Thursday, August 8, 2013
MUANDAMO WA MWEZI
Kwa nini waislam hatusherehekei mwezi mmoja?KAMA kuna wakati
ambao umoja baina
yao basi hakuna
wakati muafaka kama
huu tulio nao. Lakini
kutafuta njia za
kutufikisha katika
umoja huo, sisi
tumekuwa
tukijishughulisha zaidi
na mambo madogo
madogo yenye
ikhitilafu baina yetu,
ambayo hayana faida
yoyote kwetu,
isipokuwa
kutuongezea uhasama
na utengano.
Sala ya Idi ni Sunna lakini
umoja wa Waislamu ni
wajibu. Sisi tumeacha
kulishughulikia lile jambo la
wajibu, ambalo ni umoja wa
Waislamu na tumeamua
kutowafikiana katika kusali
sala ya Idi siku moja bila
ya kuwa na sababu yoyote
ya msingi.
Maswali ya lini tuanze
kufunga Ramadhani na lini
kufungua pamoja na swali
la saumu ya Arafa yameleta
ikhtilafu kubwa baina ya
wanazuoni wetu. Kundi moja
linadai kwa kuwa dunia ni
moja na mwezi ni mmoja,
basi mwezi ukiandama
katika nchi yoyote
ulimwenguni inabidi nchi
nyingine zote zifuate.
Itaendelea......
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment