Njia tano (5) za kupunguza uzito.
Kutaka kupunguza uzito wa mwili ni nia nzuri ya kuweka mwili wako katika afya njema. Hapa tujikite zaidi kwenye uzito wa mwili usio wa kawaida. Sababu kuu mbili zinazosababisha mtu awe na uzito uliozidi kuliko kawaida ni ulaji mbaya wa vyakula na kutofanya au kufanya mazoezi kidogo kwa kiwango ambacho si stahiki. Unaweza kujiuliza,utajuaje kuwa uzito wako ni mzuri au umezidi uzito?
Tumia kanuni yaBody Mass Index (B.M.I), kanuni hii inatumika kutafuta uwiano pekee kati ya urefu/kimo katika mita na uzito wako wa mwili katika kilogramu.
Utakapo kokotoa uwiano wako wa urefu/kimo na uzito wako wa mwili kwa kutumia hiyo kanuni hapo juu, utaweza kujua upo katika hali gani yani unaweza kujijua kama unauzito mdogo wa afya mgogoro (underweight), upo katika uzito mzuri wa afya bora au una unene uliokithiri (obesity). Baada ya kukokotoa na kupata jibu jitathmini mwenyewe kwa kujilinganisha na ufafanuzi huu. Kama upo katika hali ya afya njema utapata jibu kati ya 18.5 - 25. Ikiwa uwiano wako utakuwa chini ya 18.5 (inaashiriwa kuwa underweight) au zaidi ya 25 (inaashiria kuwa na unene wa kupindukia yani obesity) hivyo ni vyema umwone daktari akupe ushauri wa lishe na tiba ya mazoezi.
Tumia hizi njia 5 kukusaidia kupunguza uzito wa mwili na utaona matokeo mazuri kila baada ya wiki.
1. Kunywa maji kwa wingi (kiasi cha lita2 kwa siku). Kabla ya kula kunywa angalau glasi 1 ya maji, hii itakusaidia ujisikie umeshiba hivyo utakula kiasi cha kawaida kinachokutosheleza.
2. Usipende kula sana vyakula vilivyopikwa na mafuta mengi. Mfano: Chips, Mishikaki, Mayai na vingine vya asili hiyo. Ukila sana vyakula vyenye mafuta mengi vitakuongezea mafuta mwilini na kukusababishia unene ambao sio mzuri kwa afya yako.
3. Punguza kula vyakula vya wanga (mchele, mikate, tambi n.k) badala yake penda kula mbogo mboga za majani na matunda kwa wingi. (Juisi ya malimao ni nzuri zaidi kwasababu husaidia kuyeyusha mafuta tumboni)
4. Fanya mazoezi mpaka utokwe na jasho angalau kwa dakika 30 kila siku. Kama upo busy sana na huwezi kufanya mazoezi kila siku basi jitahidi kufanya mazoezi angalau mara 3-4 kwa wiki kwa dakika 60. Unaweza kukimbia au kuendesha baiskeli kwa kilometre chache (2KM itakuwa vizuri zaidi), au tembea kwa angalau dakika 45 kwa siku, fanya mazoezi ya ruka kamba uwapo nyumbani nakadhalika. Mazoezi husaidia kuchoma calories mwilini na kufanya mwili wako kuwa mwepesi. Unapotokwa na jasho ni namna ya asili ya kuondoa sumu na uchafu mwilini.
5. Pumzika vya kutosha, mwili hutumia chakula cha ziada kilichopo mwilini wakati ukiwa umepumzika. Mfano mzuri ni wakati umelala, mwili hutumia kiasi cha ziada cha chakula kilichopo mwilini kwaajili ya kujikarabati hivyo huzuia mkusanyika wa chakula kisichotumika mwilini ambao sio mzuri
No comments:
Post a Comment