BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013
Imetolewa Na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
25Februari, 2014
UFAFANUZIWA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMUKUHUSU MATOKEO YAMTIHANI WAKIDATO CHA NNE(CSEE)2013
Baraza la Mitihani la Tanzania lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013 tarehe21/02/2014. Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Baraza limekuwa likipokea maswali mbalimbali yanayoashiria kuwa baadhi ya wadau wa elimu hawakuelewa vizuri kuhusuViwango vya Ufaulu(grade ranges),alama yachiniya ufaulu(pass mark) naUfaulu wajumlawa mtahiniwa(overall performance). Baraza la Mitihani linapenda kutoa ufafanuzi katika mambo hayo kama ifuatavyo:
1.
Viwango vya ufaulu (grade ranges) ni makundi ya alama yanayopangwa ili kuwaweka pamoja watahiniwa wenye uwezo unaofanana katika somo husika na kuwatofautisha na watahiniwa waliopo katika kundi jingine. Makundi haya hupangwa ili kuwawezesha wadau kutambua namna watahiniwa walivyotawanyika katika viwango mbalimbali vya umahiri wa somo husika. Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likitumia makundi Matano (5) kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2012. Aidha, Kuanzia Mtihani wa Kidato cha Nne(CSEE)2013, Baraza limeanza kutumia utaratibu waMakundi Saba (7)ambayo niA, B+, B, C, D, EnaF. Utaratibu huu umelenga kupunguza mlundikano mkubwa wa alama katika kundi moja. Mgawanyo wa makundi hayo ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali la 1.
Jedwali Na 1:Viwango vya ufaulu vilivyotumikakatika Matokeo ya CSEE 2013.
Kundi
Gredi
Alama
Idadi ya Pointi
1
A
75 - 100
1
2
B+
60 - 74
2
3
B
50 - 59
3
4
C
40 - 49
4
5
D
30 - 39
5
6
E
20 - 29
6
7
F
0 - 19
7
Aidha, Idadi ya makundi ya ufaulu hutofautiana kati ya nchi na nchi kulingana na mahitaji ya nchi husika. Kwa mfano; Kenya wana makundi Kumi na mbili (12), Malawi Tisa (9), Uganda Tisa (9), Nchi za Afrika magharibi (Nigeria, Ghana, Siera Leone na Liberia) makundi Tisa.
1.
Kwa kuzingatia viwango vya ufaulu vilivyoainishwa katika makundi saba yaliyopo kwenye Jedwali na 1, kiwango cha chini cha ufaulu ni gredi D na kiwango cha juu cha ufaulu ni Gredi A. Mtahiniwa atakuwa amefaulu somo husika iwapo atapata gredi D na kuendelea. Aidha, mtahiniwa aliyepata gredi E na F atakuwa hajafaulu somo husika.
1.
Madaraja ya ufaulu yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20 (1)-(6) cha Kanuni za Mitihani kinachoelekeza kuwa Ufaulu katika daraja la Kwanza hadi la Tatu upangwe kwa kuzingatia jumla ya alama (Points) na Ufaulu katikaDaraja la Nne unapangwa kwa kuzingatia ufaulu wa chini aliopata mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo yasiyopungua mawili au ufaulu kwa kiwango kisichokuwa chini ya Gredi C katika somo moja. Hivyo, madaraja yaliyotumika ni kama yanavyoonekana kwenye Jedwali la 2.
Jedwali 2: Madaraja yaliyotumika katika CSEE 2013
Daraja
Pointi
I
7 - 17
II
18 - 24
III
25 - 31
IV
1.
Ufaulu katika somo moja kwa kiwango kisichokuwa chini ya Gredi C au
2.
Ufaulu katika masomo yasiyopungua mawili katika Gredi D
0
Alama chini ya D mbili
1.
Kwa mujibu wa Kanuni za Mitihani, ufaulu wa somo katika Gredi A hadi C utakuwa ni ufaulu wa “Credit” na Gredi D itahesabika kuwa ni “pass”. Aidha Gredi E na F zitakuwa alama za kufeli.
1.
Baraza la mitihani la Tanzania linapenda kutoa taarifa kwamba ufafanuzi wa sifa za kujiunga na mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutumia mfumo huu mpya wa madaraja utatolewa na mamlaka husika ambapo Kamishna wa Elimu atalitolea ufafanuzi zaidi.
Imetolewa Na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
Friday, February 28, 2014
Saturday, February 22, 2014
Friday, February 21, 2014
Monday, February 10, 2014
Faida nne (4) za kufanya mazoezi ya kukimbia.
Wakati tatizo la unene likiongezeka kwa kasi katika jamii yetu, watu bado wamekuwa wakijisahau kufanyisha mazoezi miili yao licha ya kupata ushauri wa afya katika vyombo vya habari (redioni, T.V, magazetini) na sehemu nyingine mbalimbali wanapotoa huduma za afya. Elimu ya lishe bora pamoja na ile ya kuishi vizuri kwa afya bora ni elimu muhimu sana kwa kila mtu kufahamu. Ukiwa na maarifa ya namna ya kula vizuri na kufanya mazoezi kwa afya, bila shaka utakuwa na upeo mkubwa wa kujua na kuelewa ni jinsi gani chakula na mazoezi yalivyomuhimu kwa maendeleo mazuri ya mwili wako na afya kiujumla.
Kuna sababu nyingi za mtu kutofanya mazoezi inaweza kuwa ni maradhi aliyonayo, kutoweka kipaumbele kufanya mazoezi ya mwili, ukosefu wa maarifa nakadhalika lakini swali muhimu la kujiuliza wewe mwenyewe hapa ni, je unasababu yeyote ya msingi ya wewe kutofanya mazoezi? Sababu nzuri ya wewe kutofanya mazoezi inaweza kuwa ni huna muda lakini ni jambo la busara kufikiri je ni kweli unakosa angalau dakika 30 kwa siku kukimbia na kupata muda mwingi wa kutosha wa kulimbikiza mafuta mwilini yanayochangia uzito na unene wa mwili?
Zoezi la kukimbia lina manufaa mengi, hizi hapa ni baadhi ya faida.
1. Hurefusha maisha.
Uchunguzi wa kisayansi umethibitisha kuwa kukimbia angalau kwa saa chache kwa wiki sio tu kutakufanya uwe mchangamfu na kuongeza utendaji wako wa kazi bali pia huongeza miaka ya kuishi.
2. Huimarisha moyo na mapafu.
Kwa mtu wa kawaida mwili hutumia oxygen mara 10 zaidi wakati wa kufanya zoezi rahisi la kukimbia ukilinganisha na akiwa amekaa. Mtu anapofanya zoezi la kupasha mwili kwa muda huimarisha mfumo wa moyo wa usukumaji damu hivyo moyo na mapafu pia hufanya kazi zake kwa ufanisi.
3. Huboresha utendaji kazi wa ubongo na kuongeza uwezo wako wa kufikiri.
Ikiwa inaaminika mazoezi ni afya, licha ya kuwa mazoezi yana manufaa mengi kiafya pia inaaminika mazoezi ya kukimbia husababisha ubongo kuzalisha homorne iitwayo ‘’endorphin’’ ambayo kemikali hii huibua hisia za furaha na kumfanya mtu awe katika hali ya kuwa na raha na mwenye mawazo chanya. Sio tu kwamba mazoezi haya yatakufanya ujihisi katika hali ya furaha kwa muda bali yatakufanya pia uongeze ujasiri wako wa kujiamini na kujikubali mwenyewe hivyo pia utapunguza msongo wa mawazo na matatizo mengine yanayosababishwa na kuchoka kwa ubongo.
4. Hupunguza uzito wa mwili na mafuta mwilini.
Sote tunajua unapofanya mazoezi, baada ya muda utajisikia kuchoka, kutokwa na jasho, kuhema sana nakadhalika. Haya yote ni matokeo baada ya kufanya zoezi la kukimbia, unapofanya maozezi unachoma calories mwilini na hatimaye kupunguza mafuta. Ikiwa utakuwa unafanya mazoezi ya kukimbia ipasavyo na kwa malengo ni rahisi kwako kuona mabadiliko ya mwili wako baada ya wiki chache. Kama wewe ni mnene na una uzito mkubwa wa mwili huu ndio wakati wako wa kuanza kufanya mazoezi ya kukimbia.
Kujua zaidi:Soma Njia za kupunguza unene wa mwili wako.
Kumbuka kama una matatizo yoyote ya kiafya kama pumu, maradhi ya moyo, mapafu, matatizo ya mifupa, misuli na mengineyo ni vyema ukamuona daktari kwa ushauri kabla ya kuanza kufanya mazoezi haya.FANYA MAZOEZI KWA AFYA BORA!
Sunday, February 9, 2014
Mambo sita (6) ya kukusaidia kuboresha afya yako leo.
1. Punguza kutumia kilevi (pombe) badala yake ongeza kunywa chai, maji na juisi asilia ya matunda.
2. Punguza kula nyama (hasa nyama nyekundu za wanyama waliwao) badala yake ongeza ulaji wa mboga mboga za majani.
3. Punguza kutumia sukari nyingi au kula vyakula vyenye sukari nyingi badala yake ongeza ulaji wa matunda kwa wingi.
4. Punguza utumiaji wa chumvi nyingi au kula vyakula vyenye chumvi nyingi badala yake ongeza utumiaji wa siki (vinegar)
5. Punguza kuwa na wasiwasi au hofu ya aina yeyote ile badala yake pumzisha mwili wako kwa kuongeza ubora wa usingizi wako kwa kulala mahali safi, tulivu, penye hewa ya kutosha na kwa muda wa kutosha. (saa 6 mpaka 8)
6. Punguza kuwa na hasira kila wakati badala yake ongeza kutabasamu na kucheka kwa furaha kila unapofurahishwa.
Saturday, February 1, 2014
Zijue faida za tunda tikitimaji kwa afya njema.
Tikitimaji ni tunda lenye ladha nzuri na tamu sana. Lina maji kwa 92% na sukari kwa takriban 6%. Licha ya kuwa juisi ya tikitimaji au tunda lenyewe hukata kiu kwa haraka bado kuna faida nyingine nyingi za kiafya tunazonufaika kutokana na tunda hili. Je ulikuwa ukijua tikitimaji lina sukari asilia yenye kukupatia nguvu mwilini, vitamin A, C, E, D, niacin na madini kama ya chuma (iron), calcium, magnesium, manganese, potassium, phosphorus, zinc nakadhalika. Faida nyingine ya tunda hili ni kwamba halina mafuta kabisa hivyo ukila tikitimaji huwezi kuongeza mafuta au cholesterol mwilini.
Angalia hii video hapa chini yenye maelezo ya namna ya kutengeneza juisi ya tikitimaji na faida za tunda lenyewe.
Hebu tuangalie manufaa ya kiafya tunayopata kutokana na tikitimaji.
1. Huepusha saratani.
Tikitimaji ni moja ya tunda lenye wingi wa kemikali iitwayo ‘’lycopene’’ ambayo pia inapatikana katika matunda mengine pamoja na mboga za majani. Kemikali hii inaaminika kuwa ni kuzuizi na tiba asilia ya saratani ya tezi dume (prostrate cancer) kwa wanaume. Saratani ya aina hii inazidi kushamiri ulimwenguni hivyo ikiwa wewe ni mwanaume wa shoka na hutaki kuwa mmoja wa wagonjwa wa saratani ya aina hii (prostate cancer) ni vyema ukafanya tikitimaji kuwa kimbilio lako.
2. Hupambana na maambukizi mbalimbali yaletayo magonjwa.
Kwa kula tikitimaji unaongeza uwezo wa mwili wako kuwa imara na kujikarabati kwa haraka. Mfano katika ugonjwa wa ngozi, tikitimaji huboresha ngozi yako na kufanya ionekane yenye afya na yenye kunawiri. Hii ni kwasababu tikitimaji lina kemikali iitwayo ‘’amino acid citruline’’ ambayo baadae hubadilisha na kuwa katika mfumo wa kemikali nyingine ‘’arginine’’. Arginine huchochea uzalishwaji wa chembechembe nyeupe za damu ambazo huwa kama kinga katika eneo lenye jeraha. Licha ya hivyo Vitamin C inayopatikana kwenye tikitimaji huongeza kinga ya mwili. Kazi nyingine ya vitamin C ni kuponya vidonda kwakuwa ina uwezo wa kukarabati na kutengeneza sehemu iliyoharibika kwa ugonjwa. Kama wewe una tatizo la vidonda kutopona kwa haraka, tikitimaji pamoja na matunda mengine yenye wingi wa vitamin C ndio chaguo lako.
3. Husafisha figo.
Kwa kuwa asilimia kubwa ya tikitimaji ni maji hivyo maji hayo hufanya tunda hili kuwa ni dawa ya asili inayosaidia figo kuondoa taka mwilini kupitia mkojo. Pia tikitimaji husaidia ini kuvunjavunja na kuondoa sumu mbalimbali na hivyo kurahisisha utendaji mzuri mwili kujisafisha na hatimaye kuwa wenye afya njema.
4. Husaidia kudhibiti ongezeko la shinikizo la damu.(High blood pressure)
Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanasayansi wa chakula dawa, wamebaini kuwa kemikali zinazopatikana katika tikitimaji ‘’L-citrulline’’ ambayo ina uhusiano wa karibu na kemikali nyingine iitwayo ‘’L-arginine’’ zote mbili kwa pamoja zinaaminika kusaidia kupunguza shinikizo la damu (high blood pressure) na hivyo kuepusha maradhi mengine yanayohusiana na moyo.
5. Huongeza hamu na nguvu ya kufanya mapenzi.(Viagra asilia)
Uchunguzi uliofanywa na wataalamu mbalimbali wa afya ukiwemo utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Havard Marekani umebaini sio tu kwamba tikitimaji huboresha mfumo wa mzunguko wa damu wa moyo bali hata pia huongeza hamu na nguvu ya kufanya mapenzi kwa wanaume. Kemikali inayojulikana kama ‘’citruline’’ katika tikitimaji inasaidia kuchochea mishipa ya damu ku-relax na kuruhusu damu izunguke kwa ufanisi wake na kuleta muhamko wa uume kama inavyofanya kazi dawa ya kuongeza nguvu ya kufanya mapenzi (Viagra). Tikitimaji pia linaaminika kuongeza nguvu ya mwili kwa asilimia 23%, hii ni kwasababu tikitimaji lina madini ya magnesium ambayo husaidia katika utengenezwaji wa nguvu mwilini (adenosine triphosphate ATP ) na vitamin B6 ambayo huchochea uzalishaji wa hormone ya kukufanya ujisikie mwenye furaha (dopamine hormone).
Angalia hii video clip hapa chini upate maelezo kuhusu tikitimaji kama Viagra asilia kutoka kwenye jarida la afya la Havard University.
Ndugu msomaji, leo tumeona ni jinsi gani tunda hili la tikitimaji lilivyo na faida nyingi katika miili yetu. Ushauri wangu ni kwamba kuliko kunywa soda au kilevu chenye sukari nyingi ni bora kama ukiweza tengeneza juisi yako mwenyewe ya tikitimaji ukiwa nyumbani kwa manufaa ya afya yako na familia yako kiujumla.
NAKUTAKIA AFYA NJEMA!
Subscribe to:
Posts (Atom)