Friday, January 3, 2014
Faida saba (7) za kupenda kujisomea.
Kupenda kusoma ni tabia nzuri ambayo kila mtu ni muhimu awe nayo. Tunalazimika kusoma kwasababu asili ya mazingira yetu kuna mambo mengi ya kujifunza licha ya matukio mengi ya kidunia yanayotokea kila siku. Ukiachilia mabadiliko ya kijamii (namna tunavyoishi), kiteknolojia, kisiasa na ya kiuchumi yanayotokea kila mahali ulimwenguni bado kuna sababu muhimu sana ya sisi kupenda kujisomea hata pale tunapokuwa hatupo shuleni (vyuoni). Inapendeza na kuleta hamasa pale mtu anaposoma mambo ya kujiendeleza yeye binafsi kwaajili ya kujijenga na kuimarisha maisha yake mbali na vile vitu anavyosoma au alivyosoma darasani kama taaluma yake ya kikazi. Ikiwa bado unakuwa mzito katika kupenda kusoma tafadhali soma hizi faida hapo chini kisha utajifunza kitu kuhusu kusoma.
1. Noa maarifa (panua ufahamu na uelewa wako) kwa kusoma.
Usomaji wa vitabu utakufanya ujue mambo mengi sana katika mazingira yako. Hebu tafakari kama leo utasoma kitu fulani cha kukusaida au kubadilisha maisha yako, bila shaka utakuwa umeingiza kitu cha ziada katika maisha yako kwa siku ya leo.Mfano:Kwa siku ya leo umesoma namna ya kumhudumia mtu aliyepata ajali (iwe ni ajali kazini, nyumbani, barabarani n.k)kwa kumpatia huduma ya kwanza. Kwa kujifunza namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu anayehitaji msaada utakuwa umesoma kitu muhimu sana cha kuweza kukusaidia popote pale na wakati wowote ule kwakuwa utakuwa unatambua na kufahamu nini cha kufanya. Kila siku soma chochote kile cha kukuongezea maarifa ya maisha na ipo siku utatumia ujuzi ulionao kujisaidia mwenyewe au mtu mwingine kutatua matitizo.
2. Kusoma kunaongeza utashi wa kutamka maneno vizuri.
Unaposoma sana ndivyo unavyoona na kujua mengi, ni vigumu kwako kushindwa kusoma kabisa au kutamka maneno vizuri ikiwa unafahamu asilimia kubwa ya maneno. Kama wewe ni msomaji mzuri wa vitabu au unaperuzi sana kwenye mtandao wa intaneti utakuwa umesoma maneno mengi sana kiasi cha kuweza kutamka vizuri maneno mengi bila shida yoyote. Huwezi kuwa unafahamu maneno yote bali utajiongezea uwezo kutambua maneno na kukisia vizuri namna yanavyosomwa na kutamkwa. Fanya hivyo na utaona unapata maendeleo katika kuongea.
3. Kusoma kunaongeza uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu.
Ukisoma na kuvutiwa na kitu ulichosoma bila shaka utahifadhi kumbukumbu akilini au kwenye karatasi ya kile ulichosoma kwa manufaa ya baadae. Ukiwa umesoma hadithi yenye mkasa wa kuburudisha, matukio yaliyotokea mahali fulani au historia ya kitu fulani, kumbukumbu hizo za kile ulichosoma zitahusisha mambo mengine ili uweze kukumbuka kitu chenyewe. Hivi ndivyo mfumo wa kumbukumbu unavyofanya kazi.Mfano:Ili uweze kuvuta taswira ya hadithi uliyosoma kwenye kitabu fulani ni lazima utakumbuka picha ya kitabu chenyewe ndipo ukumbuke ndani mwa kitabu hadithi yenyewe ilikuwa inahusu nini. Ubongo unafanya kazi nyingi sana katika mwili wa mwanadamu, kwa kadri unavyojaza kichwa chako na mambo mengi mazuri ndivyo unavyoufanya ubongo uboreshe kumbukumbu halisi ya kile unachotaka ukumbuke.
4. Kusoma kunaongeza uwezo wa kufikiri.
Unaweza soma kitabu chenye maelezo mengi ya kimafumbo au misamiati ya kukutaka kufikri ili uweze kuelewa, wakati ukiendelea kusoma utakuwa unajiuliza maswali mengi ni yapi majibu ya hicho unachosoma. Kwa kutafakari ili ufumbue kilichoandikwa utapanua fikra zako na hivyo kuongeza uwezo wako wa kutambua, kufahamu na kuelewa mambo kwa haraka. Faida moja wapo ya kuongeza uwezo wako wa kufikiri ni kuweza kutatua matatizo unayokumbana nayo katika mazingira yako kwa usahihi na ufanisi mkubwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment