kujijenga na kujiweka sawasawa wakati ukiwa umelala hivyo usingizi ni tiba ya maradhi mengi madogomadogo.
3. Kuwa na tabia ya kulala muda maalum kila siku.
Jijengee mazoea ya kulala muda maalum kila siku. Mwili wako utazoea na kukufanya uamke asubuhi na mapema ukiwa mwenye nguvu nautulivu wa akili.
Wataalamu wa usingizi (sleep experts) wamekadiria inachukua wiki3 hadi mwezi 1 mtu kujenga mazoea ya kuamka asubuhi na mapema mwenyewe bila kushtuliwa na alamu au mtu wingine. Anza leo na wewe kulala mapema na kuamka asubuhi na mapema kwa afya njema ya kiakili na kimwili.
NENO LA SIKU:
"Morning is an important time of a day, because how you spend your morning can often tell you what kind of day you're going to have."- Lemony Snicket

No comments:

Post a Comment