Sunday, January 4, 2015

Tangazo la Mtihani wa Kidato cha Nne 2015


TANGAZO BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato Cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) Mwezi Novemba 2015 kwamba usajili umeanza rasmi tarehe 01 Januari 2015. Watahiniwa watakaojisajili katika kipindi cha kawaida yaani tarehe 01 Januari 2015 hadi 28 Februari 2015 watalipa ada ya Shilingi 50,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 30,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Maarifa (QT). Watahiniwa watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01 Machi 2015 hadi tarehe 31 Machi 2015 watalipa ada ya Shilingi 65,000/ kwa Kidato cha Nne na ada ya Shilingi 40,000/- kwa mtihani wa Maarifa (ada pamoja na faini). Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani: www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo wanavyokusudia kufanyia mtihani kuchukua namba rejea (Reference Number). Wakuu wote wa vituo nchini wamekabidhiwa namba rejea na watazigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo. Aidha waombaji watapaswa pia kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au M-Pesa kabla ya kujisajili kwani hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kulipa ada ya mtihani. Waombaji wote wazingatie kwamba kipindi cha usajili kitafungwa rasmi tarehe 31 Machi 2015 Imetolewa Na: KATIBU MTENDAJI

Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2015 Haijabadilika.


BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA RATIBA YA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2015 HAIJABADILIKA Baadhi ya watu wamekuwa wakitumiana ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wenye kupotosha kwamba Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ametangaza kuwa Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2015 utafanyika kuanzia tarehe 2 hadi 25 Machi 2015 badala ya tarehe 4 hadi 27 Mei 2015. Aidha, ujumbe huo umetoa sababu kuu ya mabadiliko ya ratiba ya mtihani kuwa inatokana na mwingiliano wa ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwafahamisha watahiniwa wa Mtihani wa Kidato cha Sita 2015 na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kuupotosha umma wa watanzania. Baraza linapenda kusisitiza kuwa ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2015 HAIJABADILIKA na kwamba Mtihani huo utafanyika kuanzia tarehe 4 hadi 27 Mei 2015 kama ilivyopangwa awali, Baraza la Mitihani linaomba wadau wazipuuze taarifa hizi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwa kuwa zina lengo la kupotosha umma. Imetolewa na, AFISA HABARI NA UHUSIANO

Thursday, December 4, 2014

Utaratibu wa kutunuku matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na cha sita kwa kutumia mfumo wa GPA.


BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA UTARATIBU WA KUTUNUKU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE NA CHA SITA KWA KUTUMIA MFUMO WA GPA 1. Mfumo wa Wastani wa Pointi (Grade Point Average - GPA) Huonesha wastani wa pointi alizopata mtahiniwa katika masomo aliyofaulu katika mtihani wake. GPA hutokana na masomo saba (07) aliyofaulu vizuri zaidi mtahiniwa katika Mtihani wa Kidato cha Nne na masomo matatu (03) ya tahasusi katika Mtihani wa Kidato cha Sita. Mtahiniwa aliyefanya masomo pungufu ya 07 kwa CSEE au pungufu ya 03 kwa ACSEE, atafaulu katika kiwango cha ※Pass§ endapo atapata angalau Gredi D katika masomo mawili au gredi C, B, B+ au A katika somo moja. Uzito wa Gredi A= 5, B+ = 4, B = 3, C = 2, D = 1, E = 0.5 na F = 0. Utaanza kutumika kupanga madaraja ya ufaulu katika Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2014 na Kidato cha Sita (ACSEE) 2015. 2. Ukokotoaji wa GPA ya Mtahiniwa Hufanyika kwa kuchukua jumla ya uzito wa gredi katika masomo saba (07) aliofanya vizuri kwa Mtihani wa Kidato cha Nne na matatu (03) ya tahasusi kwa Mtihani wa Kidato cha Sita na kugawanya kwa idadi ya masomo. Ukokotoaji huo huzingatia kanuni ifuatayo: Jumla ya Uzito wa gredi za masomo -----------------------------------------------Idadi ya Masomo GPA = Masomo yatakayotumika katika ukokotoaji wa GPA ya mtahiniwa ni yale ambayo amefaulu; yaani amepata Gredi A, B+, B, C au D. 3. Muundo wa Madaraja Kwa Kutumia Mfumo wa GPA Katika mfumo wa Wastani wa Pointi (GPA) kutakuwa na madaraja manne ambayo ni Distinction, Merit, Credit na Pass. Daraja la juu la ufaulu ni Distinction na la chini ni Pass kama ilivyoainishwa katika Jedwali lifuatalo: DARAJA Distinction Merit Credit Pass Fail CSEE 3.6 每 5.0 2.6 每 3.5 1.6 每 2.5 0.3 每 1.5 0.0 每 0.2 ACSEE 3.7 每 5.0 3.0 每 3.6 1.7 每 2.9 0.7 每 1.6 0.0 每 0.6 Mfano; Mtihani wa Kidato cha Nne, mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Civics (A), History (B+), Geography (B+), Kiswahili (B), English (C), Physics (C), Chemistry (C), Biology (C) na Mathematics (E) atakuwa na jumla ya pointi 22 kwenye masomo saba aliyofanya vizuri. Idadi hiyo ya pointi ikigawanywa kwa idadi ya masomo saba (07), Mtahiniwa huyu atakuwa na Wastani wa Pointi (GPA) 3.1 na atatunukiwa daraja la Merit. Katika Mtihani wa Kidato cha Sita mtahiniwa aliyepata ufaulu wa Physics (A), Chemistry (B+), Biology (A), Basic Applied Mathematics (D) na General Study (A) atakuwa na jumla ya pointi 14 kwenye masomo ya tahasusi (PCB). Idadi hiyo ya pointi ikigawanywa kwa idadi ya masomo matatu (03), mtahiniwa atakuwa na Wastani wa Pointi (GPA) 4.7 na atatunukiwa daraja la Distinction. 4. Manufaa ya kutumia Mfumo wa Wastani wa Pointi (GPA); Kuwa na mfumo wa kutunuku matokeo wa aina moja katika ngazi zote za mafunzo kuanzia Elimu ya Msingi hadi Elimu ya Juu; Matokeo yaliyo katika mfumo wa wastani wa pointi kwenye cheti yatarahisisha kazi ya udahili wa watahiniwa unaofanywa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) katika ngazi za juu za mafunzo na Mfumo wa wastani wa pointi (GPA) ni rahisi kueleweka kwa wadau wa kada mbalimbali kwa sababu hutoa tafsiri yenye kuonesha mtahiniwa aliye na GPA kubwa ndiye aliye na matokeo mazuri kuliko aliye na GPA ndogo. Maelezo zaidi kuhusu GPA yanapatikana katika tovuti ya Baraza la Mitihani ( www.necta.go.tz).

Tuesday, December 2, 2014

Utaratibu wa kutunuku matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na cha sita kwa kutumia mfumo wa GPA.


Utaratibu wa kutunuku matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na cha sita kwa kutumia mfumo wa GPA Bofya hapa kupakua

Saturday, July 12, 2014

TANGAZO ACSEE 2015.

TANGAZO
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi,Mei2015 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kilianza rasmi tarehe1 Julai,2014hadi tarehe30 Septemba, 2014kwa ada ya Shilingi50,000/=.Aidha kuanzia tarehe1Oktoba,2014hadi tarehe31Oktoba,2014waombaji watajisajili kwa ada ya Shilingi65,000/-(ada pamoja na faini). Waombaji wotewanasisitizwakuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz.Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mtihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewaburena kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au M-pesa.
Imetolewa Na:
Kaimu Katibu Mtendaji Baraza laMitihanilaTanzania.

Tomorrow May Never Come

''Life's changing every moment'' ''Life is noW a shade...'' ''Iife is noW sunshine'' ''Every moment on earth...'' ''Iive Iife to the fuIIest'' ''Whatever time you have is yours...'' ''for tomorroW might never come'' ''Life's changing every moment'' ''Life is noW a shade...'' ''Iife is noW sunshine'' ''Every moment on earth...'' ''Iive Iife to the fuIIest'' ''Whatever time you have is yours...'' ''for tomorroW might never come'' ''Someone to Iove you With aII his heart...'' ''is difficuIt to come by'' ''ShouId there be someone Iike that...'' ''he's the one for you, be sure'' ''His hand...'' ''you must take'' ''For aII you knoW...'' ''tomorroW might never be'' ''Every moment on earth...'' ''Iive Iife to the fuIIest'' ''Whatever time you have is yours...'' ''for tomorroW might never come''